Wakenya walivunja utaratibu, wasilaumu

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Mitandao ya habari Afrika Mashariki na kati imekuwa imejichimbia katika habari ya mjini, jinsi ujumbe wa wa maofisa kadhaa wa Nishati kutoka Kenya walivyozuiliwa pasipoti zao jijini Tanga.

Maofisa hao kutoka Kenya walitaka kutembelea bandari ya Tanga wakati ujumbe wa Uganda ambao ndio uliotarajiwa kupokewa na wenyeji maafisa wa Tanzania na maafisa hao wa Kenya ambao walikuwa na lengo la baya la kukwamisha mradi huo wa ujenzi wa bomba la mafuta laikini ulitibuliwa na maafisa wa Tanzania.

Kiini cha mgongano huo ni juhudi isiyo ya kawaida ya Rais Uhuru Kenyata na washauri wake kuhakikisha kwa njia yeyote ile kuwa bomba hilo la mafuta kutoka Sudani ya kusini, yenye mpaka mrefu na Uganda, pamoja na Uganda yenyewe linapitia Lamu badala ya Tanga.

Mwelekeo wa Tanga unatokana na kuwa inaeneo la kina karibu na bandari ya sasa, na reli amabayo inahitaji tu maboresho.

Mradi wa bomba la mafuta kutoka Sudani ya Kusini na Uganda hapo awali ilipangwa uishie bandari ya Lamu,pwani ya kaskazini ya Kenya. Aambako miundo mbinu kadha wa kadha ilianza kupangiliwa na fedha, wabia kupatikana.

Kilichotea ni kuwa baadhi ya washika dau muhimu wa makampuni ya mradi huo, hasa kampuni ya kubwa ya mafuta ya Total yenye makao makuu Ufaransa, ilianza kuwa na wasiwasi kuhusu uendelevu wa mradi huo unaojengwa katikati ya ardhi ya Al shabab ndiyo chanzo cha mzozo.

Kimsingi kupitisha bomba hilo kandokanfdo ya mpaka wa Somalia ni kuwaletea wapiganaji hao wa kigaidi chakula mezani, waamue wenyewe kisiasa walifunge bomba hilo ili kulazimisha Kenya na Uganda kutoa askari wao Somalia.

Vinginevyo watakuwa wanatega mabomu na kuwateka wafanyakazi wa mradi huo hadi walipwe mamilioni ya dola za Kimarekani. Kama jinsi ilivyokuwa katika mwambao wa Somalia.

Cha kushangaza ni kwamba Rais Kenyatta amejichimbia katika kuamini propaganda za maafisa usalama wake kuwa “hali ya usalama Somalia inazidi kuimarika wakati kila siku wa wanashambuliwa kotekote hata ndani Mogadishu.

Anajaribu kuuza fikra hiyo kwa rais Museveni amabaye bado si wazi kama aligundua hilo yeye mweyewe au alishangaa hakulifikiri pale kampuni ya Kifaransa ilipotoa hoja dhidi ya kujenga bomba hilo la mafuta kuelekea Lamu, maskani ya Al shabab. Wakaanza kupingana.

Taarifa zinasema wakuu hao wawili walikutana hivi karibuni Ikulu ya Nairobi ambako hawakuafikiana muafaka unaokubalika na pande zote mbili kuhusu suala hilo.Kenya iling’ang’ania mpango wa awali uendelee, nan i mshikadau mkubwa wa miradi ya mafuta ya Sudani kusini kwani ilisimamia upatikanaji wa amani katika hatua za awali kabla ya kauanza (vita ya ulaji mwaka 2012). Ila makampuni ya Kenya yako zaidi katikamiundombinu, si uwekezaji wa mafuta kama ilivyo kampuni ya Kifaransa na Uganda inakuwa na neno la mwisho kama jirani amabaye bomba hilo la mafuta linapita kwakwe kwa sehemu kubwa.

Inavyoelekea Sudani kunisni yenyewe imelacha suala hilo mikononi mwa mawakala, kwa mafano kampuni ya Total inachoamaua ndicho kinachofuatwa na watawala Juba.

Juba bado wanajipanga baada ya kumalizika kwa vita ndefu vya ulaji hivi karibuni, iliyoanza pale Rais Salva Kiir alipomsimamisha gavana wa jimbo la uzalishaji wa mafuta. Zilikuwa zimewekwa dola milioni 12 katika akaunti ya nje bila ufahamu wa rais kwa Baraka za makamu wa rais.

Rais Kiir alitakiwaaitishe uchaguzi mwingine ndani ya siku 90 kama ‘katiba mpya’ ya Sudani kusini inavyotaka, kwani ma gavana huchaguliwa,lakini kwa mazingira yaliyopo gavana huyo atashinda tena au mtu wake wa karibu.

Hivyo Rais Kiir akaweka mtu wake anayemtakana kupuuza mpangiliao wa demokrasia, akakosana na makamu wake wa Dk Riek Machar, akamfukuza kazi pamoja na mawaziri wanaomuunga mkono. Hao wote wakakaa upande mmoja,wakaondoa wafuasi wao jeshini, vita ikaanzia hapo.

Kwa maana hiyo Ugandandiyo yenye sauti kwani mpaka wote wa Sudni kusini hasa ni Uganda, na Kenya ni upenyo mdogo tu, kama ulivyo upande wa kaskazini wa Ziwa Victoria.

Kwa hiyo Kenya inafanya kila aina za juhudi izuie Uganda kuongea na Tanzania, labda imejaribu kuelewana na baadhi ya watu Sudani ya kusini amabako ina ushawishi si haba, kulegeza kamba kuhusu hatari za usalama, au kulenga upungufu wa gharama bomba likipita Lamu n.k

Kenya inataka popote pale linapojadiliwa suala hilo wajumbe wake pia wawepo, kuzuia sauti ya Tanzania isisikike, na hitilafu (wasaidizi wa Kenyatta) wazipate na kuzioredhesha na za kupitia Tanga zipewe kipaumbele.

Yaani Kenya iwe msemaji kuhusu Tanzania, Uganda isiwe na haja na kuongea na Tanzania jambo ambalo haliwezekani. Ndio maantiki kuandaa ujio wa kihuni katika bandari ya Tanga amabako maafisa wa ‘Cock up’ wa Kenya walichofanya hivi majuzi, kwa kuzamia Tanga na kuingia katika msafara wa Uganda wa maofisa ya Uganda walipotembelea bandari hiyo.

Maofisa wa Tanzania wakauelewa mchezo mchafu huo uliokuwa unaendelea ziwepo pande tatu wakati katika mazungumzo hayo badala ya pande mbili. Ni kama jirani ajilazimishe aingie katika kikao cha mirathi, azuie sauti za ndugu zisikike, atoe busara zake magao uwe mpana.

Kimsingi huo mchafu amabao maafisa wa Uhamiaji na Usalama mkoani Tanga waliugundua, wakazuia pasipoti za maofisa wa Kenya kwa muda- inasemekana saa nzima-amabako hata wakipewa hati zao za kusafiria maofisa hao wa Kenya wasineweza tena kufika sehemu ya msafara.

Kwa hiyo hapakuwa na tatizo la uhamiaji au la hati za kusafiria ila gate crashing, kuingia katika mkutano ambao haukualikwa, tenakwa kuparamia ujumbe wan chi jirani, ili uwe mjumbe wa nchi jirani, ili uwe wa Afrika Mashariki badala ya Uganda . Labda unyang’au?
 
Tatizo lililopo mkuu ni kwamba sisi watanzania tunafanyakazi zetu.kama kondoo.upole umepitiliza. wakenya wanatake advantage ya upole wetu na kutuona majuha wa kutufanyia vitimbi.jana nimemsikiliza katibu mkuu wizara ya madini akiwa na wafanyabiashara wa mafuta.hana confidence ya.kueleza wananchi/mwandishi wa habari comperative advantage yetu dhidi ya kenya.katika mradi wa mafuta.anaeleza tu kuwa bandari yetu inakina kirefu na tutatengeneza ajira! useless pale ndio palikuwa pa kushusha nondo kama ulizotoa hapo juu.kuwakandia wakenya hata kueleza namna gharama za uwekezaji kwetu zitakavyokuwa ndogo kwa figures,kina cha Tanga angetaja kwa ujazo dhidi ya kile cha kenya! kazi wanapata vilaza hii Tanzania.Katibu mkuu wa wizara anaongea kwa kigugumizi swala tunaloshindania! Hovyoo kabisa.
 
Back
Top Bottom