Wakili aeleza walivyosota gerezani na mkewe miezi 18, waamua kudai fidia

Uko sahihi kabisa. Na hata kama atashinda hiyo kesi, basi ni kutokana tu udhaifu wa vyombo vyetu vya kiuchunguzi kufanya kazi zao kwa kukurupuka.
Huyo lawyer na mke wake Wana kesi za kujibu, conflict of interest mke anamupa insider info, jamaa mume wake anapita nazo, anashinda kesi za wateja wake. Kuna mambo mengi yamefichwa hapo huyo jamaa anataka huruma toka kwa jamii
 
Acha hizo, Kwani si alihamishwa na baadaye akaamuwa kuacha kazi? Mgongano gani wa kimaslahi? Walibambikiwa kesi ili kuwakomoa. Tulia na utafakari ukiwa sober.
wewe ndio unatakiwa utafakari sio wote waliowekwa ndani na awamu iliyopita walionewa , kuna mtu alileta uzi jinsi alivyonyanyaswa na huyu jamaa akiwa polisi kwa kifupi karma imemkuta.
 
DPP Mganga anapaswa kuchunguzwa kwa uhalifu,malalamiko juu yake ni mengi mno
Na waliokuwa uhamiaji wakiandaa permit fake au kuwanasumbua wageni nao wachukuliwe hatua. Tunasahau kama vile kila mtu anaonewa. Wengine walikuwa ndani kihalali kabisa
 
Hii nchi ina mambo mengi sana, unamuweka mtu ndani muda wote huo bila dhamana na huna uthibitisho wa makosa yake, hii ni zaidi ya ukatili, atlist hata wangemuacha nje kwa dhamana wakati uchunguzi unaendelea

Wamempotezea muda, malengo, wameyumbisha familia yake, wamesimamisha mambo yake mengi, bad enough wamemkamata na mke wake pia
Kwenye hii kesi, ili mradi amekata rufaa, tutasikia upande wa pili wa story. Iko maneno mengi kuliko haya aliyoeleza jamaa. Hizi ofisi za serikali kuna watu wengi wanazitumia vibaya ikiwemo wengine wachache, askari uhamiaji
 
Hii nchi ina mambo mengi sana, unamuweka mtu ndani muda wote huo bila dhamana na huna uthibitisho wa makosa yake, hii ni zaidi ya ukatili, atlist hata wangemuacha nje kwa dhamana wakati uchunguzi unaendelea

Wamempotezea muda, malengo, wameyumbisha familia yake, wamesimamisha mambo yake mengi, bad enough wamemkamata na mke wake pia
Lengo lao kuu ni kumpotezea muda na kumtoa kwenye ramani. Usikute hapo walishindwana kwenye mgawo ndiyo wakaamua kumkomoa au Hata ugomvi Wa kimapenzi tu..

Ifike mahali ukishitakiwa na Serikali kisha ukakutwa huna hatia basi yule aliyefungua hiyo Kesi ndiye umshtaki personally Kwa kukupotezea muda, maana kuna kesi nyingi sana zinafunguliwa Kwa kisingizio cha Serikali ila nyuma yake kuna personal interest..
 
Kazi imeanza, kesi hizi zitakuww nyingi sana na serikali inaweza kujikuta inalipa watu mafidia mengi sana...
 
Huyo wakili na mkewe hawakutumia akili as if hawajasoma sheria. Walistahili yote hayo. Ukisoma maelezo yake ya awali unaona kabisa aliyakanyaga mwenyew.
 
Tukiwalipa hawa wote kweli nchi itabaki na rupia hata moja ?

Sababu ni wengi kweli kweli....
 
THURSDAY JUNE 17, 2021

Dar es Salaam. Wakili Peter Madeleka na mkewe, Jamila Augustine Ilomo wameishitaki Serikali wakidai fidia ya mali kwa kukaa gerezani kama mahabusu kwa zaidi ya miezi 18 na baadaye kuachiwa buru baada ya makubaliano na DPP.

Katika kesi Na. 10 ya mwaka 2021 aliyoifungua katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Madeleka anadai fidia kwa kusababishiwa hasara na kushushiwa hadhi mbele ya jamii kwa kitendo cha kushitakiwa kwa tuhuma ambazo Serikali imeshindwa kuzithibitisha.

Kisa kilivyoanza

Akizungumza hivi karibuni na Mwananchi, Wakili Madeleka, aliyewahi kuwa ofisa wa Jeshi la Polisi mwenye cheo cha mkaguzi kabla ya kuacha kazi hiyo mwaka 2016, alisema kisa kilianza baada ya kuhamia jijini Arusha na kufungua ofisi yake ya uwakili.

“Niliamua kuhamia Arusha nikimfuata mke wangu aliyekuwa ofisa uhamiaji. Yeye pia alikuwa mwanasheria kitaaluma,” alisema.

Hata hivyo, anasema mambo yalianza kubadilika baada ya kazi yake ya uwakili kuanza kupata mafanikio.

“Mimi kazi yangu ni kwenda kuwatetea watu wenye matatizo ya kisheria, wakiwemo waliokamatwa na uhamiaji. Siwezi kuwakataa watu waliokamatwa na uhamiaji anakofanya kazi mke wangu.

