Wakili Albert Msando amepotosha umma kwa kudai CAG hana kinga ya kutohojiwa na Kamati ya Bunge

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
6,718
2,000
Amani iwe kwenu Wadau.

Kwanza napenda kuwasalimu na kuwaomba radhi kwa kipindi chote ambacho sijaonekana katika jukwaa hili.

Nimekuwa kimya kwa kipindi nikifutilia mijadala mbalimbali kwenye jukwaa hili huku nikitafakari kwa kina ni kwa jinsi gani jukwaa hili linatoa mchango chanya katika ukuaji wa nchi yetu kwenye Nyanja zote.

Niliamua kuwa msomaji tu na sio mchangiaji ila hili alilolipost Wakili Msando leo limenifanya nirudi haraka na mie nitumie mchango wangu katika kuuelewesha umma wa watanzania katika mambo ya msingi ya kisheria kwa sababu nikikaa kimya umma wa watanzania utalishwa matango pori na watu wanajiita kuwa wanasheria ila wanapotosha kwa makusudi kwa sababu zao binafsi.

Albert Msando amepotosha umma kwa kiwango kikubwa sana kwa kusema kuwa CAG HANA kinga ya kutohojiwa na kamati ya Bunge kwa kauli inayosemekana ya kulidhalilisha Bunge. Napenda kusema kuwa Msando amekosea sana na anastahili kuiomba radhi tasnia ya sheria kwa upotoshaji huu uliotukuka.

Katika katiba ya Jamhuri ya Tanzania ya mwaka 1977 kati ya nafasi ambazo zimelindwa na zimewekwa kuwa nyeti mojawapo ni nafasi za Jaji( Mahakama kuu na Mahakama ya rufaa) pamoja na CAG. Watu hawa wamewekewa utaratibu maalumu wa kuwawajibisha endapo watafanya makosa yeyote yale iwe wao kama wao au wao kama taasisi na Katiba ya Tanzania haikuacha mwanya wowote katika hayo.

CAG wa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Tanzania ya mwaka 1977 ibara za 143 na 144 ana njia mbili tu za kumuwajibisha nazo ni
  • MAHAKAMA
  • KAMATI/TUME MAALUM YA MAJAJI AMBAYO LAZIMA IJUMUISHE MAJAJI KUTOKA JUMUIYA YA MADOLA
Katika katiba ya Jamhuri ya Tanzania haijasema popote pale kuwa kamati ya Bunge inaweza kumuhoji CAG kwa iyo jibu kama kamati ya Bunge ina mamlaka ni HAPANA HAINA MAMLAKA HAYO.

Mussa Assad alikuwa nchini Marekani kama CAG akiwakilisha Tanzania kama CAG ana hata pale alikuwa akihojiwa kama CAG wa Tanzania kuhusu utengaji wake wa kazi za U CAG wa Tanzania. Kama kuna kosa limefanywa pale taratibu za kumshughulikia ni za njia mbili tu yaaani ni kwa Mahakama au Tume maalumu ya Majaji ambayo lazima ijumuishe majaji/ jaji kutoka nchi za jumuiya ya Madola.

Naomba Msando usitumike katika kupotosha juu ya hili na napenda sote tukumbuke jambo hili linahusu katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo ndo inayotuongoza sote.

Ingawa Katiba ya Jamhuri ya muungazo ya 1977 ina mapungufu mengi na wengine kudai imepitwa na wakati lakini pia ina mambo mazuri mengi sana yakiwemo haya ya kulinda taasisi ya Mahakama/Majaji na taasisi/nafasi ya CAG.

Asanteni.
 
mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,461
2,000
msando mbabaishaji tu anataka aonekane kule ccm mtetezi
Amani iwe kwenu Wadau.
Kwanza napenda kuwasalimu na kuwaomba radhi kwa kipindi chote ambacho sijaonekana katika jukwaa hili. Nimekuwa kimya kwa kipindi nikifutilia mijadala mbalimbali kwenye jukwaa hili huku nikitafakari kwa kina ni kwa jinsi gani jukwaa hili linatoa mchango chanya katika ukuaji wan chi yetu kwenye Nyanja zote. Niliamua kuwa msomaji tu na sio mchangiaji ila hili alilolipost Wakili Msando leo limenifanya nirudi haraka na mie nitumie mchango wangu katika kuuelewesha umma wa watanzania katika mambo ya msingi ya kisheria kwa sababu nikikaa kimya umma wa watanzania utalishwa matango pori na watu wanajiita kuwa wanasheria ila wanapotosha kwa makusudi kwa sababu zao binafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MISULI

