Elections 2010 Wakenya Wanataka Nini Tanzania??

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Leo nikiwa kwenye daladala, nilikuwa nikisikiliza matangazo ya Amka na BBC. Moja ya habari ya leo ilikuwa kuhusu Uchaguzi wa Tanzania.

Nilishtuka sana kumsikia mwanamke mmoja kutoka Kenya akisema maneno yaliyoko kwenye link hii hapa chini: (jamani jaribuni kuifungua mutamsikia huyo maza alivyokua anaropoka). ni matangazo ya nusu saa lakini utamsikia huyo maza within the first 10 minutes.

Nadhani amesha *i*a na mafisadi tayari.

BBC Swahili - Redio - Amka na BBC
 
Wakenya wanafaidika na utawala wa sasa ambapo Wakenya wanapata ajira kwa urahisi Tanzania, pamoja na mambo mengine. Sera za Dr. Slaa zinaashiria kuwa akiingia madarakani, uhondo huo hautakuwepo tena. Wanasahau kuwa KANU pamoja na kuwa chama chenye nguvu sana, kiliondolewa madarakani!
 
Kwa kweli nilikasirika sana asubuhi, hadi kufikia sehemu nikasema labda BBC wanaipigia debe CCM, kama ukimsikiliza huyo mama anasema amekuwa Tanzania kwa mwezi mmoja tu hivyo hajui lolote kuhusu Tanzania na hawezi kuwaamulia watanzania kwa kusema CCM itashinda si chini ya asimilia 80% hata wale watafiti wa kuchakachua hawakutoa maksi za juu kiasi hicho. Kigezo anachotumia eti ni wingi wa Mabango ya CCM aliyoyaona, Namshauri kama hajui cha kuongea arudi kwao Kenya.
 
Ukweli unauma...

oh yeah, kwamba sisi tu wajinga saaana na jirani zetu wanafaidika na ujinga wetu. na ni kweli inauma saana unapo onekana wewe ni mjinga, si jambo la kufurahia, labda kama wewe umjinga/juha basi utafurahia.
 
Kwa kweli nilikasirika sana asubuhi, hadi kufikia sehemu nikasema labda BBC wanaipigia debe CCM, kama ukimsikiliza huyo mama anasema amekuwa Tanzania kwa mwezi mmoja tu hivyo hajui lolote kuhusu Tanzania na hawezi kuwaamulia watanzania kwa kusema CCM itashinda si chini ya asimilia 80% hata wale watafiti wa kuchakachua hawakutoa maksi za juu kiasi hicho. Kigezo anachotumia eti ni wingi wa Mabango ya CCM aliyoyaona, Namshauri kama hajui cha kuongea arudi kwao Kenya.
Wanadhihirisha ujinga wao hadharani. Hali halisi imejionyesha mpaka sasa kuwa mabango, show za wasanii na wingi wa watu waliosombwa kwa malori hauna mvvuto. Watanzania sio wajinga hivyo, wanajua wanachokitaka na watakisema ifikapo Oktoba 31. Wengine humu wanaoishabikia ccm wana woga mkubwa sasa hivi ccm itakapopigwa chini. Katika woga wao huo wanakuwa kama mbuni ambaye anajificha kwa kuingiza kichwa chake kwenye mchanga, anasahau kuwa kichwa chake ni kidogo, lakini mwili wake wote unaonekana.
 
Hata mimi nilimsikia na kwa kweli alinishangaza sana na kuniacha na maswali mengi. Ila nikajua tu kuwa mfa maji ......................!!!
 
Huyu mama kama yupo humu nchini aondoke mara 1 kabla dr. Slaa hajachukuaa nchi la sivyo .....................................
 
Nyie hamuwajui BBC...subiri muone wanavyojiandalia udirector mwaka huu au hamjui ya Tido!
 
kwa nini ahojiwe mkeii wakati uchaguzi ni wetu wa bongo?

Kuna yule mwanamuziki pia wakenya anayesema JK ni handsome.
Hapo ni baada yakumfananisha na Kibaki na Odinga wao.
Natoka lini wakenya wakaitakia Tanzania mema?
 
BBC swahili, eti wamekuja kuweka kambi TZ! aaliniudhi sana huyo mwanamke, eti, Watu wengi wanamheshimu Nyerere, ndio, ni kweli tunamheshimu. Amekosea kumuhusisha Nyerere na ccm ya leo! ccm ya leo sio ile ya Nyerere, hii ya leo ni mafisadi, akina Lowasa, Mramba, Rostam nk.. hivi hawa ndio wanamuenzi Mwl. Nyerere?
Nyi BBC Kenya, tokeni humu nchini, kama mnaleta habari ambazo hazina mantiki!
 
Unajua wakenya wanatuona sisi kama "bwanamdogo" wao au kakoloni kao kadogo ambako wanaweza kuka-dictate jambo lolote wanalolitaka. Ni watu wa ajabu sana hao nyang'aus. Hawana adabu hata chembe.
 
Wakenya wengi wanaifaidi sana Tanzania kutokana na utawala wetu mbovu. Wana wasiwasi kuwa tukipata utawala imara basi watakosa ile miyanya wanayoipata sasa hivi na kwa vile kule kwao wajanja wachache walishawahi kila kitu, basi watakuwa na hali ngumu tena
 
Back
Top Bottom