Wakenya wawili waliyokuwa wanachama wa kundi la Al-Shabaab wauawa kwa madai ya kuwa vibaraka

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,484
Wakenya wawili waliyokuwa wanachama wa kundi la Al-Shabaab wauawa kwa madai ya kuwa vibaraka. Abdullah Abdulmajid, na Jared Omambia wameuawa kwa madai ya kuwa majasusi wa NIS ya Kenya na CIA ya Marekani. Hawa jamaa hawana huruma kabisa. Dah! Issa James Mwesiga kutoka tanzania aliuwawa mwezi wa nne wakihofia alikua mpelelezi. leo wakenya wameuawa tena.

=============

Two Kenyans have been executed by Al Shabaab for allegedly spying for the Anti terror police unit (ATPU), M16 and the CIA
CkqPEJIUoAM9wOp.jpg

31 year old Jared Mokae Omambia from Eldoret and Abdullah Abdulmajid Faraj from Mombasa were executed in the remote Somalia town of Jilib after they were suspected of providing intelligence information to the Kenyan government and the CIA which led to the killing of Sheikh Aboud Rogo and Makaburi.

Several Foreign jihadists from Kenya and Tanzania have been executed by Alshabaab this year.
 
Mungu awalaze pema peponi aisei, huo ni ujasiri wa hali ya juu. Kuna watu dunia hii wamejitolea kufanya kazi hatari sana ili tulale na kunywa salama. Hii inataka roho juu, ujasiri na kujitolea kiakili. Hivyo kesho wakati unakunywa bia yako na kubwatuka ovyo ovyo, kumbuka kuna ndugu zako wapo maeneo hatari na wanapitia hali ngumu ili uishi kwa usalama.

Nawapa hongera hao Wakenya, pamoja na yule Mtanzania aliyechinjwa pia.
 
Ni kweli walikuwa majasusi?
 
Hata majasusi wa alshabab wanapopatikana ktk nchi zetu huuawa pia, ni kawaida kwa majasusi kuuliwa wanapobainika
 
Ni kweli walikuwa majasusi?

Sina uhakika kama walikua majasusi, lakini tunajibu taarifa kama zilivyoletwa. Japo nafahamu kuna Wakenya na Watanzania ambao hujipata matatani pale baada ya kujiunga na hivi vikundi, halafu kwenye vita wanawekwa frontline, wanakuta kule kuna chuki za kiaina dhidi yao kutoka kwa hao hao Wasomali wa alshabaab.

Sasa wanapotaka kutoroka na kurudi kwenye nchi zao, wanakamatwa na wengi huuawa hivi kwa kumbambikiziwa ujasusi.
 
Back
Top Bottom