Wakenya: Tunawashangaa Watanzania, Polisi wa Tanzania wanafanya zaidi ya hiki cha Polisi wa Kenya lakini huwa hawasemi

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,818
5,007
Nikiwa hapa katika viunga vya jiji la Nairobi nimejaribu kupata maoni kutoka wa watu mbalimbali ambao nilitaka kufahamu kuhusu sakata la Polisi kupiga watu siku za hivi karibuni na jinsi suala Hilo lilivyoleta mtafaruku ndani na nje ya Kenya.

Wengi wamesikitishwa na kitendo hicho ila wengi walienda mbali kwa kusema kuwa matendo Kama haya ni kawaida kufanywa na vyombo vya ulinzi kwa nchi za Afrika na hasa wanawashangaa Watanzania walivyoguswa na matukio hayo wakidai kuwa Polisi wa Kenya wamekiuka sheria na Hali za binadamu.

Lakini walienda mbali kwa kusema je Tanzania matendo Kama haya au zaidi ya haya hayajawahi kufanywa na vyombo vya ulinzi, mbona huwa hatuoni Watanzania wakipaza sauti Kama walivyofanya katika suala hili la Kenya.

Ilinibidi kusitisha mahojiano nikaondoka bila kuaga.
 
Ufipa leo imekuwa Nairobi? Usidanganye watu kwamba hayo ni maoni ya wakenya ,ni maoni ya wanaCHADEMA wa ufipa na ukitaka nirudie kwa sauti kubwa nitafanya hivyo. Sababu zifuatazo zinaonesha ni ya ufipa:

1. Ulipokuwa katika viunga vya Nairobi ukikusanya maoni juu ya suala Hilo, Je kulikuwa na umuhimu wa kujitambulisha wewe ni mtanzania? Kama hukujitambulisha walijuaje kuwa wewe ni mtanzania? Hivyo kwa maswali hayo inaonesha ulikuwa ni ubishano wa wakenya na watanzania juu ya majeshi yao na ubishano huo ulitokea UFIPA.

2. Kwa mtu makini hawezi kufanya ulichofanya wewe ugenini ambacho ni kinyume na sheria za nchi husika. Amri yoyote halali inatekelezwa kwa manufaa ya nchi hata Kama ni kinyume na haki za binadamu. Kwa uoga wetu sisi watanzañia ,kweli unaweza kufanya mahojiano nchi nyingine juu ya amri halali ya Rais?

Siku nyingine ukitaka kudanganya kumbuka kanuni moja ya muhimu, unaowadanganya uwe umewazidi akili.
 
Kwa sasa polisi wamejikuta huru kuyafanya maana taifa lote tumetaharuki kwa suala la Corona, halafu kuna baadhi yetu Wakenya tunafanya mambo ya hovyoo, nimesoma sehemu kuna kundi la Wakenya walikamatwa wamejifungia kwenye klabu wanakunywa pombe kimya kimya, sasa kama hao ndio wanasababisha hata tunashindwa kuwasema polisi wakifanya yao.

Lakini uhalisia wa Kenya na Wakenya, polisi huwa hawana hamu ya kupambana na sisi maana huwa wanakumbuka mziki wa miaka ile tulikimbazana nao mpaka uongozi mbaya uliokuwepo wakati huo ukaachia kunyanyasa Wakenya, tulikua tunaishi kama wanavyoishi Watanzania wa leo.

Japo kwa Watanzania kujifanya wanahoji mambo ya polisi Kenya, ni unafiki na ujinga maana mkizingua tutawaletea mapicha humu ya matukio ya kwenu hadi muukimbie huu uzi, hapa nawapa tu kama onja fulani hivi, picha hii ya polisi baada ya kumlipua mwandishi wa habari Daudi Mwangosi hadi akabaki manyama yamezagaa

majeruhi-polisi-na-marehemu.jpg

Nyololo%252520masacre%2525206_thumb%25255B11%25255D.jpg
 
Mnavyotushangaa ndivyo tunavyowashangaa. Hasa ukizingatia kuwa Kenya huwa inajinasibu kuwa nchi ya kidemokrasia na yenye katiba rafiki inayotoa uhuru wa kujieleza, wa kukusanyika na wa mahakama kuliko zilivyo katiba za nchi nyingine zote za EA.
 
Ndio Umemaliza kutetea ukatili wa polisi ?
 
Mnavyotushangaa ndivyo tunavyowashangaa. Hasa ukizingatia kuwa Kenya huwa inajinasibu kuwa nchi ya kidemokrasia na yenye katiba rafiki inayotoa uhuru wa kujieleza, wa kukusanyika na wa mahakama kuliko zilivyo katiba za nchi nyingine zote za EA.
Sasa kama wakenya wanayapitia hayo nasi pia tufuate mkondo?
 
Kuwa na heshima kijana, na acha kujiifariji hapa jukwaani na picha za Marehemu Mwangosi.

Unataka tufukue makaburi tuanze kuleta tena picha za ukatili wa Kenyan Police during the post election violence 2007 - 2008?

Your police massacred hundreds of innocent civilians simply because they didn't like a Kikuyu candidate, mpaka Mkapa na JK wakaja kuokoa jahazi.

Kwa sasa polisi wamejikuta huru kuyafanya maana taifa lote tumetaharuki kwa suala la Corona, halafu kuna baadhi yetu Wakenya tunafanya mambo ya hovyoo, nimesoma sehemu kuna kundi la Wakenya walikamatwa wamejifungia kwenye klabu wanakunywa pombe kimya kimya, sasa kama hao ndio wanasababisha hata tunashindwa kuwasema polisi wakifanya yao.

Lakini uhalisia wa Kenya na Wakenya, polisi huwa hawana hamu ya kupambana na sisi maana huwa wanakumbuka mziki wa miaka ile tulikimbazana nao mpaka uongozi mbaya uliokuwepo wakati huo ukaachia kunyanyasa Wakenya, tulikua tunaishi kama wanavyoishi Watanzania wa leo.

Japo kwa Watanzania kujifanya wanahoji mambo ya polisi Kenya, ni unafiki na ujinga maana mkizingua tutawaletea mapicha humu ya matukio ya kwenu hadi muukimbie huu uzi, hapa nawapa tu kama onja fulani hivi, picha hii ya polisi baada ya kumlipua mwandishi wa habari Daudi Mwangosi hadi akabaki manyama yamezagaa

majeruhi-polisi-na-marehemu.jpg

Nyololo%252520masacre%2525206_thumb%25255B11%25255D.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom