Wakenya kupumzika siku ya tarehe 25 october 2017 kusubiri uchaguzi wa marudio

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,506

Serikali ya Kenya imetangaza kuwa siku ya Jumatano itakuwa ya mapumziko ili kuwapa wananchi muda wa kutosha kwa maandalizi ya uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika Alhamisi ya Oktoba 26.

Kaimu Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiang'i ameweka notisi hiyo leo katika Gazeti la Serikali na kufahamisha kwamba Alhamisi ya Oktoba 26 itakuwa siku ya mapumziko pia.

Wakenya watakwenda kwenye vituo kuchagua kati ya Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi Mkuu wa muungano wa upinzani (Nasa) Raila Odinga ingawa alitangaza kujitoa kwenye uchaguzi huo wa marudio siku chache zilizopita.

Hata hivyo Raila amewataka wafuasi wake kususia uchaguzi huo na kampeni zake kubwa kwa sasa ni kuhakikisha haufanyiki kwa madai Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imeshindwa kutekeleza marekebisho muhimu ambayo amekuwa akitaka yafanyike tangu yalipobatilishwa matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8.


Muungwana
 
Duh, mbona mkanganyiko? Which is which? Tumetangaziwa tayari kuna kesi mahakamani itakayo husu mustakabali wa uchaguzi huu, tusubirie jumatano October 25
 
Back
Top Bottom