wakenya waandamana mpaka bungeni

TOWNSEND

JF-Expert Member
May 8, 2011
2,598
460
Civil society occupaying parliament kulaani wabunge kujiongezea mishahara kwa sasa wanalipwa one million na point ksh kama m20 ya tsh per month
live ntv
 
Civil society occupaying parliament kulaani wabunge kujiongezea mishahara kwa sasa wanalipwa one million na point ksh kama m20 ya tsh per month
live ntv

Shauri zao sisi wenzao (TZ) tunapiga hatua kubwa ya kimaendeleo kwa kuwekeza kwenye Technolojia, waache wakalie Demokrasia, demokrasia ushenzi mtupu, sisi kwetu Amri moja tu, toka juu inashuka chini na hakuna kupingwa hapo kati kati, ndio maana tunafanya mambo makubwa tumewekeza kwenye Teknolojia, ona hapa! Tanelec Limited
 
hawa viongozi wa Afrika sijuhi wanaumwa maradhi gani haya Mungu wangu,pesa yote hyo nchi inayoitwa LDC's
 
993091_10151273062357609_571789693_n.jpg



Harakati za waandamanaji kupinga kuongezewa mishahara wabunge wao imechukua sura mpira, ukiukwaji wa haki za wanyama haswa Nguruwe umezidi kuonekana baada ya waandamanaji kuwachinja wanyama hao na kutupa nje ya ukumbi wa bunge.Wengine walikua na vinyago vya pua za nguruwe walivyomwagia damu.

Jengo la bunge lina baadhi ya madoa ya damu kutokana na nyama iliyokuwa inarushwa na waandamanaji.Jeshi la polisi limefanya jitihada za kutosha kuhakikisha waandamanaji hawaingii ndani ya eneo la bunge.Polisi wameamuru waandamanaji waondoke na baadhi wameanza kutawanyika huku wengine wakigaili amri bila shuruti. Ustadi mkubwa umeoneshwa na jeshi la polisi kwani hakuna mtu aliyeumizwa mpaka sasa, lakini kuna wakati vikosi vya kutuliza gharia vililazimika kutumia mabomu kuwatawanya waandamanaji.

Heshima kwa waandishi wa habari ni kubwa na CITIZEN TV wanarusha live.

Jeshi letu la polisi lijifunze kitu Kenya!
 
Shauri zao sisi wenzao (TZ) tunapiga hatua kubwa ya kimaendeleo kwa kuwekeza kwenye Technolojia , waache wakalie Demokrasia, demokrasia ushenzi mtupu, sisi kwetu Amri moja tu, toka juu inashuka chini na hakuna kupingwa hapo kati kati , ndio maana tunafanya mambo makubwa tumewekeza kwenye Teknolojia, ona hapa! Tanelec Limited
Hapo kwenye bold, umeongea kishabiki zaidi, ukiona mwenzako ananyolewa, na wewe tia kichwa maji, kwa mwenendo wetu wa ndioooooooo usije shangaa tukaishia pabaya zaidi, usichokijua ni kwamba wetu wana njia zao za kujilipa sasa ya nini kuhangaika ...hushangai kila siku majengo yanaporomoshwa ukiulizia ya nani majibu unayo tayari....
 
@Kyenjo: Haki za wanyama ni pamoja na kutunzwa,kulishwa na kuheshimiwa.Binadamu waliostaarabika ndiyo wanaojua mipaka ya kuwatumia wanyama ili kulinda hadhi yao,mazingira na mahusiano baina ya watumiaji wa nyama ama wanyama hao. Kumekuwa na debate kubwa kama wanyama wana haki zozote au ni binadamu pekee mwenye haki juu ya wanyama.Uchunguzi unaonesha kwamba jamii mbalimbali ikiwamo jamii ya Wabudha huheshimu sana haki za wanyama haswa Ng'ombe huku makundi mengine ya dini yakiheshimu haki za wanyama kwa kuchinja kistaarabu na kuwatumia kama alivyoagiza Mwenyezi Mungu kinyume na walivyofanya wanaharakati nchini Kenya. Kwa upande mwingine, wanyama wana haki ya mahusiano baina yao na ndiyo maana binadamu akimwingilia Mnyama hushitakiwa.Pia kwa mila za kiafrika si haki kumbeba kuku miguu juu, kichwa chini au kuleta wanyama kwenye shughuli za kijamii kama mikutano,vikao n.k
 
Hapo kwenye bold, umeongea kishabiki zaidi, ukiona mwenzako ananyolewa, na wewe tia kichwa maji, kwa mwenendo wetu wa ndioooooooo usije shangaa tukaishia pabaya zaidi, usichokijua ni kwamba wetu wana njia zao za kujilipa sasa ya nini kuhangaika ...hushangai kila siku majengo yanaporomoshwa ukiulizia ya nani majibu unayo tayari....

Umetembelea hapa laniki http://www.tanelec.co.tz/ lakini uone mambo yetu ya kiteknolojia?
 
Mkuu Makala Jr, hiki kitendo cha kutuwa nyama hasa nyama ya nguruwe maeneo ya bunge Wakenya wanakiongeleaje, amoja na wabunge pia ukizingatia kuwa nguruwe kwa imani ya watu wengine ni haramu.
 
Back
Top Bottom