kinepi_nepi
JF-Expert Member
- Aug 16, 2007
- 869
- 235
Kamanda wakili Albert Msando ni diwani wa kata ya mobogini moshi vijijini kwa tiketi ya chadema. Nilijua jina hili nilipofika mabogini kwa shughuli mbalimbali nikiwa na kombati za chama, mara vijana wengi wakanizunguka na kuniuliza kama ninamfahamu Albert Msando diwani wao. Nikawaambia simfahamu kwani sijawahi kukutana naye na nilikuwa sipo kipindi cha uchaguzi.
Wakaniambia ni mwaka sasa tangia tumchague hatujamwona. Nilisikitika sana, wakaniambia ni wakili wa kujitegemea na ofisi zake walikuwa wanadhani zipo Arusha hivyo anaishi AR.
Nikataoa ripoti kwa viongozi wa chama moshi kuwa tuna diwani ambaye hajulikani alipo, na ofisini hafiki.
Mabogini ni kijiji kinachotegemea zao la mpunga kutokana na mradi wa mwaka 1985 chini ya ufadhili wa japan. Zao hili linaathirika kwa kiasi kikubwa kwa ukosefu wa maji, maji ya umwagiliaji hayatoshi. Mradi huu haukuzingatia uvunaji maji na uhifadhi wake kutokana na mahitaji.
Nimeshauri mara nyingi kujengwa kwa mabwawa makubwa mara baada ya vyanzo vya maji yanaoyoweza kukidhi umwagiliaji huu kwa msimu. Gharama za mabwawa haya ni ndogo ukilinganisha na hasara wanayopata wakulima ambapo kuna wananchi zaidi elfu arabaini kwenye kata ya Mabogini na Kahe wanaotegmea kwa kiwango kikubwa kilimo hiki.
Mashamba haya kwasasa yanakosa uzalishaji kama ulivyoakinishwa hapo awali. Siioni mtu yeyote kwa dhati anayetaka kutatua tatizo hili kwa kina. Nilimtafuta sana Msando ili niweze kumshauri jinsi ya kutatua tatizo hili kama diwani ambaye wapiga kura wake ni waathirika wakubwa.
Mabogini ni kata iliyotengwa na mbunge wa Moshi vijijini Cyril sijui nani. Barabara inayounganisha mabogini na pasua then Mjini moshi iko kama imepigwa bomu. Barabara hii ni kiunganisha kizuri sana cha Moshi mjini, pasua, Mabogini, Chekereni, Kahe na Kileo. Barabara hii wanakaa wakzi zaidi ya elfu 50 wanaunganisha inayotaka kuwa jiji la moshi.
Mipango miji bado ni shaghalabaghala haieleweki.
Kwanini ninamlaumu Wakili Albert Msando, Kamanda huyu ni kijana msomi hivyo wananchi walifikiri wanaingiza chachu ya mabadiliko fikra na maono mapya. Namuomba akimaliza kutetea wateja wake najua ni kazi kwani ndio kazi ya mwanasheria kutetea wahalifu ili watendewe haki, arudi kwenye kata yake tutatue matatizo ya wananchi.
Kwa Niaba ya wakazi wa Mabogini-tunamtafuta Diwani.
Msando ni diwani kwa tiketi ya CDM