Wakenya ndiyo Waafrika wenye roho nzuri kuliko wote kwa mujibu wa Utafiti

Wakenya ni wa2 hatari mno, wengi wao wanaroho mbaya
Wakenya wana roho mbaya kwa Waafrika wenzao kwa wazungu wanajikomba sijawahi ona.Hilo shirika lililofanya utafit ni la wazungu ni kuwa wameangalia mwafrika gani anayelamba sana miguu ya mzungu na kumnyenyekea kupindukial wakaona ni mkenya wako sahihi kabisa
 
Musoma wababe sana kuna siku nilienda huko nilikuwa sijui maeneo vizuri nikachukua boda kutoka mara Dishezi mpaka mkendo kati eti anataka buku 2000 wakati hata kwa mguu ningetembea Ata kilomita moja haifiki.

Nimeishi Tarime 3 years, yasemwayo na yaliyopo ni tofauti, wapo safi kama hutowaletea dharau,na hata wakisumbuana wenyewe kwa wenyewe watahakikisha mgeni anabakia salama.
Na kwa asilimia zaid 80 tabia walizonazo Wakurya wanashabihiana na Kenyan
 
Tangu kabla ya uhuru hadi leo Wakenya wamekuwa na harambee ya kuchangia watoto wa familia zisizojiweza fedha za kuwawezesha kusoma ndani na nje ya nchi. Sisi tunachangia arusi tu kwa vile tunajua tutakwenda kula pale sehemu ya fedha zetu irudi
 
Wakenya wana roho mbaya kwa Waafrika wenzao kwa wazungu wanajikomba sijawahi ona.Hilo shirika lililofanya utafit ni la wazungu ni kuwa wameangalia mwafrika gani anayelamba sana miguu ya mzungu na kumnyenyekea kupindukial wakaona ni mkenya wako sahihi kabisa

Aisee!
 
Kazi ipo!

Na hii ni kwa mujibu wa Kampuni / Taasisi ya Utafiti ya huko Ulaya iitwayo Charities Aid Foundation ( CAF ) ambao imedai kwamba Wakenya na nchi yao kwa ujumla ndiyo wanaongoza kwa kuwa na roho nzuri, ukarimu na huruma kuliko Waafrika wengine wote na wapo katika nafasi ya nane ( 8 ) Kidunia.

Nimejaribu kwa hali na mali kuitafuta nchi ya Tanzania hadi ' top 80 ' hadi hivi sasa sijaiona ila kama kuna Mwenzangu yoyote hapa aliyeiona Tanzania katika Utafiti huu anisaidie kuniambia ipo nafasi ya ngapi.

Hongereni sana na mno Wakenya na ama hakika kwa aina ya ' Matabasamu ' ya Rais wenu Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Ruto na huku mara kwa mara wakionyesha ' Uungawana ' wao hadharani na kuwaunganisheni nyote bila kujali Dini zenu, Makabila yenu na tofauti zenu za Kisiasa hakika mnastahili.

Wewe kama kila siku tu Watu ni Kutekana, Kukomoana, Kupigana Majungu, Kutupana Baharini na Mitoni huku wengine wakipewa rushwa kuhama kutoka upande mmoja kuja mwingine na hapo hapo tena mara mwingine akigoma kuhamia upande fulani basi anabambikiwa Kesi ya ' Ufisadi ' na hujakaa sawa Mtu anaona raha kumuona Mwenzake akiwa na Shida na wala hapendi Kusaidia na Mwenyezi Mungu nae tumeshamsahau hiyo Roho Nzuri kama ya Wakenya tuitoe wapi?

Shikamooni Wakenya wote!

Source: Standard Digital.com

Nawasilisha.
Kaka hivi unawajua Wakenya au unawasoma tu kwenye hayo magazeti,hamia Kenya au nenda ukaishi Kenya ndio utawajua Wakenya mambo mengine tuwe tunafanya tafiti kwanza kabla tu sababu za kiushabiki unakimbilia kucopy na kupaste jambo ambalo hulijui
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom