Wakenya msione aibu, leteni Harambee Stars kwa Mkapa

Guus

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
1,130
823
Leo tarehe 17 mwezi wa 9, Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limekataa kuuidhinisha uwanja wa soka wa Kasarani kutumika katika mchezo baina ya timu ya taifa ya Kenya (Harambee Stars) na Mali wa kufuzu fainali za kombe la Dunia. CAF wamegoma kuuidhinisha uwanja huo, katika mchezo unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi, kutokana na kutokidhi vigezo vya ubora hasa eneo la kuchezea (pitch). Katika kuonesha msimamo zaidi, CAF wamelitaka shirikisho la soka la Kenya (FKF) wawasilishe picha za uwanja mbadala wa Nyayo ndani ya siku hii ya leo, kama FKF inadhani uwanja wa Nyayo unaweza pia kufikiriwa na shirikisho hilo la Afrika. Na endapo watashindwa, CAF wataipanga mechi hiyo kuchezwa nchini Mali.

Mtazamo wangu: Wakenya msijisumbue kutuma sijui picha za Nyayo, ninyi muwataarifu CAF tu, ya kuwa mechi zenu za nyumbani mtachezea Tanzania. Kama ni pitch tu, msihofu hata Manungu-Turiani inafaa.

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom