Wakenya Wamshukia Magufuli Amuachie Gichana (Mfungwa wa Kisiasa kutoka Kenya)

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
13,767
2,000
upelelezi wa utakatishaji pesa una vikwazo vyake
Inategemea na upande wa pili mihela ilipoibiw/kupelekwa una respond vipi legal queries kutoka kwa DPP,akae tu sio papai hilo kusema litaoza
kuhusu uamsho nikuulize,mbona tokea wamewekwa ndani zanzibar imepoa?,makanisa hayachomwi wala mapadri hawauawi
Nimeandika mara tatu kukujibu mara zote nimefuta. Na hiki nilichotaka kukwambia nimefuta tena baada ya kusoma Mithali 26:4
 

Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,562
2,000
Wametuacha mbali wapi? Hujaona wakenya kibao wanakuja shangaa shangaa Tanzania? kenya ni nchi ya kibepari , wachache tu ndio wenye maendeleo , wengi ni masikini sana .

Mkuu hata Nchi zilizo endelea wapo Masikini ,tuna Wachina kibao Nchini na wao ni Masikini ?
 

Wo shi niubi

JF-Expert Member
Aug 14, 2015
1,069
2,000
Huyo Jamaa Gichana sio money laundering tu, Kenya semeni vizuri huyo Jamaa ni drug dealer na kwao ni Kisii, na alidakwa Enzi za Kikwete, pindi kikwete alipokwenda Kenya kuhutubia Raila alijaribu ku-convince Uhuru aongea na kikwete ili waweze kumtoa, ni kama Kikwete aliwapotezea, Namfahamu huyo jamaa driver mmoja alikuwa alinipa story zake kitambo jinsi alivyodakwa Tz.
 

kenna

JF-Expert Member
May 30, 2014
2,458
2,000
Mkuu hata Nchi zilizo endelea wapo Masikini ,tuna Wachina kibao Nchini na wao ni Masikini ?
Sawa kabisa nchi zina watu masikini , lakini la kutuacha mbali kiuchumi ni wapi ? Uchumi wao unakuzwa na mabepari wachache waliojilimbikizia ardhi kubwa nchini mwao , huku wananchi wao wakiwa maskini sana, uchumi wao si rafiki kwa maslai ya wote bali kwa wachache mabepari , kwa hilo watanzania tupo mbali , fursa za kiuchumi ni kwa wote .
 

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
5,424
2,000
Marekani ameanza kuwatumia wakenya kumsambaratisha magu hapa tutashuhudia mazingaombwe ya kila namna ilimradi jiwe akwame......ule ugomvi na barick gold mine hautamuacha magu salama
 

Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,562
2,000
Wewe ni Mwanasheria!? Sheria za Nchi zinasemaje juu ya Kosa husika!?

Mkuu sio lazima uwe Mwana Sheria ,yapo mambo mengine yana onekana kwa Macho.Kwanza huyo bado ni Mtuhumiwa sababu haja patikana bado na Hatia .Pili hakuna Sheria yoyote (Kali) isiyo toa Uhuru wa kujieleza kwa Mtuhumiwa yeyote yule ,mpelekeni Mahakamani msishikile tu kama vile mna Mfuga.

Tuzingatie Utawala wa Sheria ili kudumisha Amani ya Nchi.
 

DrLove69

JF-Expert Member
Jan 20, 2018
3,117
2,000
Mkuu sio lazima uwe Mwana Sheria ,yapo mambo mengine yana onekana kwa Macho.Kwanza huyo bado ni Mtuhumiwa sababu haja patikana bado na Hatia .Pili hakuna Sheria yoyote (Kali) isiyo toa Uhuru wa kujieleza kwa Mtuhumiwa yeyote yule ,mpelekeni Mahakamani msishikile tu kama vile mna Mfuga.

Tuzingatie Utawala wa Sheria ili kudumisha Amani ya Nchi.
Nimekuuliza SHERIA YA NCHI INASEMAJE KUHUSU MASUALA YA KESI HUSIKA!? Nipe jibu tafadhali.
 

Jmc06

JF-Expert Member
May 11, 2016
1,924
2,000
Kuna kitu sijaelewa hapa, hivi 2013 - 2018 ni miaka 7?, na wamerudia mara mbili mbili.. Hii habari ni feki au mwandishi hesabu zimempita pembeni?
 

Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,562
2,000
Nimekuuliza SHERIA YA NCHI INASEMAJE KUHUSU MASUALA YA KESI HUSIKA!? Nipe jibu tafadhali.

Mtu yeyote atakaye-
(a) jihusisha, moja kwa moja au kwa njia nyingine katika muamala
unaohusisha mali itokanayo na ya mapato ya fedha haramu akiwa
anafahamu au anapaswa kufahamu au alipaswa kufahamu mali hiyo ni ya
mapato yatokanayo na makosa ya uhalifu ambayo ni msingi wa
utakatishaji wa fedha haramu;
(b) badili,hamisha,safirisha, pitisha mali ikiwa anafahamu au anapaswa
kufahamu au alipaswa kufahamu kuwa mali hiyo ni ya mapato
yatokanayo na uhalifu ambayo ni msingi wa utakatishaji wa fedha
haramu, kwa malengo la kuficha, kupoteza ukweli au chanzo halisi cha
mali hiyo kuwa ni haramu au kumpa msaada mtu yeyote aliye husika
katika kufanya kitendo hicho kwa lengo la kukwepa madhara ya kisheria;
(c) ficha, funika ukweli, zuia upatikanaji wa ukweli,
chanzo,mahali,Uhamishaji wa umiliki, mzunguko, au umiliki wa au haki
kuhusiana na mali hiyo, akiwa anafahamu au anapaswa kufahamu au
alipaswa kufahamu kuwa mali hiyo imepatikana kwa mapato yatokanayo
na fedha haramu
(d) jipatia, miliki, tumia au simamia mali, ikiwa anafahamu, au anapaswa
kufahamu au alipaswa kufahamu wa kupokea mali hiyo kuwa mali hiyo
imetokana na makosa ya uhalifu amabyo ni msingi wa utakatishaji wa
fedha haramu; au
(e) shiriki katika, jihusisha na, kula njama ya kutenda, jaribu kutenda, saidia
au shiriki au wezesha na shauri utendwaji wa jambo lolote lililoelezwa
katika aya (a) hadi (d) ya kifungu hiki atakuwa amefanya kosa la
kutakatisha fedha haramu.
Adhabu za makosa
ya kutakatisha
fedha haramu 13. Mtu yeyote atayevunja kifungu cha 12 cha sheria hii, ikiwa atakuwa na hatia:
(a)Ikiwa ni mtu kawaida atahukumiwa kulipa faini isiyozidi shilingi millioni mia Tano za kitanzania na isiyopungua shilingi milioni mia moja za kitanzania au
kifungo kisichozidi miaka kumi au kupungua miaka mitano; au
(b) ikiwa ni shirika, shirika hilo litatakiwa kulipa faini isiyozidi shilingi za
kitanzania bilioni moja na isiyopungua shilingi milioni mia tano au kuamriwa
kulipa kiwango sawa na mara tatu ya thamani halisi ya mali katika soko, chochote
kitakachokuwa kikubwa.
Makosa ya 14.-(1) Ikiwa kosa katika kifungu cha 12 limetendwa na taasisi au asasi ya
mashirika watu, mtu yeyote ambaye, wakati kosa hilo linatendeka alikuwa-
(a) mkurugenzi, meneja, msimamizi au mbia; au
(b) alihusika katika uongozi,
anaweza kutiwa hatiani kwa kosa hilo na atawajibika kulipa faini kama ilivyoelezwa
katika kifungu cha 13 isipokuwa akithibitisha kuwa kosa hilo lilitendeka bila ridhaa
yake au hakulifumbia macho na alifanya juhudi ya kuzuia kutendeka kwa kosa kama
alivyopaswa kufanya, kwa kuzingatia majukumu yake katika nafasi hiyo na mazingira
yaliyofungamana na utendaji wa kosa.
(2) Mkurugenzi, meneja, msimamizi, mbia au mtu yeyote anayehusika katika
Usimamizi wa shughuli za shirika au jumuiya anaweza kutiwa hatiani kwa kosa chini ya
kifungu kidogo cha (1) bila kujali kuwa shirika hilo au jumuiya hiyo haijatiwa hatiani
kwa kosa hilo.
(3) mtu yeyote ambaye angeweza kutenda kosa kama angetenda kitendo chochote
au angeacha kutenda kitendo chochote, ametenda kosa hilo na atakapotiwa hatiani
atapewa adhabu sawa kama vile kitendo hicho kimetendeka au hakikutendeka na wakala
wake au afisa akiwa katika ajira yake kama itakavyokuwa mpaka tu atakapodhibitisha
kwamba kosa lilitendwa bila yeye kujua na alichukua tahadhari zote muhimu kuzuia
kufanyika , au kutokufanyika kwa kitendo hicho.

HIYO HAPO..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom