Wakenya kukomba almasi za Tanzania

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,191
672
Wakenya kukomba almasi za Tanzania :: Kiwanda kujengwa Nairobi kwa msaada wa Urusi
:: Ahadi za kuzuia madini ghafi bado hazijatekelezwa
:: Madini yetu yawatajirisha watu India, Afrika Kusini

NAIROBI, Kenya

KENYA nchi ambayo haina mgodi wa almasi, inajiandaa kufungua kiwanda cha kuchonga madini hayo, wakati Watanzania tukiendelea kupiga siasa.

Serikali ya nchi hiyo, tayari imeingia katika mazungumzo na Serikali ya Urusi, kwa ajili ya kuanzisha kiwanda hicho katika Jiji la Nairobi.

Imeelezwa wazi kwamba kwa kuwa Kenya haina madini hayo, itakachofanya ni kuyakusanya kutoka Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Kenya (KBC), Ijumaa iliyopita, wawekezaji kutoka Urusi walikutana na Makamu wa Rais wa Kenya, Kalonzo Musyoka, katika ofisi zake zilizopo Jogoo House, na kufanya mazungumzo kuhusu kuanzishwa kwa kiwanda hicho.

Mapendekezo ya Warusi hao ni kwamba wanataka kuifanya Nairobi iwe moja ya miji maarufu duniani kwa uchongaji almasi kama ilivyo kwa mji wa Antwerp nchini Ubelgiji.

Timu ya Warusi hao iliongozwa na Balozi wa Urusi nchini Kenya, Valery Yegoshkin.

Balozi huyo alisema wawekezaji kutoka nchini mwake, wamependa kiwanda hicho kijengwe kwenye Ukanda wa Unaozalisha Biashaa Zinazouzwa Nje (EPZ) jijini Nairobi. “Madini ghafi itatoka nchi jirani za Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,” alisema balozi huyo.

Kwa upande wake, Musyoka alisifu urafiki imara kati ya Kenya na Urusi, na kusema Serikali inakaribisha wawekezaji kwenye madini ili waweze kuwekeza kwa kadri wanavyoweza.

Musyoka alisema pamoja na kuwekeza katika madini, Serikali ya Kenya itanufaika katika sekta ya utalii, na akasisitiza umuhimu wa kuzidi kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Yegoshkin, alisema wawekezaji kwenye madini watafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Wizara ya Maliasili, na kwamba wako tayari kuleta vifaa, teknolojia na kuwafundisha Wakenya biashara ya madini ya vito.

Alisema madini yakayochongwa, yatakuwa ya Wakenya, na kwamba wawekezaji hao wako tayari kuanzisha chuo kikuu kwa ajili ya kuwafundisha Wakenya masuala ya madini. Alisema kitega uchumi wanachoanzisha, kitatoa ajira kwa Wakenya, kitasaidia masuala ya elimu, utalii na kukuza uchumi.

Miongoni mwa wawekezaji walioongozana na Balozi huyo kwenda kumwona Musyoka, ni Mkurugenzi wa Eidos-lik Diamond Company, Kim Peter; na Bazolin Konstantin. Pia kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Ludeki Chweya.

Kwa miaka mingi, wachimba madini wazalendo nchini Tanzania wameitaka Serikali izuie usafirishaji wa madini ghafi, lakini hakuna hatua zozote za maana zilizokwishachukuliwa.

Pamoja na kuzalisha almasi, dhahabu na madini mbalimbali ya vito, Tanzania ndiyo nchi pekee duniani, kunakochimbwa madini ya tanzanite.

Mawaziri kadhaa wenye dhamana na madini, akiwamo Daniel Yona aliyeshikilia nafasi hiyo katika serikali ya awamu ya tatu, walishaahidi bungeni juu ya kupiga marufuku usafirishaji madini ghafi, lakini hawakutekeleza ahadi hizo.

Wakati Serikali ilipothubutu kwa kutishia kuzuia usafirishaji tanzanite ghafi, Serikali ya India ilituma ujumbe mzito kuibembeleza Tanzania isizuie usafirishaji madini ghafi.

Inaelezwa kwamba katika jiji la Jaipul pekee, watu karibu nusu milioni wanaishi kwa kutegemea kazi ya ukataji madini ya tanzanite na mengine. Kuzuia usafirishaji tanzanite ghafi, maana yake ilikuwa ni kuvuruga ajira nchini India.

Pamoja na Tanzania kuwa ndiyo yenye tanzanite duniani, Kenya inajulikana kama msafirishaji mkuu wa madini hayo duniani, ikifuatiwa na Afrika Kusini ambayo kampuni yake ya TanzaniteOne, inahodhi kitalu ‘C’ chenye utajiri mkubwa wa madini hayo.

