Wakenya watatuelewa tu sisi Watanzania

Mugabe one

JF-Expert Member
Nov 15, 2016
2,327
1,681
Wakati Wakenya wakizidi kuihujumu kiuchumi Tanzania huku wakiwa wamelewa chan'gaa na mirungi hawajui Tanzania imejikita wapi kiuchumi.

Eti wakaibagua Tanzania kwenye usafiri wa ndege kijanjajanja wakatoa orodha ya mataifa 11 kesho yake wakaongeza 8 huku wakijua wazi Tanzania wataiumiza.

Kwa utawala wa Rais Magufuli ni hakika Kenya wataisoma namba hadi za Kirumi kabisa ifikapo 2023 tu, waone mashirika ya ndege makubwa kama KLM kuanza kutua Dar na Kilimanjaro ni ishara bora kama hatuihitaji tena Kenya kupeleka nyanya zetu Ulaya. Kabla ya ndege zetu 2 za mizigo zitakazo kuja miezi ya hivi karibuni mwakani.

Kama kuna taifa linawachomekea maneno ya uovu Wakenya dhidi ya Tanzania, nawasihi wajitafakari upya na wavunje urafiki na hilo taifa, linawapotosha.
 
Duh! mnahangaika sana na Kenya, wamesgawaruhusu pelekeni ndege basi msikie raha.

Hamna chochote mnafaidika nao lakini mmekomaa tu, mnafaidikaje na migogoro?
 
Duh mna hangaika sana na Kenya, wamesgawaruhusu pelekeni ndege basi msikie raha.

Hamna chochote mnafaidika nao lakini mmekomaa tu, mnafaidikaje na migogoro?!
Nimetembea sana nchi za Afrika mashariki. Katika watu wanowaona Watanzania ni ndugu zao basi Wakenya wanaongoza. Kuna tofauti chache ambazo pengine zinaletwa na utamaduni, viwango vya elimu au maendeleo ya kiuchumi lakini kiujumla Wakenya wanatuchulia sisi kama ndugu zao tofauti na sisi tunavyowachukulia wao.

Na ukilinganisha na nchi nyingine ndio kabisaa unaona kama Kenya na Tz(ndio wanavyoiita nchi yetu)ni wamoja. Ukienda Zambia unajihisi mgeni, Waganda wako arrogant na hata lugha yetu adhimu waniita lugha ya wezi!, Burundi wanatukubali lakini wanatuona kama sisi ni economic giants kwa hiyo unakua stranger tu, Rwanda nao kama Burundi lakini ile nchi hua siilewi kabisa saa zote raia wake wako very reserved na pengine baada ya Kagame tuwaombee Mungu wasije wakakinukisha tena.

Mozambique ndio kama mnavyosikia kila siku Wabongo wanatimuliwa na wengine kujeruhiwa na kuuwawa kabisa! Hili hulioni kwa Wakenya na kama lipo ni kwa kiasi kidogo sana. Tuwe positive kwa wenzetu. Hatuwezi kichagua jirani japo tunaweza kuchagua rafiki.
 
Wakenya ni mazuzu sana ardhi yao 30%ndio kilimo ,tanzania 90% ndio kilimo wajitafakari kabla hatujajenga ukuta kwenye mpaka.
 
Nimetembea sana nchi za Afrika mashariki. Katika watu wanowaona Watanzania ni ndugu zao basi Wakenya wanaongoza. Kuna tofauti chache ambazo pengine zinaletwa na utamaduni, viwango vya elimu au maendeleo ya kiuchumi lakini kiujumla Wakenya wanatuchulia sisi kama ndugu zao tofauti na sisi tunavyowachukulia wao

Na ukilinganisha na nchi nyingine ndio kabisaa unaona kama Kenya na Tz(ndio wanavyoiita nchi yetu)ni wamoja. Ukienda Zambia unajihisi mgeni, Waganda wako arrogant na hata lugha yetu adhimu waniita lugha ya wezi!, Burundi wanatukubali lakini wanatuona kama sisi ni economic giants kwa hiyo unakua stranger tu, Rwanda nao kama Burundi lakini ile nchi hua siilewi kabisa saa zote raia wake wako very reserved na pengine baada ya Kagame tuwaombee Mungu wasije wakakinukisha tena.

Mozambique ndio kama mnavyosikia kila siku Wabongo wanatimuliwa na wengine kujeruhiwa na kuuwawa kabisa! Hili hulioni kwa Wakenya na kama lipo ni kwa kiasi kidogo sana. Tuwe positive kwa wenzetu. Hatuwezi kichagua jirani japo tunaweza kuchagua rafiki
Mkenya anatuona sisi jamaa yake kama ambavyo sisi tunamuona Mrwanda ni jamaa yetu. Sisi sio Rwanda ya Kenya.
 
Back
Top Bottom