Wakili Albert Msando hakushirikishwa na Mhe.Zitto katika kusaini kiapo kwa AG?

Makala Jr

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,395
1,110
Kila mtu ana swali lake kuhusu sakata la Mhe.Zitto kusaini kiapo cha kukiri kutokuwa na majina ya Watanzania walioficha fedha haramu nchini Uswisi.

Hakika Mhe.Zitto Kabwe amejidhalilisha/amedhalilishwa sana na sakata hili kwa kuonekana mzushi, mwongo, na mnafiki asiye na woga wa kuwadanganya Watanzania.

Kwa vyovyote vile, Zitto alishurutishwa kusaini kiapo hicho kwa mujibu wa AG;sheria ilichukuwa mkondo wake kupitia sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Inawezekana Mhe.Zitto anajua kitu kuhusu mabilioni ya Uswisi (na sisi wananchi baadhi yetu tunajua kwani vijisenti vya Chenge hatukuvisikia?).

Lakini kinachotia doa harakati za kuwasaka wahusika kwani katika sheria za utandawazi ukweli huwa kando kwanza bali ushahidi (alioukana Zitto) hupewa kipaumbele.

Kama Zitto alisaini ili kutunza siri (EVASION), je alimshirikisha wakili wake Albert Msando? Ikawaje Zitto aligusia suala hilo hali anajua alisaini?
 
Kuna Habari kwamba hata yeye Zitto ana pesa Uswisi hivyo aliamua kulichukua hili soo kuwafanya watu wengine wasijitokeze kufuatilia, Zitto ni kichwa jamani
 
Last edited by a moderator:
wanaomshobokea zitto kwa sasa inabidi wakapimwe akili kama zipo sawasawa. Maana yeye ameshajidhisha kwamba akili hana

Usalama kwanza. Inaelekea kuna kitu kimemtisha sana Zitto. Hata mama yake alikaririwa akishukuru kuwa kuvuliwa kwake kwa nyadhifa zake CDM kumemuepushia majanga makubwa yaliyokuwa yakimnyemelea.
 
Kookolikoo; Unataka kutuaminisha kwamba alikiri kutokuwa na majina wala kuwajua wahusika kwasababu za kiusalama? By the way, ikawaje alijidumbukiza kwenye aibu ya kulizungumzia jambo ambalo alishindwa kutoa ushirikiano kwa kamati iliyoundwa?
 
Mkuu Msando kaomba kwa ZITTO amsaidie kuwa msemaji wake ktk kukiuka katiba na maamuzi ya CC ili apate kaumaarufu.Yule anatafuta atoke vp,zitto ampi hata mia.

ndo maana yake..Umaarufu ndo chanzo cha huyu msando kuomba kula japo vijiko 2 kwenye sahani ya ZZK.
 
Zitto na Mtikila wote zafanana ,
tuanze na Zitto, anapenda sifa na hoja binafsi, ni muongo na haaminiki tena huenda alipotaja wizara zao nafasi zao wakamfuta na kumpoza kama alivyo Mtikila aliposema Rostam sio raia akaaidi kutoa ushaidi kuwa ni raia wa Irani, alipopozwa akala kona.
 
Kila mtu ana swali lake kuhusu sakata la Mhe.Zitto kusaini kiapo cha kukiri kutokuwa na majina ya Watanzania walioficha fedha haramu nchini Uswisi.

Hakika Mhe.Zitto Kabwe amejidhalilisha/amedhalilishwa sana na sakata hili kwa kuonekana mzushi, mwongo, na mnafiki asiye na woga wa kuwadanganya Watanzania.

Kwa vyovyote vile, Zitto alishurutishwa kusaini kiapo hicho kwa mujibu wa AG;sheria ilichukuwa mkondo wake kupitia sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Inawezekana Mhe.Zitto anajua kitu kuhusu mabilioni ya Uswisi (na sisi wananchi baadhi yetu tunajua kwani vijisenti vya Chenge hatukuvisikia?).

Lakini kinachotia doa harakati za kuwasaka wahusika kwani katika sheria za utandawazi ukweli huwa kando kwanza bali ushahidi (alioukana Zitto) hupewa kipaumbele.

Kama Zitto alisaini ili kutunza siri (EVASION), je alimshirikisha wakili wake Albert Msando? Ikawaje Zitto aligusia suala hilo hali anajua alisaini?

Ukiambiwa kuwa alishauriwa na wanasheria wake kuwa asitoe orodha hiyo chini ya kiapo utabadili mtizamo juu ya kauli ya AG?

Tofauti na kutowapatia hiyo orodha chini ya kiapo, bado kuna ushahidi na ushauri ambao Zitto aliutoa ili kuisaidia tume. Sasa mbona AG hakuyasema hayo? Au alijua mnataka kusikia hayo?