Kiwanda cha kukata almasi cha Tancut mkoani Iringa, kilishafungwa, na hakuna dalili za kufufuliwa.

source: http://www.newhabari.com/mtanzania/habari.php?id=4750&section=kitaifa
 
haya sasa kumekucha,,watu wanafikiria na kuona mbali wameshashtuka,,na ngoja uone moto wao utavyokua,,,hivi sie hata vitu kama hivi tunashindwa kuomba kwa hao tunawaita marafiki wetu wa maendeleo??
 
tunaisubiri serikali yetu itueleze, jee hili wanaliangalia kwa jicho lipi?
 
tunaisubiri serikali yetu itueleze, jee hili wanaliangalia kwa jicho lipi?

au ndio maana wenzetu walikua wana force tuanzishe shirikisho haraka!!...walitaka kuziwahi mali zetu kabla wazungu hawajamaliza,,,yaani hata wao wameshatuona sio tunaviongozi mbumbumbu,,,inatia hasira sana aise
 
SAFI SANA WAKENYA..KEEP IT. Usimwamshe aliyelala...sasa kama watanzania tunawagawia wazungu..si mara mia wachukue waafrika wenzetu..(Its a very painful statement..but I had no better words..)
 
Shein na JK hivi Kenya nao wanaenda kuwatfuta wawekezaji ? Kama siyo inakuwaje wanawapata na hata wamepata kitu kikubwa kama hiki badala ya sisi kukipata ? Wamechukua Nchi juzi hawajaenda kujitambulisha kama nyie vipi sisi ?
 
SAFI SANA WAKENYA..KEEP IT. Usimwamshe aliyelala...sasa kama watanzania tunawagawia wazungu..si mara mia wachukue waafrika wenzetu..(Its a very painful statement..but I had no better words..)

I salute that idea, its betta wazichukue mungiki aise maana kukitokea janga ndipo itkua rahisi kukimbilia
 
sshhhhhhhhh........maendeleo ya almasi yetu ni SIRI!!.....JF nyamazeni.........Ngeleja asije kuwasikia
 
Shein na JK hivi Kenya nao wanaenda kuwatfuta wawekezaji ? Kama siyo inakuwaje wanawapata na hata wamepata kitu kikubwa kama hiki badala ya sisi kukipata ? Wamechukua Nchi juzi hawajaenda kujitambulisha kama nyie vipi sisi ?


Wengine kabla hawajajiuzulu walienda kujiombeleza 'mvua za kutungua' kwenye misafara yao. Na wengi wao wanaenda huko kwa mikeke mikeke na kurudi na masoko ya kahawa (ambayo yapo tayari)..... Safari za kuitangaza Tz nje haziishi, wanapotoka nje wanaenda kujitafutia vi 10% na kusign on our behalf mamikataba ya kipuuzi..... sasa leo hii tunaona, watu wasio chimba almasi wanaweza kuleta wawekezaji wa viwanda vilivyo tayari kwa finished goods na siyo mambo ya kupeleka udongo nje ya nchi....:(
 
is it time to take a gun??!! coz kikwete nae hafanyii kazi malalamiko ya waTanzania kama inavyotakiwa,,,Shein hata haongei kazi yake mikasi,,,Pinda ndio kwanza anafanya live performance through media,,,mawaziri wako bize kwenda nje kutunza vijihela wanavyovipata,,,,can i get myself a gun??
 
is it time to take a gun??!! coz kikwete nae hafanyii kazi malalamiko ya waTanzania kama inavyotakiwa,,,Shein hata haongei kazi yake mikasi,,,Pinda ndio kwanza anafanya live performance through media,,,mawaziri wako bize kwenda nje kutunza vijihela wanavyovipata,,,,can i get myself a gun??

JK can only act kama US ana EU wamesema lakini si Watanzania .Ushahidi upo wa wazi kwamba watu walimkataa Chenge lakini akamrudisha hadi juzi yamemkutana sasa hana la kusema .Kazi sasa kukimbia hata wafanyakazi kwenye May mosi .Mkapa kakimbia Muungano sherehe na yeye kakimbia May mosi .Kenya jamani Kenya .Sisis na mali zetu kimya hivi hivi.Mbona hawajafika Russia kuomba mambo haya ? wanaenda kule kwenye 20% ?

Haya Mungu wape laana hawa.
 
Sawa kama ni njia mojawapo ya kukuza uchumi wao hakuna shida.

Pengine wana mpango wa kuchukua madini from DRC. Sisi hapa kwanza suala la kusafishia dhahabu Japan sidhani kama kuna mkataba wowote.It's nonesense!

Sasa kama ni Tanzania pekee yenye madini ya Tanzanite duniani halafu Tunsaini mikataba ya Kimangungo si ni upuuzi.Serikali iangalie pia jinsi ya kuimarisha upimaji na usafishaji wa madini
 
Back
Top Bottom