Wakenya wanaharibu kiswahili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakenya wanaharibu kiswahili?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pape, Dec 29, 2009.

 1. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  11. Chora kistari chako vizuri. Kistari chako kiwe cheusi na kisijitokeze nje ya kisanduku


  21. Udogo wa neno mtoto ni:
  A. jitoto
  B. kitoto
  C. toto
  D. mtoto
  Jibu sahihi ni B

  huu ni mfano mmoja tu, mingine jisomee mwenyewe yaani ni vituko tupu....

  kwa maelezo zaidi soma katika mitihani ya mwaka 2007 na 2008 ya kiswahili ya darasa la saba (KCPE)!


  Source: http://www.elimu.co.ke/exams/index.php?option=com_docman&task=cat_view&gid=1&Itemid=1
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,186
  Trophy Points: 280
  Wenyewe watakuambia ndio mabingwa wa kiswahili..
  Hawa jamaa ni magwiji wa ulaghai na wamejaaliwa nyama ya ulimi.
  Wamewapiga magiri wazungu na kuwasadikisha kuwa wanakiweza haswa ..
  Wamekuwa wakitamba kwenye vyuo vikuu vya nje kwa ufundishaji wao wa kiswahili,
  matokeo yake wanaofundishwa wanaongea kiswahili kibovu kama jaa la vingunguti..
  Utawasikia wakise iko vile mei najifill vibad sitoweza kukam kazini leo..
  Sasa hiii ni nini?
  Lugha ya wapi?
   
 3. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Unajiumiza bure, kile ni kiswahili chao na hicho unachokisifia ni kiswahili chako. Lugha zote ziko hivyo hivyo, hutofautiana kwa kutegemea eneo, nchi hadi bara. Kiingereza cha London hakifanani na cha New York na hata vitabu wanavyovitumia kama dictionary ni tofauti. Kiingereza cha Afrika Kusini hakifanani kabisa na cha Nigeria na hivyo hivyo kiingereza cha Kenya hakifanani na cha New Zealand na kote huko Kiingereza ndiyo lugha kuu ya taifa. Kiswahili nacho kinatofautiana - cha Zaire hakifanani na cha Uganda na cha Zanzibar hakifanani na cha Mwanza, sasa kwa nini useme cha Kenya ni kibovu na huku wanaelewana wazungumzaji. Nimeshuhudia wakitucheka kwa kuongea Kiswahili kibovu hasa tunaposema maiti huyu badala ya maiti hii, au ng'ombe huyu badala ya ng'ombe hii - sasa hapo !
   
 4. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  teh teh teh...
   
 5. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hata Kihispania kinachoongewa Cuba, Mexico, Venezuela, Chile, Puerto Rico etc ni tofauti sana.

  Ukisema wanaharibu Kiswahili lazima useme wanaharibu kiswahili gani?

  Kwa maana kama unaongelea kuharibu Kiswahili hata watu wa Unguja wanaweza kusema Wabara wanaharibu Kiswahili, kalam wanaiita kalamu, jengine wanasema jingine, markiti wanasema soko, hapana wanasema hakuna etc.

  Kwa hiyo kama Wakenya wanataka kusema Kiswahili cha Unguja halafu wakasema hivyo, watakuwa wamekosea, lakini kuna lahaja za Kiswahili za Comoro na Congo huko unaweza kusikia watu wanaongea Kiswahili hata usifahamu wanasema nini.

  Kiswahili ni kipana kuliko Kiunguja, Kimrima na Kimvita.
   
 6. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  nimekuelewa...
   
 7. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  It's not about merely "wanaharibu kiswahili" au "hawaharibu kiswahili"

  For all I know they could be butchering "Kiswahili Sanifu" according to "Kamusi ya Kiswahili Sanifu"

  But you need to qualify that as such.Kwa sababu ukisema "wanaharibu Kiswahili" bila ku qualify Kiswahili gani, wanaweza kuwa wanaongea lahaja za Turkana au Kisomali huko, ambao nao wakikusikia wewe watasema unaharibu Kiswahili.

  Unanikumbusha nilikuwa naongea na Wamarekani fulani wakaniambia nina accent, na mimi nikawaambia kwangu mimi wao ndio wana accents. Unless you qualify your statements with your posibly subjective point of view, "wanaharibu kiswahili" can be meaningless.

  Ndiyo maana walipojaribu kuandika Biblia ya Kiswahili yenye lahaja nyingi ukakuta kuna a jumble of terms kama "hapo papo" etc etc.

