Uchaguzi 2020 Wakereketwa wote wa Vyama vya Siasa, msiweke matarajio makubwa kwa Wagombea wenu

mtingi1

JF-Expert Member
Mar 21, 2020
945
923
Wasalaam wana JF wote, niliwamiss sana kwa muda.

Nimeeleza vema kwenye kichwa tajwa hapo juu.

Ukiwa mkereketwa/mfuasi/mwanachama kindakindaki wa chama chochote cha siasa hapa kwetu Tanzania, chonde USIWEKE MATARAJIO MAKUBWA kwa wagombea wako.

Chochote kinaweza kutokea, ama Mgombea/Wagombea wako KUSHINDA au KUSHINDWA!

Jiandae kisaikolojia kwamba wanaogombea wote ni watanzania, hivyo kushinda au kushindwa ni haki yao wote.

Matarajio makubwa yanakuwa na athari hasi ikiwa matokeo yatakuja tofauti na matarajio yako.

STAY SAFE, KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI.

Maandalizi mema ya UCHAGUZI.

Wenu mtiifu nisiye na chama, MTINGI1
 
Back
Top Bottom