“Kukawa na malalamiko kutoka Idara ya Uhamiaji wakisema kuna mgongano wa kimasilahi. Mimi nikawaeleza kuwa kuoana na ofisa wao si kosa kisheria,” alisema.

Baadaye malalamiko yalipozidi, anasema alimwandikia barua Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kumjulisha malalamiko hayo na kwamba hana hatia. Lakini anasema barua hiyo ilimgeuka.

“Nilipomwandikia barua hiyo Kamishna Jenerali mwaka 2017, hatua iliyofuata ikawa ni kuhamishwa kwa mke wangu kutoka Arusha kwenda Singida na familia yetu iliathirika.

“Mimi nikamwambia mke wangu aache kazi, wakati huo alikuwa na nyota tatu na amesomea sheria. Aliporudi tukaendelea na kazi zetu za uwakili,” anasema.

Kesi ndani ya kesi

Ilipofika Agosti 2, 2019 ikatokea kesi inayohusu idara ya uhamiaji ambayo pia alikwenda kutetea wateja wake.

“Kuna mtu alitoka Afrika Kusini, alikamatwa akiwa na visa feki za Tanzania. Agosti 11, 2019 mtu huyo akapelekwa mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam pamoja na aliyekuwa kamishna wa sheria wa uhamiaji. Mimi nikaenda kumtetea huyo kamishna baada ya kuombwa na ndugu zake,” anasema.

Alisema kitendo hicho kiliibua hasira ya uhamiaji na hapo mzozo mpya ukaanza.

“Kwa hiyo nilipokuwa katika harakati za kumtetea yule kamishna ndipo nilikamatwa mimi, mke wangu pamoja na wakili mmoja aliyekuwa kwenye ofisi yangu,” anasema.

Anasema wakati kesi ikiwa imetajwa mara mbili, polisi walikwenda kwenye nyumba aliyofikia Upanga na kumkamata.

“Siku hiyo hiyo, mke wangu aliyekuwa Arusha naye akakamatwa na yule wakili mwingine, wakasafirishwa kuja Dar es Salaam, tukaunganishwa kwenye hiyo kesi ya visa feki.”

Anasema walifikishwa mahakamani Agosti 25, 2019 wakihusishwa na utengenezaji wa visa feki na kosa la utakatishaji fedha.

“Ilikuwa kesi ya uhujumu uchumi Na. 81 ya mwaka 2019. Tukapelekwa gereza la Segerea ambako tulikaa miezi saba,” alisema.

Kuanzia Agosti 25, 2019 alisema walikuwa wanahudhuria mahakamani na kuambiwa upelelezi unaendelea hadi Mei 12, 2020 Serikali iliposema haina nia ya kuendelea na kesi hiyo, hivyo ikafutwa wakaachiwa huru.

“Wakati tunatoka mahakamani Kisutu tukijiandaa kwenda nyumbani, tukakamatwa tena na kuambiwa tuna kesi nyingine inayotukabili Arusha, hivyo tuko chini ya ulinzi, tukapelekwa Kituo cha Polisi Mburahati tukalala mpaka Mei 13, 2020 tukasafirishwa kwenda Arusha.”

Anasema wakiwa Arusha Mei 14, 2020 wakapelekwa mahakama ya Arusha wakituhumiwa kwa kosa la uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, hivyo baada ya kesi kutajwa wakapelekwa gereza la Kisongo ambako walikaa miezi 11 na siku 13.

Anasema huko nako kesi ilikuwa ikitajwa lakini haiendelei.

“Nilijaribu kumwandikia barua Jaji anayesikiliza kesi na hakimu kwa kuwa niliona kesi yenyewe ni ya kunikomoa tu, lakini walikuwa wakipiga chenga.”

Hata hivyo, anasema ilipofika Machi 30, 2021, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), (sasa Jaji Biswalo Mganga), alitembelea gereza la Kisongo na kumtafuta.

“Alisema siwezi kutoka gerezani mpaka tufanye makubaliano, vinginevyo, nitaozea huko gerezani,” anasema.

Alisema baada ya ujumbe huo, mwakilishi wa DPP Mkoa wa Arusha alimwandikia barua mkuu wa magereza mkoani humo akiwaarifu watuhumiwa wanaotaka kumaliza kesi kwa majadiliano na DPP waandike barua.

“Kwa hiyo na mimi nikaandika barua, lakini nikijua kwamba utaratibu anaoagiza wa plea bargain umekosewa.

“Mimi nikafanya hivyo, Nikapeleka hizo fedha zilikuwa Sh2 milioni kwenye akaunti ya DPP ya BoT. Aprili 27 mwaka huu nikaitwa mahakamani, DPP akasema ameshakubaliana na mimi, akaomba mahakama iniachie.”

Baada ya kutoka jela Madeleka na mkewe sasa wamefungua kesi wakitaka walipwe fidia na Serikali, japo anasema kiasi cha fidia hiyo kitaamuliwa na mahakama.