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
7,389
2,000
Kinga alizo nazo CAG ni katika kutimiza majukum yake ya uCAG tu,Hakuna sehem speaker atamwita CAG kuhusiana na mambo ya Auditing kuwa yamekosewa, amechelewa kutoa au kashindwa kutimiza jambo lolote katika kazi yake. Hapa speaker hana Nguvu yyt ya kumhoji CAG. Mfano hata kwa Makonda speaker asingekuwa na mamlaka yyt ya kumwita makonda kwa makosa ya utekelezaji wa majukum yake ya uRC. Makonda hata awe anachelewa kuingia ofisini, anatukana watu au anafanya mambo yyt kinyume na maadili bado bunge halina haki ya kumhoji. Makonda na CAG waliitwa na Bunge kwa kosa moja tu,KUDHARAU BUNGE. Hapa huna cha nilikua kwenye majukum yangu au nilikua wapi,Swala ni umedharau Mhimili wa Bunge na Bunge haliwez kukupa adhabu yyt nje ya onyo na kama ni kutaka ufukuzwe kazi ni wao kuwasiliana na Mhimili uliokupa ajira ambao ni Serikali. Bunge likiona makosa yako ni makubwa na hayabebeki wao ni kutoa maazimio kwenda kwa serikali na Mwisho serikali itatakiwa kutoa uamuzi juu ya jambo hilo.CAG na ofisi yake sio muhimil unaojitegemea,Huu uko chini ya serikali na kinga alizo nazo ni ktk kutimiza majukum yake ya uCAG na sio nje ya Hapo.Kama kulidharrsha bunge ni sehemu ya kazi za CAG basi hakuna shida.

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
 
Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
23,736
2,000
Mkuu hapa unatuingiza Chaka Rudi tena kwenye reference zako. CAG hawajibishwi na mahakama, CAG anawajibishwa na Rais hii ni baada ya tume maalum aliyoiteua yeye Rais kumpelekea mapendekezo yake.

Ila kwa tafsiri ya Ibara ya 143 ni mahakama pekee ndiyo yenye uwezo wa kuingilia utendaji kazi wake.
 
Right Guy

JF-Expert Member
Mar 11, 2016
289
1,000

Hii tafsiri kwamba kinga aliyonayo CAG ni kwenye kutekeleza majukumu yake tu umelitoa wapi? Je, hii tafsiri yako inatumika kwa CAG peke yake au hata kwa majaji, rais na wabunge ambao wote wana kinga ya kikatiba? Unamaanisha kwamba hata rais anaweza kushitakiwa kwa kuwatukana wale wanafunzi wa UDOM kwamba ni "vilaza" kwa kuwa kutukana siyo sehemu ya majukumu yake kama rais?

Hili kosa la kudhalilisha bunge lipo kwenye kifungu gani? Ingredients zake ni zipi na adhabu yake ni ipi? Mbona mnatengeneza makosa ya hisia au kauli inayomkera Ndugai ndo kudhalilisha Binge?
 
Kujibu hoja yako ya mwanzo tafadhali rejea Ibara ya 143 (6) ya katiba 1977.
 
Right Guy

JF-Expert Member
Mar 11, 2016
289
1,000
Mkuu hapa unatuingiza Chaka Rudi tena kwenye reference zako. CAG hawajibishwi na mahakama, CAG anawajibishwa na Rais hii ni baada ya tume maalum aliyoiteua yeye Rais kumpelekea mapendekezo yake.

Ila kwa tafsiri ya Ibara ya 143 ni mahakama pekee ndiyo yenye uwezo wa kuingilia utendaji kazi wake.
Vyovyote utakavyochagua kusema lakini cha msingi ni kwamba tume itatoa mapendekezo kwa rais na rais atalazimika kufuata mapendekezo hayo, hana chaguo.
 
