Wakiingia madarakani, wananchi tunageuka kuwa maadui zao, na wanajilinda dhidi yetu, kwanini?

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
8,444
10,921
Hawa watawala waajabu sana, wanatoka miongoni mwetu, lakini wakiishaanza kutawala sisi ndiyo tunakuwa maaadui zao wanalindwa dhidi yetu.
Huu uadui huwa unaanza lini na kwanini iwe hivyo?!

Wanakuja kwetu wanalindwa kwa bunduki za moto, hawataki kuwa karibu na watawaliwa, eti wanahofia usalama wao.

Na hili linaendelea hata wakistaafu, au kuondoka madarakani. Ni lini tunawatisha, ni lini tunatisha hadi wajilinde dhidi yetu wananchi?!

Wengine wanateuliwa lakini nao wanalindwa kweli kweli, adui yao ni sisi hawa hawa kweli au ni mwingine?!

Humo barabarani wanapita kwa kasi hadi kutishia usalama wetu, huwa wanafukuzwa na nani, au wanamkimbia nani?!

Sisi hatulindwi na sisi ndio tunalipa kodi, wao wakianza kutawala kodi wanaacha kulipa, kila kitu bure hata ulinzi wao tunaulipia sisi, na ni sisi wabaya wao tunalipia usalama wao tusiwadhuru, huwa sielewi hili.

Huwa na jaribu kuelewa ni lini huwa tunaanza kuwa tishio kwao, au ni wakati gani.

Kwanini wanatuogopa?!

Huwa najiangalia kwenye kioo sitishi kihiivyo, na nikiwaangalia wananchi wenzangu hawatishi kiiivyo, lakini watawala wanatuogopa, kwanini?!.

Haka ka video ni nyongeza
 
Attachments

  • 2196475_74815219_1243880762464691_5155013924130652160_n.mp4
    797.3 KB
Wakitumbuliwa Uoga dhidi yet Unaisha. Kwa maana hiyo System Ya Utawala Si Rafiki Kwa Watawaliwa.
Au wanatishana wao kwa wao, kama ulivyosema mbona wakitumbuliwa hawapewi ulinzi kurudi nao huku kwetu?!
 
Ukiona kiongozi ana ulinzi kama huo ni wazi hakushinda kihalali na hapendwi. Hofu ya uovu wao ndio kiini cha ulinzi. The guilty are always afraid!
Lakini hili huanza siku ya kwanza kabisa ya utawala wao, sijui hapo wanakuwa wamesha fahamu watawaonea wananchi au kujiandaa kudhulumu wananchi?
 
Huenda hufahamu lakini kinacholindwa ni cheo na sio mtu. Yale madaraka/cheo ndio yanayohitaji ulinzi.
Kuna mtumishi mmoja anaitwa Mwakasege aliwahi kueleza hili jambo kwa urefu na kugusia hata baadhi ya vifungu kwenye biblia kuwa mamlaka za duniani zinatoka kwa Mungu nazo zinakibali machoni pa Bwana sema ndio vile tena wanadamu tumeumbiwa kukengeuka.
 
Kiongozi mwenye ulinzi mkali ana mapungufu mengi kupita maelezo. period
Unadhani ni viongozi hawa au ni watawala? Kiongozi kwanini uwe na ulinzi dhidi ya unaowaongoza? Utawaogopaje unaowaongoza?
Huu utamaduni ulitoka kwa wakoloni, lakini walipaswa kuuacha baada ya uhuru, badala yake wameurithi na wameongeza ulinzi maradufu. Wakoloni walikuwa na sababu ya kujilinda dhidi yetu, walitutawala kwa mabavu, siyo kwa ridhaa yetu. Hawa wa sasa naweza kusema, pia wanfuata huo mtindo wa kututawala kwa mabavu, kiaina. Unakuta kuna mtu anajitokeza kutuomba atuongoze, tunamkataa. Anateuliwa wilaya hiyo hiyo au mkoa huo kututawala sasa tena kwa nguvu, nadhani hawa ndio wana endeleza haya mambo ya kujilinda.
 
Huenda hufahamu lakini kinacholindwa ni cheo na sio mtu. Yale madaraka/cheo ndio yanayohitaji ulinzi.
Kuna mtumishi mmoja anaitwa Mwakasege aliwahi kueleza hili jambo kwa urefu na kugusia hata baadhi ya vifungu kwenye biblia kuwa mamlaka za duniani zinatoka kwa Mungu nazo zinakibali machoni pa Bwana sema ndio vile tena wanadamu tumeumbiwa kukengeuka.
Sidhani kama kila mtu humu anamfahamu huyo Mwakasege, au kila mtu anafuatilia mafundisho yake. lakini bila shaka ninge pingana naye vile vile, kwa muktadha huo. Unaposema cheo/madaraka ndio kinalindwa/hilindwa hata sielewi na haileti maana kabisa, Nikikuuliza unakilinda cheo dhidi ya nani? Kama uliomba lidhaa ya wananchi uwaongoze wakakubali, na ukawa kiongozi wao, kwanini ukilinde hicho cheo au hayao madaraka? umepewa dhamana uitumikie siyo mali yako binafsi hadi uilinde. Cheo ukiteuliwa, pia nidhamana umepewa ili utumike kwenye nafasi hiyo, au madaraka umekabidhiwa uyatumikie kwa nafasi hiyo, sasa unayalinda dhidi ya nani, aliyekuteua asikunyang'anye au WANANCHI AMBAO HAWAKURIDHIA UTEUZI WAKO WASIKUNYANG'ANYE?
Unalinda cheo au madaraka? kwanini? kama yametoka kwa mungu kwanini usitegemee ulinzi wa huko mbinguni? au Mungu alikileta bila ulinzi sasa wewe unakianzishia ulinzi kidumu mwilini mwako?
Any way labda ungeeleza zaidi huyo mtumishi Mwakasege alimaanisha nini kulinda cheo au madaraka ningekuelewa, lakini sielewi kwa uchache wa maelezo yako, hainipi maana ya kunifanya nielewe.
 
Ni katika kutafuta maarifa ndiko kuliko nifanya nikutane na huyo mtumishi.kwa kifupi nilizielewa hoja zake kwa sababu hii.
Kiongozi yeyote nje ya cheo ni binadamu wa kawaida na hata kauli zake hazitakua na uzito tena kwa sababu kilichokua kinasikilizwa sio sauti ya yule mtu bali madaraka aliyovishwa huyo kiongozi na kwa muktadha wa kiimani/kibiblia mamlaka na vyeo vinatoka kwa Mungu kwani ndio anateua mmoja kati ya wengi tena kwa sababu fulani.
Uhalisia wa kauli hiyo upo hapa jaribu kumtazama mtu kama sumaye au Ernest Mangu ambayo kwa nyakati tofauti waliwahi kupata neema za kuwa kwenye mamlaka tazama tofauti zao sasa na kipindi hicho walivyokuwa kwenye vyeo.
Au wale walinzi wa viongozi ukiwauliza wanalinda nini watakwambia ni raisi Magufuli ila kiuhalisia ni yeyote ataye ingia ili mradi ana cheo rais wao watamlinda tu tena kwa weledi ule ule
 
Shukrani kwa jibu lako, sasa turudi kwenye msingi wa swali langu, kwanini wakilinde cheo? na wanakilinda ili iweje, na wanakilinda dhidi ya nani? nini hasa maana ya kukilinda cheo au madaraka uliyopewa na Mungu? Je, ni kweli kwamba wananchi ni hatari kwa vyeo vyao au madaraka yao? wakati wa mkoloni alikuwa na sababu, leo hii kwanini mtu alindwe, au tuache urais na makamu wa rais, kwanini mkuu wa mkoa alindwe? kwanini waziri alinswe, kwanini mkuu wa wilaya alindwe? ni nani mbaya wao, au wananchi wamewatishia lini kuhusu vyeo hivyo, maana wananchi hata hawahusiki kuvitoa vinatoka ikulu, why vilindwe?
 
Wana jimwambafy kwa ulinzi tunaowalipia sisi, na wanajikinga dhidi yetu Sisi.
 
Leo mnabembelezwa mkajiandikishe, mkimaliza mtabembelezwa mkapige kura, wanaongea haya wakiwa wamelindwa na bodyguards wao.

Kwanini tuwapigie kura, wakati sisi ndio maadui zao?!
Nimeona huko wamejizungushia geti la vyuma kutuzuia tusiwasogelee na ulinzi wa bunduki zimebebwa na askari wamejificha nyuso zao, wanatishaaa.

Bado wanatudanganya wao ni sehemu yetu, jamani msijiandikishe na msipige kura. Wakapigiwe kura masaki na oysterbay huko kwenye usalama.

Kataeni uendawazimu huu.
 
Hii mada nzuri na yenye akili sana..wachangiaji tutakua wachache kwasababu ujahitaja CCM ,CUF,CHADEMA, Mbowe,JPM nk..
 
Hii mada nzuri na yenye akili sana..wachangiaji tutakua wachache kwasababu ujahitaja CCM ,CUF,CHADEMA, Mbowe,JPM nk..
Hii inawahusu wote, ukiangalia kwasasa wanakuja hadi huku uswahilini kwetu hawana ulinzi, wakianza kutawala basi tunageuka maadui zao. Huwa tunaanza kuwatisha lini?!
 
Back
Top Bottom