Wakikataa..Tuunde Muswada Wetu..Maoni kisha Tuunde Katiba Yetu! Tupige Kura!

IsangulaKG

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
706
385
Nimekaa kimya muda mrefu nikiangalia jinsi ambavyo CCM inachezea vichwa vya watanzania wasomi. Wabunge wa CCM kama akina Ole Sendeka wanashindwa kuelewa maoni ya upinzani na kubaki wakijipendekeza kwa Kikwete na kuukaripia upinzani. Ndugu zangu watanzania, Hii ndiyo nafasi pekee tuliyonayo ya kuondoa ubepari na ubeberu wa CCM na chama chochote kitakachoshika hatamu kwa Kutengeneza Katiba Mpya. Kama ninavyosema Kila siku, ni vema kushi siku chache kwa shida ukiwa umetenda mema kuliko kuishi siku nyingi kwa amani ukiwa umetenda maovu. Namaanisha wanachokifanya makamanda wa Chadema , kinamaanisha kutenda mema kwa Taifa hili japo wanapata shida za mara kwa mara tofauti na wabunge wa CCM wanaoishi kwa sera za 'kutompinga mkuu' huku wamafunikwa na Ufisadi, ushirikina, kujipendekeza, Majungu na Busara finyu.

USHAURI KWA CHADEMA NA WADAU WENGINE
Kuna haja ya kuunda katiba mbili, Moja ya CCM nyingine ya Watanzania. Hata nchi wafadhiri wanaweza kufadhiri hili ili kupanua Demokrasia. CCM ,wabunge wanke, spika wao waking'ang'ana na Katiba yao, Tuwaache waendelee, Tuunde kamati yetu ya wadau wenye uchungu na nchi, Tukusanye maoni, Tuandike katiba ya Nchi. Siku ya kupiga kura , Watu watapiga HAPANA kwa katiba ya CCM na NDIYO kwa katiba ya Wananchi. Mimi si mtaalamu sana wa sheria japo nina utalaamu katika sekta nyingine bali naamini wazo langu linawezekana.
 
Mkuu, ngoja waje wajuzi wa sheria watakujibu kwa ufasaha.
 
hilo haliwezekani... Hakutakua na tofauti na serikali kivuli
 
Back
Top Bottom