  Kwa hiyo ukiongea kwamba wakenya wana butcher Kiswahili Sanifu nitakukubalia, kwa sababu mifano uliyoitoa hapo juu haiendani na Kiswahili sanifu, lakini je, wamesema kwamba wanatumia Kiswahili sanifu? Vipi kama wanatumia Kiswahili cha hybrid ya lahaja za Kenya?
   
 8. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  No comment mkuu...
   
 9. B

  BrownCurtis Member

  #9
  Oct 4, 2015
  Joined: Nov 27, 2014
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnajua nyi waTz mmekua mkituingilia sana joh!
   
 10. Clarity

  Clarity JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2015
  Joined: Jul 6, 2010
  Messages: 811
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 80
  ??? Kuwaingilia?jamani kiswahili ......
   
 11. naiman64

  naiman64 JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2015
  Joined: Nov 22, 2013
  Messages: 3,726
  Likes Received: 1,285
  Trophy Points: 280
  Uuuwiii nanyie mnakubali!!??? Yamekuwa hayo tena? Kwi kwi kwi
   
 12. a

  ally aziz Member

  #12
  Oct 4, 2015
  Joined: Sep 20, 2015
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mmmh!,,,kuwaingilia?kivipi?kuingiliwa ni kujamiana.Sawa musee!!!!
   
 13. LIKE Niku ADD

  LIKE Niku ADD JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2015
  Joined: Jul 21, 2014
  Messages: 3,435
  Likes Received: 1,639
  Trophy Points: 280
  atisasa ndo uko nafanya nini we manzi au umelipwa chapaa na ccm? ka vp piga nduru sisi wa genge bana uwez uka tu TI-CHI hio lugha bana sisi ndo twamiliki ati
   
 14. SAUTI YAKO

  SAUTI YAKO JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2015
  Joined: Jan 25, 2014
  Messages: 2,313
  Likes Received: 754
  Trophy Points: 280
  Hao Watoto Wa Kenyata,wawil Nafanya Nao Kazi Kwel Kiswahili Chao Ni Shida,na Mmoja Wao Ninakaa Nae Ni Vile Vile Kiswahili Chao Ni Shida Na Wananikera Kwa Tabia Yao Ya Ujuaji
   
 15. J

  Jongwe JF-Expert Member

  #15
  Oct 4, 2015
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 979
  Likes Received: 484
  Trophy Points: 80
  Umenena vizuri kabisa... hata kiingereza cha england na kile kinaongewa Scotland si sawa japo wote waingereza.
   
 16. Jimena

  Jimena JF-Expert Member

  #16
  Oct 4, 2015
  Joined: Jun 10, 2015
  Messages: 24,482
  Likes Received: 92,042
  Trophy Points: 280
  Kuwaingilia kwa wapi?
   
 17. Jimena

  Jimena JF-Expert Member

  #17
  Oct 4, 2015
  Joined: Jun 10, 2015
  Messages: 24,482
  Likes Received: 92,042
  Trophy Points: 280
  Huyu mtoa uzi ako na shida gani? Ye hudhani watz tu ndo hujuanga kiswahili? Sa hapa ndo namshow jinsi vile tunaongea bila shida!
   
 18. David Harvey

  David Harvey JF-Expert Member

  #18
  Oct 4, 2015
  Joined: Jul 17, 2014
  Messages: 1,702
  Likes Received: 1,273
  Trophy Points: 280
  kuna ticha 1 wa kenya alikuwa anafundisha wingi na umoja ilikuwa ni balaa tupu.
  wingi wa KISU anakwambia MIBISU.. sasa iko ni kiswahil cha wapi.
   
 19. bongo-live

  bongo-live JF-Expert Member

  #19
  Oct 4, 2015
  Joined: Jul 3, 2013
  Messages: 824
  Likes Received: 350
  Trophy Points: 80
  immigration mmelala jaman...mijitu imejaa huku!!
   
 20. U

  UHURU JR JF-Expert Member

  #20
  Oct 4, 2015
  Joined: Jul 24, 2014
  Messages: 6,114
  Likes Received: 1,572
  Trophy Points: 280
  Ingekuwa wanaishia kukiongea tu basi isingekuwa ajabu lakini ndio wanatumia hadi kwenye mitihani hilo sidhani kama ni sawa. Maana hebu chukua mfano leo hichi kiswahili chetu tunachokiongea mtaani ndio kitumike kwenye mitihani!
   
Loading...