Watanzania bado wanaukumbuka ufisadi wa rada na orodha ya waliotuhumiwa kupatiwa mgawo kupitia akaunti zao zilizopo visiwa vya Jersey, akiwepo Mh. Chenge na Dr. I Rashidi. Hata kama mahakama haikuthibisha uhusika wao bado hawakukana kuwa na akaunti kwenye visiwa hivyo. Je hizo akaunti zilifunguliwa kwa mujibu wa sheria zetu? Je hivyo vijisenti /mabilioni yaliyoingizwa humo yalitokana na kipato halali kinachotambuliwa na tume ya maadili?

Hata mtandao wa waandishi wa habari ulimwenguni unaofuatilia mambo haya umeshaanza kutoa majina ya watanzania wenye mabilioni Uswisi akiwepo Yusuf Manji. Lakini mwenye jukumu la kuchunguza kama fedha hizo zilipatikana kihalali au la, si ZZK bali ni tume/serikali.

Mbona hamjiulizi ni kwa nini Zitto alishindwa kuwataja hata hawa.? Je hawajui? Na hao wanaotaka orodha ili wawataje, mbona wanashindwa kuwataja hata hawa?

Hivi umeshajiuliza legal implication kwa Zitto kusema kuwa anawajua watanzania walioficha hizo fedha nje ya nchi.? Tena chini ya kiapo?

Sasa kulikuwa kuna haja gani ya kuunda hiyo tume kama serikali ilikuwa inategemea ushahidi wa kiapo cha Mtanzania mmoja (ZZK)? Tume inapaswa kuacha siasa bali ifanye kazi yake (uchunguzi)
 
Zitto ni Tapeli wa Kisiasa, amekuwa akitumia uenyekiti wake kwenye kamati za bunge kublack mail wakurugenzi wa mashirika ya uma, hata katika hili alitaka kublack mail mafisadi, wamemzidi ujanja.

Pia alikuwa anatumia kinga ya kwenda kupeleleza mapesa uswis kwenda kusafisha pesa zake alizokuwa anapewa na ccm katika mkakati wake wa kukipaka chama rangi ya ugaidi na usaliti mwingine wa kukiangamiza, thanks Lema and tundu, kwa hili nalo wamemnasa.

sasa analazimika kwenda kuomba msamaha kwa Mola wake, asamehewe madhambi yake mengi sana, ili aweze kupata ujasiri wa kuendeleza mapambano dhidi ya ccm hasa sasa kwa sababu atakuwa amekwisha tambua ccm wako tayari hata kufanya nini ili wabaki madarakani.

ama aongezewe ulinzi, kuna hatari akajisuicide.
 
Hapo ndo tujiulize kwenye mambo yanayohusu chama kilichomfikisha hapa alipo mbio kuchukua mwanasheria kumkingia kifua lakini kwenye mambo ya maslai ya Taifa anakuwa mpole na kukubali kusaini kiapo tena kwa siri na wana CCM kuficha ukweli! Jamani mwenye macho haambiwi ona huyu jamaa ni traitor na yuko katika ule mpango wa kukismbaratisha CHADEMA kaeni chonjo jamani! Ubaya haulipwi kwa uzuri
 
Labda alijua ni upepo tu,na utapita.Huku akijua maCcm yatamsaidia,sasa wameona hana dili maana Chadema wameanza kutoa nguo zake,soon watamtoa na yeye mwenyewe!hivyo wanaanza kufunga mlango wao ili akikurupushwa huko,asije akaingia kwao nyoka mkubwa,ameshatumika tupa kule.
 
Kila mtu ana swali lake kuhusu sakata la Mhe.Zitto kusaini kiapo cha kukiri kutokuwa na majina ya Watanzania walioficha fedha haramu nchini Uswisi.

Hakika Mhe.Zitto Kabwe amejidhalilisha/amedhalilishwa sana na sakata hili kwa kuonekana mzushi, mwongo, na mnafiki asiye na woga wa kuwadanganya Watanzania.

Kwa vyovyote vile, Zitto alishurutishwa kusaini kiapo hicho kwa mujibu wa AG;sheria ilichukuwa mkondo wake kupitia sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Inawezekana Mhe.Zitto anajua kitu kuhusu mabilioni ya Uswisi (na sisi wananchi baadhi yetu tunajua kwani vijisenti vya Chenge hatukuvisikia?).

Lakini kinachotia doa harakati za kuwasaka wahusika kwani katika sheria za utandawazi ukweli huwa kando kwanza bali ushahidi (alioukana Zitto) hupewa kipaumbele.

Kama Zitto alisaini ili kutunza siri (EVASION), je alimshirikisha wakili wake Albert Msando? Ikawaje Zitto aligusia suala hilo hali anajua alisaini?

Mkuu Msando ni Wakili kwa ajili ya Maamuzi ya Vikao vya Chadema tu huko hawezi Kabisa na wala hana ujanja huo hata Dogo Mwenyewe anajua hilo.
 
Back
Top Bottom