Kuhusu kesi ya pili, Madeleka anasema bado yuko mbioni kufungua nyingine kupinga mchakato wa plea bargain uliomfanya akiri kosa na kulipa Sh2 milioni.

“Kiutaratibu, plea bargain inatakiwa ifanywe na mwendesha mashtaka wa kesi husika, lakini DPP alitaka afuatwe Dodoma, halafu yeye ndiye ajadiliane na mtuhumiwa na fedha ziwekwe kwenye akaunti yake iliyoko Benki Kuu ya Tanzania.

“Kwa mujibu wa kanuni ya 21(3(a) ya kanuni za plea bargain zilizotiwa saini na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, zinasema anayetakiwa kulipwa fedha ni msajili wa hazina ambaye yuko chini ya Wizara ya Fedha,” alisema.

Anaitaja pia kanuni ya 23 inayosema; kama plea bargain itafanyika kinyume cha hapo kwa namna yoyote ile basi aliyefanya plea bargain anaweza kwenda mahakamani na hiyo hukumu itatenguliwa.

Chanzo: Mwananchi
Pole sana wana ndoa kwa kubambikiwa kesi. Kuna wakati unawaza matukio kama haya pamoja na ya Sabaya yaliyotokea wakati wa utawala wa Kayafa unajikuta unamshukuru Mungu kwa kumwita katika ufalme wake vinginevyo angefikisha miaka kumi wengi wangeteketea. Asante Mungu ingawa ulichelewa kidogo kufanya maamuzi. Better late than never.
 
Nakumbuka jinsi Maguchizi alivyotamani gari ya Manji nayo ingekamatwa na kuwekwa ndani pamoja naye. Ndio ilikuwa michezo yao hii, kunyang'anya watu mali zao.
 
Ukisoma vizuri kuna maelezo ameficha, inaonyesha wazi kulikuwa na mgongano wa kimaslahi kwa yeye kusimamia kesi za uhamiaji wakati mke wake yupo huko. Naunga mkono polisi kukamata watu kama hao wanaichafua sana nchi.
Kama hujui kitu kaa kimya tu, mbona kuna watu wengi tu wanafanya kazi TRA, idara ya kodi za ndani, wameolewa na mawakili, tena kuna kesi nyingi za mambo ya kodi, wana zitetea?nenda ofisi ya upelelezi pale makao makuu ya polisi, kuna wapelelezi kibao wameolewa na mawakili, mbona hata siku moja hujasikia hayo mambo?eti kuna kitu amekificha, hahaaa!!mala ngapi mwendazake aliwatishia mawakili kuwa jitu limeiba eti ana kuja wakili kulitetea, naye inabidi aingizwe kwenye kesi hiyo kwani sio uzalendo!!!daaa huyo ni kiongozi wa nchi!!MUNGU FUNDI
 
Hizi ndo zile kesi za kubambikiana kipindi cha Kayafa mwanaharamu mwendazake
 
Huyo lawyer na mke wake Wana kesi za kujibu, conflict of interest mke anamupa insider info, jamaa mume wake anapita nazo, anashinda kesi za wateja wake. Kuna mambo mengi yamefichwa hapo huyo jamaa anataka huruma toka kwa jamii
Lawyer mpumbavu.
 
Afrika kuna udhalimu sana, yaani sisi tunaonewa na wazungu halafu tena tunaonewa na wenye madaraka/mamlaka...

Gademu....
 
Lengo lao kuu ni kumpotezea muda na kumtoa kwenye ramani. Usikute hapo walishindwana kwenye mgawo ndiyo wakaamua kumkomoa au Hata ugomvi Wa kimapenzi tu..

Ifike mahali ukishitakiwa na Serikali kisha ukakutwa huna hatia basi yule aliyefungua hiyo Kesi ndiye umshtaki personally Kwa kukupotezea muda, maana kuna kesi nyingi sana zinafunguliwa Kwa kisingizio cha Serikali ila nyuma yake kuna personal interest..
Hao waliomshtaki kwa kumjengea zengwe walitumwa na serikali ya mwendazake, kwahiyo serikali ndio inatakiwa ishtakiwe na ilipe fidia
 
Kama hujui kitu kaa kimya tu, mbona kuna watu wengi tu wanafanya kazi TRA, idara ya kodi za ndani, wameolewa na mawakili, tena kuna kesi nyingi za mambo ya kodi, wana zitetea?nenda ofisi ya upelelezi pale makao makuu ya polisi, kuna wapelelezi kibao wameolewa na mawakili, mbona hata siku moja hujasikia hayo mambo?eti kuna kitu amekificha, hahaaa!!mala ngapi mwendazake aliwatishia mawakili kuwa jitu limeiba eti ana kuja wakili kulitetea, naye inabidi aingizwe kwenye kesi hiyo kwani sio uzalendo!!!daaa huyo ni kiongozi wa nchi!!MUNGU FUNDI
wewe ndio kaa kimya hivi umeshawahi kujaza tenda kwenye hizi international organization na wanakwambia kabisa ndugu wa wafanyakazi hawaruhusiwi kushiriki au umeshasoma sheria za maadili unakaa unapayukapayuka bila kujua ni nini kinajadiliwa.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom