Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,227
- 26,048
Amani iwe kwenu Wadau.
Kwanza napenda kuwasalimu na kuwaomba radhi kwa kipindi chote ambacho sijaonekana katika jukwaa hili.
Nimekuwa kimya kwa kipindi nikifutilia mijadala mbalimbali kwenye jukwaa hili huku nikitafakari kwa kina ni kwa jinsi gani jukwaa hili linatoa mchango chanya katika ukuaji wa nchi yetu kwenye Nyanja zote.
Niliamua kuwa msomaji tu na sio mchangiaji ila hili alilolipost Wakili Msando leo limenifanya nirudi haraka na mie nitumie mchango wangu katika kuuelewesha umma wa watanzania katika mambo ya msingi ya kisheria kwa sababu nikikaa kimya umma wa watanzania utalishwa matango pori na watu wanajiita kuwa wanasheria ila wanapotosha kwa makusudi kwa sababu zao binafsi.
Albert Msando amepotosha umma kwa kiwango kikubwa sana kwa kusema kuwa CAG HANA kinga ya kutohojiwa na kamati ya Bunge kwa kauli inayosemekana ya kulidhalilisha Bunge. Napenda kusema kuwa Msando amekosea sana na anastahili kuiomba radhi tasnia ya sheria kwa upotoshaji huu uliotukuka.
Katika katiba ya Jamhuri ya Tanzania ya mwaka 1977 kati ya nafasi ambazo zimelindwa na zimewekwa kuwa nyeti mojawapo ni nafasi za Jaji( Mahakama kuu na Mahakama ya rufaa) pamoja na CAG. Watu hawa wamewekewa utaratibu maalumu wa kuwawajibisha endapo watafanya makosa yeyote yale iwe wao kama wao au wao kama taasisi na Katiba ya Tanzania haikuacha mwanya wowote katika hayo.
CAG wa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Tanzania ya mwaka 1977 ibara za 143 na 144 ana njia mbili tu za kumuwajibisha nazo ni
Mussa Assad alikuwa nchini Marekani kama CAG akiwakilisha Tanzania kama CAG ana hata pale alikuwa akihojiwa kama CAG wa Tanzania kuhusu utengaji wake wa kazi za U CAG wa Tanzania. Kama kuna kosa limefanywa pale taratibu za kumshughulikia ni za njia mbili tu yaaani ni kwa Mahakama au Tume maalumu ya Majaji ambayo lazima ijumuishe majaji/ jaji kutoka nchi za jumuiya ya Madola.
Naomba Msando usitumike katika kupotosha juu ya hili na napenda sote tukumbuke jambo hili linahusu katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo ndo inayotuongoza sote.
Ingawa Katiba ya Jamhuri ya muungazo ya 1977 ina mapungufu mengi na wengine kudai imepitwa na wakati lakini pia ina mambo mazuri mengi sana yakiwemo haya ya kulinda taasisi ya Mahakama/Majaji na taasisi/nafasi ya CAG.
Asanteni.

- MAHAKAMA
- KAMATI/TUME MAALUM YA MAJAJI AMBAYO LAZIMA IJUMUISHE MAJAJI KUTOKA JUMUIYA YA MADOLA