joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,613
Kwanza sio kweli kwamba hatujui kinachotokea Ethiopia kwasababu hakuna Uhuru wa habari, hiyo ni sababu mbayotumia kuhalalisha udhahifu wenu, kama mauaji ya watu wa kabila la Oromo yanayofanywa na POLISI wa Ethiopia yanaripotiwa na vyombo mbalimbali na dunia inajua, vipi kuhusu mashambulizi ya Alshabab yatokee Ethiopia dunia isijue?.Yes ethiopian troops is regarded very highly, they also have a history of being the only African county never got fully colonized.... But since we are talking about evidenced based discussion here, lets not ely on reputation or heresay, rather lets rely on things that actually happened and are documented by evidence.
1. Unlike Kenya, Ethiopia hua haina vyombo huru vya habari, Kwahivyo habari kama hii iliofanyika majuzi hautaisikia popote kwenye mainstream media, utazipata kwa tu blog twa kisomali . Kuna nyengine ilifanyika 2015 na ikasababisha Ethiopia ianze kuregesha wanajeshi wake upande wa Ethiopia..... Ingia hapa ujionee hilo tukio la 2015
Kumbuka kule Somalia Wanajeshi wa AU wamegawanywa katika Sectors, Ethiopia walipoanza kurudimpakani ikawacha eneo hilo exposed, hii ilisababisha KDF kujigawanya zaidi ili pia walinde hilo eneo manake lilikua haliko mbali na Kenya..
Uganda waliingia Somalia 2007, , Hii ni picha ya Alshabaab Controlled area 2009. Unaona hapo kwa Star ndani ya Mogadishu hapo ndo Uganda ilikua inapigana na alshabaab for control. miaka miwili baadae.
Kumbuka Ethiopia walikua Kismayu in 2005 kabla ya kujitoa, from this map you can see Alshaab was back in full control of all of South Somalia after Ethiopia withdrawal.
Alshabaab 2009
Source
KDF iliingia Somalia 2011 bila idhini ya AU/UN wala mtu yoyote, Miaka miwili baadae hivyo ndo picha ilivyokua
Source
Kama unavyoona,KDF walikua wanacontrol hilo eneo lote baada ya miaka miwili, Ethiopia nao walipoona KDF wameingia Somalia wakarudi pia hao na walikua wana control hilo eneo la blue wakisaidiana na wanamgambo wa asili ya kisomali wanaotoka ukoo flani ambao hausikizani na Alshabaab,.. Uganda na Burundi ambao ndo walikua Chini ya AU bado walikua wako hapo hapo Mogadishu na vitongoji..
Kama nilivyosema hapo juu, hilo tukio la 2015 lilisababisha Ethiopia kuregesha wanajeshi wake, kitu kilichofanya KDF wmbao wako na wanajeshi chini ya 3,600 kujigawanya zaidi ili ku patrol hio sector iliowachwa na Ethiopia,
Hivyo ndivyo Sector ziligawanywa baada ya KDF kujiunga na AMISOM.
Uganda ndo inaongoza with 6,700 troops,ikifwatwa na Burundi 5,432, Ethiopia 5,395, Kenya 3,664, Djibouti 960.
Kama unavyoona, Kenya iko ndani ya Sector 2, Lakini shambulizi ya kambi ya kijeshi lililofanyika Jan,2016 kwa kambi ya KDF iliokua na wanajeshi 200 ilifanyika Eladde ndani ya Sector 3 ambapo Ethiopia ndoo wanafaa walikua wanalinda, lakini baada ya kujiondoa KDF ilibidi ijipeleke huko manake ElAdde haiko mbali na Kenya.
2014, KDF ikiwa ishajiunga na AMISOM na inaendelea na kazi. Ethiopia ilikua inashikilia kaeneo kadogo sana, huko kwengine wameachia wanamgambo wa asili ya kisomali ambao hawasikizani na Alshabaab.... KDF na wanajeshi wake 3,600 bado inaendelea kupiga doria hilo eneo lote..