Gulwa

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
5,765
2,000
Amani iwe kwenu Wadau.
Kwanza napenda kuwasalimu na kuwaomba radhi kwa kipindi chote ambacho sijaonekana katika jukwaa hili. Nimekuwa kimya kwa kipindi nikifutilia mijadala mbalimbali kwenye jukwaa hili huku nikitafakari kwa kina ni kwa jinsi gani jukwaa hili linatoa mchango chanya katika ukuaji wan chi yetu kwenye Nyanja zote. Niliamua kuwa msomaji tu na sio mchangiaji ila hili alilolipost Wakili Msando leo limenifanya nirudi haraka na mie nitumie mchango wangu katika kuuelewesha umma wa watanzania katika mambo ya msingi ya kisheria kwa sababu nikikaa kimya umma wa watanzania utalishwa matango pori na watu wanajiita kuwa wanasheria ila wanapotosha kwa makusudi kwa sababu zao binafsi.
Albert Msando amepotosha umma kwa kiwango kikubwa sana kwa kusema kuwa CAG HANA kinga ya kutohojiwa na kamati ya Bunge kwa kauli inayosemekana ya kulidhalilisha Bunge. Napenda kusema kuwa Msando amekosea sana na anastahili kuiomba radhi tasnia ya sheria kwa upotoshaji huu uliotukuka.
Katika katiba ya Jamhuri ya Tanzania ya mwaka 1977 kati ya nafasi ambazo zimelindwa na zimewekwa kuwa nyeti mojawapo ni nafasi za Jaji( Mahakama kuu na Mahakama ya rufaa) pamoja na CAG. Watu hawa wamewekewa utaratibu maalumu wa kuwawajibisha endapo watafanya makosa yeyote yale iwe wao kama wao au wao kama taasisi na Katiba ya Tanzania haikuacha mwanya wowote katika hayo.
CAG wa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Tanzania ya mwaka 1977 ibara za 143 na 144 ana njia mbili tu za kumuwajibisha nazo ni
  • MAHAKAMA
  • KAMATI/TUME MAALUM YA MAJAJI AMBAYO LAZIMA IJUMUISHE MAJAJI KUTOKA JUMUIYA YA MADOLA
Katika katiba ya Jamhuri ya Tanzania haijasema popote pale kuwa kamati ya Bunge inaweza kumuhoji CAG kwa iyo jibu kama kamati ya Bunge ina mamlaka ni HAPANA HAINA MAMLAKA HAYO.
Mussa Assad alikuwa nchini Marekani kama CAG akiwakilisha Tanzania kama CAG ana hata pale alikuwa akihojiwa kama CAG wa Tanzania kuhusu utengaji wake wa kazi za U CAG wa Tanzania. Kama kuna kosa limefanywa pale taratibu za kumshughulikia ni za njia mbili tu yaaani ni kwa Mahakama au Tume maalumu ya Majaji ambayo lazima ijumuishe majaji/ jaji kutoka nchi za jumuiya ya Madola.
Naomba Msando usitumike katika kupotosha juu ya hili na napenda sote tukumbuke jambo hili linahusu katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo ndo inayotuongoza sote.

Ingawa Katiba ya Jamhuri ya muungazo ya 1977 ina mapungufu mengi na wengine kudai imepitwa na wakati lakini pia ina mambo mazuri mengi sana yakiwemo haya ya kulinda taasisi ya Mahakama/Majaji na taasisi/nafasi ya CAG.
Asanteni.
Ukishajiunga nao unafanana nao, ccm
 
Turnkey

JF-Expert Member
Jul 9, 2013
7,093
2,000
Kinga alizo nazo CAG ni katika kutimiza majukum yake ya uCAG tu,Hakuna sehem speaker atamwita CAG kuhusiana na mambo ya Auditing kuwa yamekosewa, amechelewa kutoa au kashindwa kutimiza jambo lolote katika kazi yake. Hapa speaker hana Nguvu yyt ya kumhoji CAG. Mfano hata kwa Makonda speaker asingekuwa na mamlaka yyt ya kumwita makonda kwa makosa ya utekelezaji wa majukum yake ya uRC. Makonda hata awe anachelewa kuingia ofisini, anatukana watu au anafanya mambo yyt kinyume na maadili bado bunge halina haki ya kumhoji. Makonda na CAG waliitwa na Bunge kwa kosa moja tu,KUDHARAU BUNGE. Hapa huna cha nilikua kwenye majukum yangu au nilikua wapi,Swala ni umedharau Mhimili wa Bunge na Bunge haliwez kukupa adhabu yyt nje ya onyo na kama ni kutaka ufukuzwe kazi ni wao kuwasiliana na Mhimili uliokupa ajira ambao ni Serikali. Bunge likiona makosa yako ni makubwa na hayabebeki wao ni kutoa maazimio kwenda kwa serikali na Mwisho serikali itatakiwa kutoa uamuzi juu ya jambo hilo.CAG na ofisi yake sio muhimil unaojitegemea,Huu uko chini ya serikali na kinga alizo nazo ni ktk kutimiza majukum yake ya uCAG na sio nje ya Hapo.Kama kulidharrsha bunge ni sehemu ya kazi za CAG basi hakuna shida.

