pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,344
Hii nayo ni hatari, Civil Society Organisations Director's Forum ambayo ni mkusanyiko wa mashirika 65 ya kitanzania ya haki za kibinadamu na kidemokrasia limeamua kupaza sauti liwe liwalo. Wanalalamika na kulilia dunia kwa kile ambacho wanakiita 'Police State' ambayo mzee mtakatifu kule ikulu ameibuka nayo kwa kukandamiza kabisa upinzani, wanahabari na uhuru wa wananchi wake. Wanasema kwa mwendo huu wa kuminya demokrasia na uhuru wa wapinzani kuwa na vikao vyao, amani ya nchi inavurugwa huku katiba ikinajisiwa na viongozi wanaotawala. Matokeo yake ni wananchi wanaoishi kwa uoga na kujihisi kwamba hawapo huru kwenye nchi yao. Wameangazia sanasana kutupwa selo kwa miezi mitatu kwa kiongozi mmoja wa upinzani, Mr. Freeman Mbowe. Kunani watani wetu watanzania? Mnanikumbusha enzi za Nyayo Kenya. Mbona mmebadilika kiasi hiki? Tuliwajua kwa ustaarabu wenu ila sasa sivyo tena. https://www.africanews.com/2019/04/...n-groups-risks-undermining-peace-in-tanzania/