wakenya kujenga uwanja wa ndege karibu na mlima kilimanjaro faida kwao au kwetu

Nadhani huijui nairobi vizuri.
Nairobi ni kubwa imepangiliwa na imejengeka Kuliko Dar hili haina Ubishi!



Ni kweli, mkuu. Mimi huwa nashabikia Dar kwa vile ndani ya nchi yetu. Lakini jiji letu kweli limekaa kienyeji sana. Unaposhuka na ndege, unaanza kuona aibu mji unavyoonekana toka juu ukilinganisha na majijji mengine yalivyojipanga.
 
Tatizo la Tanzania ni kumuendekeza rais Mwizi. Akiondoka Jambazi mkuu mtaona mambo yanavyokwenda. Huwezi kuwachekea Wezi na Mafisadi!

Kama ni jambazi atamkabidhi nchi jambazi mwenzake ili aendeleze libeneke. Uhuru wa TZ bado may be after 20years. Maana kila mtu analalamikia ndani ya shuka. Mpaka tuamke.
 
Si tulisema suala la ardhi halimo kwenye mambo ya EAC? Hawa Wakenya sijajua kwa nini hawatupendi, ni kama Waarabu wasivyowapenda Waisraeli bila sababu yoyote!

Mkuu,

kwa nini suala la ardhi lisiwemo? Sisi ardhi yetu tunaifanya nini? Ikiwa hata kujilisha hatuwezi. Kama kuna watakao weza kuzalisha ,tuwakodishe tu,tusiwamilikishe!
Mwalimu Nyerere alisema," uchumi tunao tumeukalia"

Lakini mkuu, viongozi wetu pia si wanamega tu mapande ya ardhi ya ukubwa watakao?
Tuwakodishe wakenya wazalishe, tutapata kodi, na pengine tutajifunza kutoka kwao kutumia ardhi yetu na kupata manufaa.
 
Forget about it!

Mkuu,

Unafuatilia kwa karibu huo mchakato? au ni "forget about it" tu?
Museveni na Kagame wanataka kuwa wa mwanzo kuwa marais wa hiyo federation.

Mkuu, wamarekani kama walivyosukuma kupatikana muungano wa TZ, sasa hivi wako behind the scene kulileta Shirikisho la Afrika Mashariki.
Ili mafuta ya Uganda na South Sudan yawe na easy route na mwanya wa common tariffs.
 
watanzania ebu angalieni wakenya wameamua kupeleka uwanja wa ndege karibu na mlima kilimanjaro kwa upande wa kwenya kweli tutapata wageni wa kutua uwanja wa ndege kia, tatizo nini? Au nikuwa na viongozi wasiokuwa na mtizamo? Wenzetu wanaamua kuuteka mlima wetu uwe wao kwa upande wao
Hii Habari umetoa wapi? leta source sio kuzua maana kulikuwa na April Fools' article kama nakumbuka kuhusu kujenga uwanja, ila hamna project kama hiyo!
 
..Tanzania inajenga bandari mpya eneo la mwambao Tanga.

..bandari hiyo itakuwa karibu na bandari ya Mombasa.

..as long as wanajenga kwenye ardhi yao, sioni kwanini tuwazuie.
 
Ni kweli, mkuu. Mimi huwa nashabikia Dar kwa vile ndani ya nchi yetu. Lakini jiji letu kweli limekaa kienyeji sana. Unaposhuka na ndege, unaanza kuona aibu mji unavyoonekana toka juu ukilinganisha na majijji mengine yalivyojipanga.

Nairobi land surface area: 696 km2 (268.7 sq mi)
Dar es salaam land surface area: 1,590.5 km2 (614.1 sq mi)

Hata Nairobi kuna slums pia tumpe muda mama Tibaijuka tutaona matunda maana ameshiriki kuweka nairobi kuwa ilipo kama head of UN-Habitat
 
usilinganishe uwanja wa KIA na Kenyata,wale wakijenga uwanja ni uwanja kweli hutaamini Kenyata ni KIA mia moja walifanya vile kutudhoofisha na watatudhoofisha zaidi kawakijenga huo uwanja nina uhakika hakuna ndege itakayotua KIA kuleta watalii TZ hata Precision yetu itakuwa ni ya ndani tu tena kibaya zaidi hata precision wana ubia na Kenya airways ni mbaya lakini salama

muro unaammbiwa huo uwanja una urefu wa km 8 akuna ndege itatua kia
 
Wacha wajenge labda itakuwa ni wake up call kwa serikali yetu iliyooza hata haielewi hii dunia tupo karne ya ngapi. Serikali duniani zinakwenda mbele lakini serikali ya bongo kila siku inarudi nyuma. Mwizi hajioni yeye mwizi lakini anaona mwizi aliye mwizi.
 
