Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,516
Nikiri kuwa tangu jana kumekuwa na mjadala juu ya alichokisema Wakili Msomi Albert Msando pale Serena Hotel.
Wakili Msando, ulitangaza kuwa kutakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari pale Serena Hotel. Siku ilipotimu,waandishi na wasio waandishi wakaja kukusikiliza. Ukajitokeza kama Wakili wa akina-Zitto Kabwe. Ukatoa taarifa. Naiona Taarifa yako kama taarifa tata kwakuwa ina mchanganyiko usio rasmi na ambao haukutegemewa.
Kwanza, taarifa yako imebeba 'taarifa kwa umma'. Kwamba, Zitto Kabwe na wenzake, badala ya kujibu tuhuma zao 11 walizopewa na chama chao, wao wameamua kukata rufani kwenda Baraza Kuu la CHADEMA.
Pili, taarifa yako imebeba 'rufani'. Umeainisha sababu kuu mbili za rufani ya akina-Zitto. Ukazikoeza sababu hizo kwa kutaja vifungu mbalimbali vya Katiba ya CHADEMA.
Tatu, taarifa yako inabeba 'utetezi'. Baada ya kuainisha sababu za rufani na vifungu vyake, ukaenda mbele zaidi na kuwsilisha utetezi wa Zitto juu ya tuhuma zinazomkabili. Kuna mahali umesema: 'ZITTO HAUSIKI'. Eti kwakuwa hajatajwa moja kwa moja na Waraka. Kimsingi, huu ni utetezi.
Nne, taarifa yako ikabeba 'kanusho' . Tena ni kanusho lililotokana na habari za sikia-sema (hearsay). Ukakanusha kuhusu kuhusika kwa Zitto kwa vurugu za Kigoma. Kwamba, hausiki na kupigwa mawe Dr. Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA. Wakili Msomi mwenzangu MsandoAlberto, hujui uzito wa sikia-sema? Wewe ulikuwepo Kigoma wakati Dr. Slaa anapigwa mawe? Kuwa makini Wakili Msomi.
Tano, taarifa yako imebeba 'malalamiko'. Mwanzo hadi mwisho wa taarifa yako ya Serena ni kulalamika tu. Umelalamikia utaratibu,sababu,maneno yasemwayo na kadhalika.
Je, kulikuwa kweli na haja ya kuitisha mkutano Serena na kutoa 'mchanganyiko' huu? Wakili msomi wenzangu MsandoAlberto, tafadhali washauri wateja wako wafuate taratibu za chama chao. Acheni sarakasi zisizo na tija.
Mnaweza kuwa mna hoja lakini, mnaweza kuiharibu kwakuwa mnapoitolea hapastahili. Kwa hili la sasa, si umma wala vyombo vya habari vinavyoweza kuwa msaada wenu. Msaada pekee mlionao ni Katiba yenu.
Si busara kutoa kila mchakato wa ndani ya chama nje. Msipokuwa makini, mtachokwa na kuhukumiwa kwa jazba na hasira ya viongozi wenu. Watasema: 'liwalo na liwe', msifike huko, hakuna haja ya mambo hayo!