smarte_r
JF-Expert Member
- Nov 8, 2013
- 4,536
- 11,862
boss bado unakaa mwiki au ulishahama?Wewe hapo kwa kuvimbiwa makande una ubavu gani wa kuvua uanachama wa Kenya kwenye huu muungano, ifahamike asilimia 40% ya uchumi wa EAC umemilikiwa na Kenya, hivyo nchi hii ndio baba ukanda huu, hamna anayeweza kumfukuza baba nyumbani.
Narudia tena, hizo ni kauli za mwanasiasa ambaye ameishiwa, anafahamu uchaguzi unakaribia, ndio anatafuta jinsi ya kutibua apate kiki, haya mataifa tunategemeana na hakuna mwenye ubavu wa kumfurusha mwenzie, rais wetu alishalitambua hilo na akaamrisha wana EAC wote waje na kujihisi Wakenya, wamiliki biashara na kila watakachoweza, hapa kwangu mtaani getini duka la kwanza ni la Mtanzania, familia yangu inategemea duka lake kwa bidhaa nyingi tu na haijawahi tokea sku hata moja tukawaza Utanzania wake, cha msingi ukiwa na hela, nenda dukani kwake, nunua ulichkifuata piga stori, sepa zako kafanye mengine.
Pembeni hapa kuna jengo lenye vyumba vya kupanga, yaani apartments, mali ya Mchagga fulani raia wa Tanzania, hapo amewekeza na anategemewa kwa njia moja au nyingine.
Hivyo muendelee kuropokwa na kutokwa povu ni ruksa, lakini mwisho wa siku kila mmoja wetu ataishia kitandani usiku na kukoroma, lakini uhusiano baina ya haya mataifa upo pale pale, raia tunahusiana na kufanya biashara.