mbona hatukupiga kura hii ndoa ya wakenya na watanzania,bora tuungane na wazambia tunafanana vitu vingi
hasa utashi,mikenya mijitu ya ovyo sana,yanatuona sisi watanzania kama wajinga,
na nyie mliolazimisha hii ndoa na nyie ni mazuzu wa ovyoo!!!
 
wazambia wao wameomba ndoa? tuambie kwanini wakenya ni watu wa ovyo sana,kwavipi tunafanana na wazambia na mafanikio ambayo tuko likely kuyapata kutoka Zambia ambayo hatuwezi yapata kwa ndoa na wakenya.......!!

Ninachojua,mtu anakuona mjinga kwa sababu fulani fulani,pengine yatupasa kujua kutoka kwako kwanini tunaonekana wajinga ili kama kuna uwezekano wa kubadilika kufaidi matunda ya ndoa yetu na wao.....!!!
 
tatizo kubwa la Tanzania ni kushindwa kuangalia wapi tutabenefit, hilo wakenya wapo makini sana,
Hoja ya rosemarie isingeishia Zambia tu bali Tanzania tungejua kuitumia SADC vizuri tungekuwa mbali sana kiuchumi, Bandari za Tanzania ni Shina Kubwa kwa uchumi wa nchi za SADC, huwezi amini kuna watu wanatoka Botswana, Zimbabwe acha Zambia na Malawi kuja Dar Kehemea, Watanzania tunashindwa kabisa kutumia hii nafasi
Kipindi cha Mkapa angalau kulikuwa kunaonekana mwanga kidogo wa SADC lakini kwa sasa ni Ziro kabisa
 
yaani weweupo kama mimi

sio wazambia tu

hata wamalawi na wamsumbiji tunafanana nao

yaani tulipaswa kutazama south

tungejiunga na malawi zambia na msumbiji
tusingekuwa na wasiwasi wa ardhi na kuibiwa kama tulio nao sasa
 
......................Unajua mara nyingi nimekuwa nikisema kuwa hili shirikisho la Afrika Mashariki na kati ni KIMEO...Mara nyingi watu wanapoongea ubaya wa EAC watu wengi wanasema kuwa watanzania ni waoga,wavivu,wamezubaa awawezi kuchangamkia fursa za EAC nk...Lakini tuwe wazi jamani,kuna tatizo la msingi ktk EAC tazama haya kwa uchache...
1.Kenya wanaukabila usiopingika wala kufichika...na watamani sana uzuri wa Tanzania yetu..
2.Uganda wao wana raisi ambaye hatofautiani na CCM ya huku kwetu,ni mwizi wa kura nk.........
3.Kisiasa Burundi,Rwanda,Uganda na Kenya kidogo hapajatulia...bado kuna vita vya maneno au vya silaha za moto kabisa....
4.Tanzania kwetu ndio bado kabisa ufisadi,ujanja ujanja nk....

Je hilo shirikisho litakuwaje...?
 
Serikali yetu ni maharage ya mbeya ( jike jinga)
itabeba sana watoto mgongoni kwa kutungwa mimba bila mpango

kama isipojifunza uzazi wa mpango kuna siku hii nchi itaamishwa
leo hii ndege za jeshi zinatumia KIA zinachukuwa wanyama
na kupotea nao hakuna anayeshitika mwenye cheo cha kueleweka ni
walinzi na marofa wachache kwenye hiyo chain, Mlinzi wa KIA na kutua

DEGE la jeshi pale uwanjani wapi na wapi? lilitua vipi na kupark?
mkuu wa majeshi na mlolongo wake mzima wapaswa kufukuzwa kazi,
nchi inatoa tu hata huko zambia itakuwa hivyo tu.
Lazima tuwe na uchungu na raslimali zetu kwanza sio kugawa gawa tu

na kama tutaendela kuchagua sura, jinsia, dini, ukanda na ujinga kama huo tutakwisha
 
tatizo hapa hatuna mipango
tunaingia kwenye ndoa tukisubiri kitakacho jiri

ndo matokeo yake
 
wakenya wapo kwenye Shirikisho kwa Interest zao tu,angalia issue ya Maji ya Mto Nile, Wakenya walitukana wote na wakafanya deal na Wamisri japo msimamo wa EAC haukuwa hivyo, sasa wako bize na South Sudan nadhani wanataka kuikamua ile nchi vilivyo

Tanzania inatia huruma sana
 
Back
Top Bottom