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
Kusema DHAIFU ni kosa la jinai???
 
MISULI

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
7,389
2,000
Hii tafsiri kwamba kinga aliyonayo CAG ni kwenye kutekeleza majukumu yake tu umelitoa wapi? Je, hii tafsiri yako inatumika kwa CAG peke yake au hata kwa majaji, rais na wabunge ambao wote wana kinga ya kikatiba? Unamaanisha kwamba hata rais anaweza kushitakiwa kwa kuwatukana wale wanafunzi wa UDOM kwamba ni "vilaza" kwa kuwa kutukana siyo sehemu ya majukumu yake kama rais?

Hili kosa la kudhalilisha bunge lipo kwenye kifungu gani? Ingredients zake ni zipi na adhabu yake ni ipi? Mbona mnatengeneza makosa ya hisia au kauli inayomkera Ndugai ndo kudhalilisha Binge?
Kama maelezo yote yale bado hujaelewa basi kuna walakini ktk uwezo wako wa kuchanganua Mambo. Hicho kifungu kiko wazi kabisa,kinaelezea majukum yake. Au hujui kusoma?Rais hakuna popote pale anaweza shtakiwa au hojiwa kwa jambo lolote lile analofanya hii ni katiba. Kasome vizur katiba uone kama kinga ya Rais na CAG ziko sawa.Pili umekuja na mfano mbovu kabisa wa kuita wanafunzi vilaza, Sasa wanafunzi ni wabunge au ni Bunge?Tuseme Rais asingekuwa na kinga ya kuhojiwa bado kuna tume ya utumishi wa umma inayosimamia maadili na huko ndio angepelekwa kuhojiwa na sio Bungeni. Hao wote wameitwa kuhojiwa kwa kosa la kudharau bunge sio kwa makosa ya utekelezaji wa majukum yao.CAG hana kinga yyt juu ya makosa nje ya kazi zake. CAG akipiga mtu lzm ashitakiwe, lkn Rais akipiga mtu hakuna popote pa kumshtaki. So kinga ya CAG msiikweze sana na amepewa hiyo kinga kutokana na unyeti wa kazi zake ambapo inahitaji umakini mkubwa sana bila kusumbuliwa na yyt.

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
 
MISULI

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
7,389
2,000
Kusema DHAIFU ni kosa la jinai???
Kasome Sheria za maadili ya viongoz. Sijui kazi unayofanya na elimu yako,lkn kwa Mimi niliyesoma ETHICS za Uongozi ni kosa kubwa sana kutaja UDHAIFU au kukashifu kiongoz mwenzio hadharani hata kama ni ukweli kias gani. Mkuu wa Shule Huwez simama assemble na kusema mwalimu flani hufundishi vizur na ndio maana watoto wanafeli. Unaweza kuwa sahihi kabisa kwa kauli yako lkn kimaadili ya utumishi wa umma ni kosa kubwa ambalo kama litafika sehem husika unaweza fukuzwa kazi. CAG ni mtumishi wa umma na kuna fomu ya maadili ya viongoz kajaza inasema nini kuhusu kuheshimu viongoz au taasisi unayoshirikiana nayo kufanya kazi?Na utaona kesi ya CAG haimamriwi na mahakama bali na kamati ya maadili. CAG akiiba kwanza anapelekwa kamati ya maadili na Mwisho mahakaman. Kusema Dhaifu sio kosa la jinai na ni kweli bunge ni dhaifu lkn ndio maadili ya viongoz au watumishi wa umma?

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
 
Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
23,736
2,000
Kwenye kutekeleza majukumu yake hayo ndo ametoa kauli ambayo haijampendeza mgogo mmoja kutoka Idodomia, hilo unalitenganishaje?
Majukumu ya CAG yanapatikana katika Ibara ya 143 (2) (3) , (4) ya katiba, pia kifungu cha 11 na 12 cha Public Audit Act, 2008 ;

Kutoa maoni ya Taasisi anazofanya nazo kazi sio sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake kwani majukumu yake ya msingi yamekwisha ainishwa hapo juu ambapo kitendo hicho hakifanyi sehemu ya majukumu hayo.

Kwa ujumla wake tungependa kuiona comment yake wazi wazi katika ripoti zake na sio katika vyombo vya habari vya nje.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom