Wakenya waichukua Samunge; Waanza kujitangaza kwamba iko Kusini mwa Kenya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakenya waichukua Samunge; Waanza kujitangaza kwamba iko Kusini mwa Kenya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Jun 28, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=1][/h]
  *Waanza kujitangaza kwamba iko Kusini mwa Kenya
  *Waanza kutoa takwimu potofu kuwadanganya watu
  *Wageni sasa wapitia Kenya kuelekea Samunge
  *Mbunge ataka Serikali iingilie kati, ikanushe uongo
  Na Mregesi Paul, Dodoma
  [​IMG]


  MBUNGE wa Ngorongoro (CCM), Kaika Telele, amesema Wakenya wameanza kujitangaza kimataifa, kwamba Kijiji cha Samunge kilichopo Loliondo Mkoa wa Arusha, hakiko Tanzania bali kiko Kusini mwa Kenya.

  Telele alitoa madai hayo bungeni jana alipokuwa anachangia mjadala wa hotuba ya makadirio ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012.

  “Napenda kumzungumzia Babu wa Loliondo kwa sababu amefanya mambo makubwa sana na naishukuru Serikali kwa kumpa ushirikiano wa karibu.

  “Nawashukuru pia wote waliokwenda Loliondo kupata kikombe cha Babu, waliopona ndiyo wanaojua Babu amewasaidiaje kwa sababu hiyo ni siri yao.

  “Pamoja na kwamba Kijiji cha Samunge kiko Tanzania hivi sasa Wakenya wanajitangaza kwamba kijiji hicho kiko kusini mwa Kenya… huu siyo ukweli kabisa kwa sababu wanafanya hivyo ili wageni wanaokuja kwa Babu wapitie Kenya.

  “Wanawadanganya watu kwamba, kutoka KIA hadi Samunge ni kilomita 800, wanasema kutoka Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyata hadi Nairobi ni kilomita tatu, wanasema kutoka Nairobi hadi Samunge kupitia Loliondo ni kilomita 45 wakati usahihi ni kwamba ukitoka Loliondo hadi Narok ni kilomita 156 na umbali halisi wa kutoka Narok hadi Samunge ni kilomita 200.

  “Hawa Wakenya ni watu wa ajabu sana. Wanawadanganya watu kwa sababu kila kitu kizuri kinapopatikana Tanzania wanasema ni chao. Serengeti wanasema ni yao, Kilimanjaro wanasema ni yao, kwa nini Serikali yetu haikanushi taarifa hizi?

  “Mimi sielewi kwa nini Serikali yetu iko kimya. Wakenya sasa wanapata umaarufu wa Samunge wakati siyo kijiji chao. Serikali isikae kimya, ijibu kauli hizo na iwaeleze watu ukweli badala ya kuendelea kukaa kimya.

  “Halafu muelewe kwamba wagonjwa wengi wanaoingia Samunge wanatoka Kenya, wengi wao siyo Wakenya bali ni wageni kutoka nchi nyingine wanaolazimika kupitia katika nchi hiyo kutokana na taarifa za uongo zinazotolewa,” alisema Telele.

  Katika hatua nyingine, alisema mgonjwa mmoja kutoka nchini Malawi amemzawadia Babu gari aina ya Toyota pick up lenye namba za usajili BL 9238 baada ya kupona kupitia kikombe cha Babu.

  “Nawaambia Babu yuko juu kama mkungu wa ndizi. Kuna mtu mmoja kutoka Brantyre, Malawi alifika Samunge akapata kikombe, baada ya kupona kabisa ugonjwa wake, sasa ameamua kumzawadia gari Babu,” alisema.

  Akizungumzia ujenzi wa barabara ya kutoka Mto wa Mbu -Loliondo kupitia Mbuga ya wanyama ya Serengeti, mbunge huyo alisema lazima barabara hiyo ijengwe kama ilivyoainishwa katika ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

  Aalisema kuwa, pamoja na kwamba baadhi ya wanaharakati hawataki barabara hiyo ipitishwe katika Mbunga ya Serengeti, ujenzi wa barabara hiyo ni lazima kwa kuwa haitakuwa barabara ya kwanza kupitishwa katika mbuga za wanyama.

  Katika maelezo yake, mbunge huyo liitolea mfano barabara inayotoka Dar es Salam kwenda Iringa ambayo inapitia katika Mbunga ya Wanyama ya Mikumi ingawa mbuga hiyo ina idadi kubwa ya Wanyama.

  Kwa mujibu wa Telele kinachotakiwa wakati wa ujenzi wa barabara hiyo ni kuwekwa matuta kadiri itakavyowezekana ili kudhibiti mwendo mkali wa magari yanayoweza kuwagonga wanyama pindi yanapokuwa yakipita katika barabara hiyo.

  “Ujenzi wa hii barabaa ni muhimu sana na wananchi wa Ngorongoro wanaihitaji sana na nafurahi kwamba iko katika Ilani ya CCM na imetengewa Sh bilioni 1.600.

  “Kwa hiyo, lazima ijengwe kwa kiwango chama lami kama ilivyoelekezwa na hii hoja ya kwamba barabara haiwezi kupitishwa katika Mbunga ya wanyama hatuwezi kuikubali kwa sababu wanyama hawawezi kuwa kikwazo cha maendeleo,” alisema.

  Hata hivyo, wakati mbunge huyo ana msimamo huo, Serikali imekwishapeleka barua Ufaransa kueleza kuwa kilomita 53 zinazokatiza kwenye mbunga zitabaki kuwa za changarawe na lami itaishia kwenye kingo za mbunga.
   
 2. m

  mwelimishaji Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sishangai hata kidogo kwani Cha Mjinga Huliwa na Wajanja. Isitoshe Loliondo si ilikwisha uzwa kwa Waarabu? Nchi hii inamegwa vipande vipande.
   
 3. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Tanzania haina mwenyewe wakiweza Wakenya wabebe hata mtutu kuja kuchukua madini.
   
 4. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 524
  Trophy Points: 280
  Karibu Wakenya, hata shule ya msingi lsanga niliyosoma Mbeya nayo iko magharibi mwa Nairobi.
  Tehe tehe tehe
   
 5. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Dalili ya kuchanganyikiwa hawa. Kila kitu cha kwao. Roho ya umimi itawamaliza.
   
 6. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nani Babu mzee kamba! Muongo sana huyu mzee
   
 7. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Sasa kama sisi wenyewe hatujitangazi na nchi hii ni kama haina mwenyewe unategemea nini? Kuilaumu Kenya kuhusu issue ya babu ama mt. Kilimanjaro ni kupoteza muda. Kama wizara ya utalii ingekuwa na uwezo wa kujitangaza inavyotakiwa tusingekuwa tunaongelea hii issue hapa. Uzembe wetu ndio unawafanya wengine watake advantage.
   
 8. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nami nilisoma Isanga. Ulimaliza mwaka gani?
   
 9. k

  king of heavenn New Member

  #9
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 27, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mwaliimu nyerere anatokea kenya
   
 10. TinyMonster

  TinyMonster JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Nawakaubali sana wakenya... yaani jamaa bonge ya wapiga promo ya kitu kisichokuwa kwao. Lakini tujilaumu sisi, tumeifanya Samunge kuwa sehemu ya utalii na bado tumeshindwa kuitangaza. Nimeangalia kwenye majarida yote ya utalii yanayotolewa pale Tanzania Tourist Board lakini sijaona Samunge zaidi ya matangazo ya hoteli za kitalii. Nadhani TTB walitaka 10% ili wamtangaze babu.

  Anyway, nafikiria kitu cha kupafanya kwetu Ngara kuwe kwenye Main Stream najua ndugu zangu Wakenya hawataniangusha... watasema Ngara iko mpakani mwa Kenya.
   
 11. God bell

  God bell JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 581
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Hii nchi imebaki ukiwa haina mwenyewe. Wacha Wakenya waibebe hata kichwani wakipenda. Zambia nao wajikatie sehemu kule tunduma.
   
 12. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Wakenya wakiweza waje watutawale tuwe koloni lao moja kwa moja.
   
 13. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  kweli mkuu tena pamoja na kufumbuliwa macho ngoja tuone kama kuna kitakachofanyika.
   
 14. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  wana JF nisaidieni nijue kwa nini waKenya wanashupamalia barabara ya ngorongoro isijengwe? wanapita huku na kule wakijiita wanaharakati wa mazingira wakitema cheche. nimewasikia kwa sikio langu BBC ya mwanetu Zainab Machibya. Awali walitupiga zengwe tusiuze meno ya tembo yaliyoshikwa kutoka kwa mapocha. Jamani kuna nini?? Anayejua undani atubumbulushe.
   
Loading...