Wakili achambua maagizo ya Makonda

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Wakili maarufu nchini Alberto Msando amechambua maagizo ya utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambayo amekuwa akiyatoa, likiwemo suala la uvutaji hadharani wa sigara na shisha.

Tangu alipoapishwa Machi mwaka huu, Makonda amekuwa akitoa maagizo mbalimbali na mikakati yake ya kutaka kulipanga upya jiji ili kuwe na maeneo maalum ya gereji, majumba ya maduka makubwa, maeneo ya kuuza magari tofauti na huduma nyinginezo. Mengine ni kuondoa ombaomba jijini, kutaka wasiovaa kofia ngumu kwenye bodaboda washtakiwe kwa kutaka kujiua, kuhakikisha mitaa inakuwa safi, kuondoa mashoga, kufungwa maeneo yanayofanya biashara ya shisha, kuondoa majengo yasiyo na maegesho, kutatua changamoto za elimu na barabara.

Lakini Msando anachambua mikakati hiyo, akionekana kushauri kuwa elimu itumike zaidi kwa kuwa maamuzi mengine yanahitaji nchi kutunga sheria, kitu ambacho hakitawezekana ndani ya siku saba.
 
huo ndo ukweli,sasa saiv anafanya kazi kupitia media apate sifa na werevu wameshajua hamna kitu pale,wanafanya jitihada sana kuwachafua ma mayor lkn wenzao wanapiga kazi kimya kimya.....ndo maana wanasogezwa wengi ubungo(makada) ili watibue mipango ya watu mahir.mmekwishaaaaaa tumewajua vzr sasa
 
Haya mambo hayahitaji hasira..Lazima Makonda ajipange kabla ya kutatua baadhi ya mambo,haya mambo ya kukimbilia media bila kuwa na mikakati mizuri itasababisha maagizo yatolewe lakini yasifanyiwe kazi. Mimi namshauri kaka yangu makonda akae na wadau na waangalie jinsi ya kutatua hizo kero zilizopo.
 
Uchambuzi wenyewe mbona hatujauona..tumeona maoni yako tu na ufupisho wa habari yako we we..Mwacheni Mkuu wa Mkoa afanyekazi. Alokwambia wanasiasa lazima wafuate sheria ni nani wakati media zinatoa habari bila Kodi!!
 
Wana dar wanaendeshwa kama kiberenge kibovu
1467888377054.jpg
 
Back
Top Bottom