Source
Ukilinganisha hizo AMISOM sectors na maeneo ambapo Alshabaab bado hupiga Doria wazi wazi unajionea mwenyewe kua licha ya KDF kua na wanajeshi wachache zaidi ndio imefanyikiwa kushikilia doria kubwa zaidi, Uganda na Burundi ndani ya Sector 1 na sector 5 bado wanashikilia Mogadishu na vitongoji na pia hio barabara ya kuelekea Ethiopia ili magari yao yawe yanaweza kuleta mizigo hadi mogadishu.
Bonus: Ethiopia Defence industry ni ya kuigwa https://defence-blog.com/army/ethiopia-produces-israels-thunder-armored-vehicles-under-license.html
Kitu usichojua ni kwamba, jeshi la Amison lilipiundwa kwenda Somalia, kila nchi ilipewa Eneo maalumu la kwenda kukomboa. Uganda walipewa kazi ya kuwatoa Alshabab Mogadishu na viunga vyake, ili kulinda Ikulu na kurudisha Serikali ya Somalia, hiyo kazi walikamilisha, Burundi nao walipewa kukomboa hili Eneo karibu na Mogadishu kama uonavyo katika hiyo ramani. Baada ya Uganda na Burundi kukomboa maeneo waliyopangiwa, kazi kubwa ni kuyalinda na kufundisha jeshi la Somalia ili waweze kujilinda, Uganda na Burundi hawana jukumu la kukomboa maeneo mengine ndio sababu husikii wakisogea hata kilometer moja.
Djibouti yenye askari 900 tu, ndio nchi iliyokomboa sehemu kubwa na wanalinda eneo hilo toka 2015(Block 4).
Kenya na Ethiopia, sio miongoni mwa nchi zilizochaguliwa kuunda jeshi la AMISON, Ethiopia imekua ikishambulia Ethiopia Mara kwa Mara tangu kuanguka kwa Said Barre, kwasababu wanashutumu waasi wa Ethiopia kutoka Jimbo la Somaliland kwamba wanaishambulia Ethiopia na kukimbilia ndani ya Ethiopia, Jeshi la Ethiopia linaingia Somalia sio kwa lengo la kuwapiga Alshabab, lengo lao ni kutengeneza "buffer zone" ili wapinzani wa serikali ya Ethiopia toka jimbo la Somali land ambao wengi ni waisilamu wanapata misaada toka Somalia, kwahiyo majeshi ya Ethiopia yakikaa Somalia kwa muda, huwa yanatoka na kurudi Ethiopia, kumbuka hayapo chini ya Amisom kwahiyo hawapati support ya pesa toka UN.
Kenya ninyi mlienda kwa interest zenu, kwa ujumla ninyi haikujulikana kwa uwazi nini hasa malengo yenu, mwanzo mlisema mnataka kuzuia Alshabab wasishambulie Kenya, tulitegemea mtatengeneza "buffer zone", ghafla mkaanza kuzidi kuingia ndani, bila kujiandaa, kwasababu kama lengo lenu lilikua kwenda kukomboa sehemu kubwa ya Somalia, ni wazi kwamba mngejipanga kwenda na jeshi kubwa litakaloweza kuteka sehemu kubwa ya Somalia, matokeo yake mumezidi kusonga mbele mkiwa na askari wachache ukilinganisha na ukubwa wa eneo, sasa mnauliwa kila siku kutokana na poor planning kuanzia mwanzo.
Kwa kifupi, nchi zote zilizochaguliwa kuunda Jeshi la AMISOM, walipewa majukumu na eneo maalumu toka Mwanzo, walijipanga vizuri na walianda vikosi vyao kulingana na ukubwa wa eneo na majukumu waliyopangiwa, ndio sababu hawauliwi sana kama KDF. Ninyi hamkujipanga, mlikurupuka sana, ndio sababu jeshi lenu linapigwa sana na Alshabab kwasababu ya " Poor planning from the beginning due to luck of precise Vision and missions and very poor military intelligence "