msuyaeric
JF-Expert Member
- Dec 18, 2014
- 838
- 1,167
Imeelezwa kuwa wakati serikali ikiendesha zoezi la kuweka mipaka katika Pori tengefu la Loliondo, makundi ya wananchi kutoka Kenya wamewavamia askari na kuwashambulia kwa silaha za jadi ikiwemo, Mishale, Mkuki na Marungu, watu hao ambao wamejiweka kama wananchi wa kijiji cha Ololosokwani wametokea Kenya maeneo ya mpakani na kuingia kwaajili ya kuzuia uwekaji wa mpaka wa Pori tengefu la Loliondo kwa kuwa ndipo yalipo malisho ya Mifugo yao,
Katika vurugu hizo wamewajeruhi askari kadhaa waliokuwa wakifanya doria katika maeneo hilo, ambapo walijeruhiwa wakati wakijaribu kuwatuliza watu hao wasifanye fujo, baada ya Askari kujeruhiwa iliwalazimu kutumia nguvu kidogo ili kutuliza fujo hizo ambapo baadhi watu hao walijeruhiwa, ambapo imeelezwa kwamba majeruhi hao wamepelekwa katika Hospitali za Kenya za Posmoru na Lalemtya Wilaya ya Narok
Vurugu hizo zinatokana na hamasa iliyofanywa na baadhi ya Viongozi wakenya ambao wametajwa kuwa na Mifugo yao katika eneo akiwemo Seneta wa Count ya Narok Bw. Oledema na Chief wa Posmoru na matajiri wengine wa Kenya
Baadhi ya wananchi ambao ni Watanzania wamekiri kwamba ipo nguvu kutoka Kenya ambapo wamesema lengo la wakenya hao ni kuhakikisha kwamba serikali ya Tanzania inashindwa kulihifahi eneo hilo kwa kuwa ndilo wanalotegemea kwa malisho ya Mifugo yao na kufanya ujangili wa kuwinda wanyama pori ikiwemo Tembo, wananchi hao wamesema wao wamefurahishwa na kitendo cha serikali kulihifadhi eneo hilo kwakuwa litasaidia sana kuhifadhi malisho ya Mifugo yao kwakuwa Mifugo ya wakenya itaondoka
Wananchi hao wa Tanzania wanasema "sisi tupo tayari kuungana na serikali kwa kuwa tunaamini eneo linalotengwa nikwa manufaa yetu na Mifugo wetu itapata malisho ya kutosha baada ya wakenya kuondoka" alisema mwananchi mmoja kutoka katika kijiji cha Ololosokwani, ambaye jina lake limehifadhiwa
Wananchi hao wamesema zoezi la uwekaji wa bicons za mpaka wa Pori tengefu la Loliondo linaendele vizuri na hakuna fujo kati ya wananchi Watanzania na serikali yao, ambapo wameonya juu ya watu na mitandao inaopotosha kwamba wananchi wa Tarafa ya Loliondo wamepanga kupambana na serikali katika zoezi hilo, wamesema picha zinazosambaa katika mitandao ya kijamii sio za Watanzania na kwamba hakuna Mtanzania yeyote aliyepatwa na tatizo kutokana na vurugu hizo
Wakati huo huo imeelezwa kuwa Mwana mama ambaye ni Jasusi la kimataifa raia wa Sweden bi. Susan Norduland ametuma simu nyingi za smart phone ambazo zimegawiwa kwa baadhi vijana wa Tarafa ya Loliondo katika vijiji vya Ololosokwani, Soitisambu, Kirtalo, Oloipiri, Losoito, Olorieni, Mbukeni Arashi, Piyaya na Malambo, ambapo chanzo cha habari kimesema kuwa simu hizo ziliinginzwa kutoka Kenya na Diwani wa Ololosokwani Mheshimiwa Moloimet Sain'geu ambapo alizipokea kutoka kwa Jasusi hilo pamoja na Seneta Oledama, ambapo simu hizo zitatumika kupiga picha katika matukio mbalimbali yanayohusu Uhifadhi na kumtumia Jasusi huyo mwenyewe na kusambaza katika mitandao ya kijamii, ili kuonyesha kuwa wananchi wa Tarafa ya Loliondo wananyanyasika katika zoezi hilo la uwekaji bicons na matukio mengine
Susana Norduland alipigwa maarufu kuingia Tanzania mwaka 2014 ambapo alipewa PI akitumia hati ya kusafiria ya Marekani na kurudi tena mwaka 2016 akitumia hati ya kusafiria ya Sweden ambapo pia alikamatwa na kufukuzwa tena kwa PI mwaka huo, hata hivyo amekuwa akiingia Tanzania kupitia njia za panya akitokea Kenya kwa msaada wa baadhi ya watu na Viongozi wa Kenya
Kufukuzwa kwa mwanamke huyo ni kutokana na vitendo vyake vya kichochezi ambapo amekuwa akichochea vurugu za kijamii katika Tarafa ya Loliondo tangu mwaka 2001, ambapo alianza na uchochezi wa vita vya kikabila kati ya Wamasai wa Loita na Batemi, ambapo alikuwa mnunuzi mkubwa wa Silaha za kupigania zilizokuwa zikiingizwa kwa njia za haramu, baadae kuanzisha mtandao wa uwindaji haramu wa Tembo, ambapo alikuwa mfadhili wa wawindaji haramu na mnunuzi mkubwa wa meno ya Tembo na kuendeleza uchochezi wa migogoro kati ya Hifadhi na vijiji kwa mwamvuli wa kujifanya mtetezi wa haki za wananchi wa Tarafa ya Loliondo
Sent from my SM-A325F using JamiiForums mobile app