Wakili Albert Msando diwani wa kata ya Mabogini

kinepi_nepi

JF-Expert Member
Aug 16, 2007
869
235
Kamanda wakili Albert Msando ni diwani wa kata ya mobogini moshi vijijini kwa tiketi ya chadema. Nilijua jina hili nilipofika mabogini kwa shughuli mbalimbali nikiwa na kombati za chama, mara vijana wengi wakanizunguka na kuniuliza kama ninamfahamu Albert Msando diwani wao. Nikawaambia simfahamu kwani sijawahi kukutana naye na nilikuwa sipo kipindi cha uchaguzi.

Wakaniambia ni mwaka sasa tangia tumchague hatujamwona. Nilisikitika sana, wakaniambia ni wakili wa kujitegemea na ofisi zake walikuwa wanadhani zipo Arusha hivyo anaishi AR.

Nikataoa ripoti kwa viongozi wa chama moshi kuwa tuna diwani ambaye hajulikani alipo, na ofisini hafiki.

Mabogini ni kijiji kinachotegemea zao la mpunga kutokana na mradi wa mwaka 1985 chini ya ufadhili wa japan. Zao hili linaathirika kwa kiasi kikubwa kwa ukosefu wa maji, maji ya umwagiliaji hayatoshi. Mradi huu haukuzingatia uvunaji maji na uhifadhi wake kutokana na mahitaji.

Nimeshauri mara nyingi kujengwa kwa mabwawa makubwa mara baada ya vyanzo vya maji yanaoyoweza kukidhi umwagiliaji huu kwa msimu. Gharama za mabwawa haya ni ndogo ukilinganisha na hasara wanayopata wakulima ambapo kuna wananchi zaidi elfu arabaini kwenye kata ya Mabogini na Kahe wanaotegmea kwa kiwango kikubwa kilimo hiki.

Mashamba haya kwasasa yanakosa uzalishaji kama ulivyoakinishwa hapo awali. Siioni mtu yeyote kwa dhati anayetaka kutatua tatizo hili kwa kina. Nilimtafuta sana Msando ili niweze kumshauri jinsi ya kutatua tatizo hili kama diwani ambaye wapiga kura wake ni waathirika wakubwa.

Mabogini ni kata iliyotengwa na mbunge wa Moshi vijijini Cyril sijui nani. Barabara inayounganisha mabogini na pasua then Mjini moshi iko kama imepigwa bomu. Barabara hii ni kiunganisha kizuri sana cha Moshi mjini, pasua, Mabogini, Chekereni, Kahe na Kileo. Barabara hii wanakaa wakzi zaidi ya elfu 50 wanaunganisha inayotaka kuwa jiji la moshi.

Mipango miji bado ni shaghalabaghala haieleweki.

Kwanini ninamlaumu Wakili Albert Msando, Kamanda huyu ni kijana msomi hivyo wananchi walifikiri wanaingiza chachu ya mabadiliko fikra na maono mapya. Namuomba akimaliza kutetea wateja wake najua ni kazi kwani ndio kazi ya mwanasheria kutetea wahalifu ili watendewe haki, arudi kwenye kata yake tutatue matatizo ya wananchi.

Kwa Niaba ya wakazi wa Mabogini-tunamtafuta Diwani.

Msando ni diwani kwa tiketi ya CDM
 
Kwa Niaba ya wakazi wa Mabogini-tunamtafuta
 
Huyu jamaa hata sielewi analalamika nini,,mara albert msendo,,mara mabogini,,mara kilimo kwanza,,mara diwani wetu,,mara watete wahalifu wapate haki,,,,,,,hana tofauti na kipofu aliyepata nafasi yakuona kwa sekunde,,,atahadithia kama vile ameona saa zima
 
Uliyosema kuhusu wakulima,barabara ni kweli kabisa na hta kama Msando atagombea tena kupitia CDM hataweza kushinda.Watu wanajuta kuacha kumchagua KAPAMA wa CCM kipindi kile.
 
huyu anawajibika sana kwa wananachi wake
mwenyewe ameshajitolea kujenga shule mbali mbali na vyoo jimbo mwake
kw akipato chake mwenyewe,,Ingawa tunasema ni diwani ambae hatujui utajiri wake kaupataje lakini
amewasaidia sana wananchi wake na kupigania haki zao
huwa anaweka mirejesho ya kazi zake facebook.
ndio ni wakili lakini muda mwingi huwa anawasiliana na wananchi wake...
mwenyewe yupo humu atajitokeza..unaposema kapotea mwaka mzima sikuelewi na siamini
labda umetumwa kumharibia humu
 
Kamanda mimi mzaliwa wa Mabogini, nataka Msando aje hapa aseme ni kipi amekifanya na hivyo vyoo viko mtaa gani. AU akanushe kimoja nilicho andika. Aseme mara ngapi kahudhuria vikao vya madiwani achana vya kata. Huko facebook wananchi wa Mabogini hawawezi kusoma, hakuna hata internet Cafe hapa.
 
Ukienda kinyume na mapenzi ya wapenzi wa Lema utaitwa majina yote mabaya humu. Ili ukubalike itikia ndioooh! kwa Mbowe/Mtei utasifiwa ukiwa na fikra huru basi kubali matusi yote chini ya jua kwa wafuasi wa Mbowe. Utahurumia watu wanaposhabikia kama majuha bila ya kuruhusu werngine kufikiri kinyume cha wao.

Huu ni ujinga tu hakuna jina jingine.
 
Uliyosema kuhusu wakulima,barabara ni kweli kabisa na hta kama Msando atagombea tena kupitia CDM hataweza kushinda.Watu wanajuta kuacha kumchagua KAPAMA wa CCM kipindi kile.

wananchi wambogini hawawezi kumchagua mgombea wa CCM, hilo lipo wazi, wanataka Diwani wao afanye kazi, na kama akishindwa atachaguliwa diwani mwingine mchapa kazi kwa ticket ya chadema. Tafauti ya CCM na CDM ni chama kufuatilia watendaji wake. Kilio cha wananchi husikilizwa na CDM kuliko CCM. Hivyo wananchi wa Mabogini wana Imani kubwa sana na CDM kwani hata Chami aliwakimbia.
 
Ukienda kinyume na mapenzi ya wapenzi wa Lema utaitwa majina yote mabaya humu. Ili ukubalike itikia ndioooh! kwa Mbowe/Mtei utasifiwa ukiwa na fikra huru basi kubali matusi yote chini ya jua kwa wafuasi wa Mbowe. Utahurumia watu wanaposhabikia kama majuha bila ya kuruhusu werngine kufikiri kinyume cha wao.

Huu ni ujinga tu hakuna jina jingine.

Inawezekana unafikiri kama hao majuha. Tatizo la uongozi Mabogini linahusiana vipi na ufuasi. Tatizo la maji linalohitaji uongozi na mtetezi linahusiana vipi na ufuasi. Mabogini wanataka uongozi utakaowasaidia kutatua shida zao, walimpa Msando kura za udiwani wakijua watasaidiana kutatua tatizo la Maji ya kilimo, kuipigania barabara ya moshi mjini chekereni ambayo siyo zaidi ya kilomita 20 ila nauli kutoka mjini mpaka mabogini ni zaidi ya 500 kwasababu tu njia mbovu.

Wananchi hawa wanatozwa kodi na wako tayari kuchangia maendeleo.
 
Kamanda mimi mzaliwa wa Mabogini, nataka Msando aje hapa aseme ni kipi amekifanya na hivyo vyoo viko mtaa gani. AU akanushe kimoja nilicho andika. Aseme mara ngapi kahudhuria vikao vya madiwani achana vya kata. Huko facebook wananchi wa Mabogini hawawezi kusoma, hakuna hata internet Cafe hapa.

Diwani wa kata ya mabogini albert msando akikaguwa mradi wa umwagiliaji wa lower moshi na aligunduwa ili kufufua mradi huwo inaitajika zaidi ya bilioni 60 na aliongea na wananchi kuwajuza hilo. ImageUploadedByJamiiForums1386777267.590549.jpg
 
Diwani wa kata ya mabogini albert msando akikaguwa mradi wa umwagiliaji wa lower moshi na aligunduwa ili kufufua mradi huwo inaitajika zaidi ya bilioni 60 na aliongea na wananchi kuwajuza hilo.View attachment 126123

Mradi tunaishi nao miaka zaidi ya 25 sasa, alikagua nini hapo? Wakati mradi unapanuliwa mwanzoni mwa miaka ya 90 tulisema tunahitaji vyanzo vya uhakika vya maji pamoja na kuhifadhi maji.

Kuna ngonjera za uhaba wa maji, zimekuwepo kwa muda sasa, na Msando alitumia hiyo kushinda tunataka majibu sasa. Kilimo hiki kilikuwa cha kienyeji kabla ya kufanywa cha kisasa, wakati ni sehemu ndogo ilikuwa ina tumika kulimia mpunga. Upanuzi ukahitaji uwezo mkubwa wa maji hasa kwenye vyanzo, ila urahisi ni kuvuna maji ya mvua, na chem chem asilia kwa kuyakusanya kwa kutumia mabwawa makubwa ya kisasa.

Tunachohitaji ni uwakilishi wa kusimamia maendeleo yetu kwa uhakika, tunajua Mbunge hawezi kutusaidia kwani ameweka wazi hatuhitaji. Tunahitaji Diwani tutakafanya naye kazi na kufufua kilimo hiki na kuongeza pato la wananchi hawa. Huu upuuzi wa kumpiga mtu picha na kusema anakagua hewa huuu .....

Pili muulize hiyo siku Msando alipofika kwenye hilo kalavati la Rau river alipitia barabara gani? Aeleze kwanini wanaendelea kuifanya barabara ya mabogini mtaro wa maji ya mvua.------loading
 
Wewe ni kilaza unalalamika na majibu unajipa mwenyewe sasa kama mbunge wako kashindwa kuwasaidi unategemea nini kutoka kwa diwani?umesema amepote nimekuthibitishia kwa picha anajitahidi kwa nafasi yake kama diwani kuwa karibu na wananchi wake inawezekana kwa maelezo yako wewe ndio umepotea kwenye kata yako na hujuwi kinachoendelea shule za kata ya mabogini amejitahidi kusaidi kujenga matundu ya vyoo kwa pesa zake na si za halimashauri wakati wa kampeni alituaidi zaidi kusaidia upande wa elimu na hilo analifanya.
 
Back
Top Bottom