wakenya kujenga uwanja wa ndege karibu na mlima kilimanjaro faida kwao au kwetu

zamlock

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
3,840
657
watanzania ebu angalieni wakenya wameamua kupeleka uwanja wa ndege karibu na mlima kilimanjaro kwa upande wa kwenya kweli tutapata wageni wa kutua uwanja wa ndege kia, tatizo nini? Au nikuwa na viongozi wasiokuwa na mtizamo? Wenzetu wanaamua kuuteka mlima wetu uwe wao kwa upande wao
 
Wakenya wakombele kinoma,tanzanite wao inaitwa kenyanite,ml,kilimanjaro wanasema hupo kenya nasasa wakiweka kiwanja tz hawana lao
 
Mkuu,

Umesahau kuwa tumo kwenye mchakato wa kuimarisha EAC, kama sikosei EA federation inakuja 2013. Kwa hiyo chetu chao.
ndio jamaa wa Kenya wanatuambia tuamke!
 
JK yeye wazo lake ni kujenga uwanja mpya wa ndege pale Bagamoyo...!

By the way kwani KIA bado ipo hai tena...! Nilipita hapo wakati mmoja kwa kweli ule uwanja unatia huruma. Siku zinavyozidi kwenda ndio unazidi kuharibika na kuwa hovyo kabisa. Kila huduma inazidi kuw ahafifu, mbovu na chafu kabisa.

Mpaka sasa sijui ni vigezo gani vinatumika kuuita Kilimanjaro International Airport...!
 
wao wakijenga ni sawa, haina athari yoyote kwenye mazingira na utalii, lakini sisi kuweka lami serengeti ni mbaya, kwani tutawamalizia watalii... our road will be a huge attraction to many who dont like the current road situation

lakini kama kawa sie ni kulalama tu.... waache wajenge uwanja, sie tuna viwanja viwili na tuna barabara hadi geti la ngorongoro, foo of kilimanjaro na tutaweka serengeti pia

then we will see who is at advantage
 
watanzania ebu angalieni wakenya wameamua kupeleka uwanja wa ndege karibu na mlima kilimanjaro kwa upande wa kwenya kweli tutapata wageni wa kutua uwanja wa ndege kia, tatizo nini? Au nikuwa na viongozi wasiokuwa na mtizamo? Wenzetu wanaamua kuuteka mlima wetu uwe wao kwa upande wao

----------)))))

Sidhani kama kiwanja kinachojengwa kitakuwa karibu na kilimanjaro kushinda KIA, ni sisi tu kuboresha kia wala hakutakuwa na athari, ukifatilia jiografia vizuri utagundua kia ndo the nearest route ya kufika mlimani. Its not more than 70km. Labda tushindwe kujitangaza tu lkn tatizo lisiwe kiwanja cha ndege upande wa kenya.
 
Kweli ukivuka mpakani pale Mashati unakuta Mji wa Last uliopo Kenya wanaweza kuweka kiwanja lakini ni kukame sana na mlima hauonekani vizuri kuna kilele kidogo cha Sira ambacho ni cha 3 baada ya Kibo na Mawenzi. Miaka ya 1900 Mlima huo ulikuwa Kenya ndio maana hadi leo wana Mji uitwao Rombo wanakotoka waTaita na hawana tofauti majina yao na ya ukoo ya watu wa Mkuu, Rongai, Mashati, kiboro nk
Kwa vile Mramba kashindwa weka lami labda Mbunge wa sasa akapige seng'enge mpaka wote unaotenganisha Nchi hizi mbili kama hataweza endeleza lami, au kuweka vitega uchumi kama Mahoteli maana kuna ukame kwa sababu ya kijiografia upepo wa mvua unaishia magharibi ya mlima, Marangu Kilema kibosho na Machame
Kwa hiyo huko upande wa Kenya ni nyuma zaidi na hakupandiki kirahisi acheni wajenge mradi tutapandia ndege huko. Mlima waje kwetu
 
Wabongo kwa kulalamika tunatia fora. We live in a world of competition! Wake up people! I fully support Kenya if they will provide good service for people who use that airport. Uzalendo kwa uzembe ambao watu hawawezi hata kubuni mipango endelevu ya taifa letu?

Go Kenya.....kama itakuwa ni karibu na sisi wengine tutakuwa tunatumia huo uwanja. You know what? ukila na kipofu usimshike mkono.....Tanzania sisi tumeamua kuwa watu wa kulalamika and ofcourse unavuna unachopanda. KIA imekaa hapo weee..naona inajifia..shirika la ndege watu walishalifilisi siku nyingi..na bado watu mnalalamika eti Kenya wanataka kujenga uwanja wa ndege? let them do it..si wana ndege za kutua hapo?
 
Sioni sababu ya kushangaa kwa nini Kenya inajenga uwanja. Cha kushangaa zaidi ni kwa nini Tanzania haiboreshi usafiri wa anga katika karne hii. Angalia viwanja vyote vya tanzania ulinganishe na vile vya kenya
 
Hawa wakenya wanadai mji wa Nairobi ni mkubwa kuliko miji yote EAC wakati mji wenyewe kwa Dar unaingia mara 3 hivyo usishangae wakisema Mt Kilimanjaro iko kwao,Serengeti Manyara,Ngorongoro hivyo kujenga uwanja kwao sio tatizo wameanza kuuza rasilimali zetu kitambo hawa jamaa wanataka hata mashamba yote yawe yao tusipoangalia huu muungano hautadumu zaidi ya miaka 5:embarrassed:
 
Tatizo liko wapi? Kuna Uwanja wa ndege wa KIA, Kuna Uwanja wandege wa Arusha na kuna Uwanja wa Ndege wa Moshi - ambao sijui hali yake kama unatumika. Ni changamoto kwa watanzania kupanua viwanja tulivyo navyo na kuwa na shirika imara la ndege.
 
Hawa wakenya wanadai mji wa Nairobi ni mkubwa kuliko miji yote EAC wakati mji wenyewe kwa Dar unaingia mara 3 hivyo usishangae wakisema Mt Kilimanjaro iko kwao,Serengeti Manyara,Ngorongoro hivyo kujenga uwanja kwao sio tatizo wameanza kuuza rasilimali zetu kitambo hawa jamaa wanataka hata mashamba yote yawe yao tusipoangalia huu muungano hautadumu zaidi ya miaka 5:embarrassed:
Nadhani huijui nairobi vizuri.
Nairobi ni kubwa imepangiliwa na imejengeka Kuliko Dar hili haina Ubishi!
 
usilinganishe uwanja wa KIA na Kenyata,wale wakijenga uwanja ni uwanja kweli hutaamini Kenyata ni KIA mia moja walifanya vile kutudhoofisha na watatudhoofisha zaidi kawakijenga huo uwanja nina uhakika hakuna ndege itakayotua KIA kuleta watalii TZ hata Precision yetu itakuwa ni ya ndani tu tena kibaya zaidi hata precision wana ubia na Kenya airways ni mbaya lakini salama
 
Nairobi najua tena sna usitishwe na yale majumba Town centre nenda reserve uone
 
Mkuu,

Umesahau kuwa tumo kwenye mchakato wa kuimarisha EAC, kama sikosei EA federation inakuja 2013. Kwa hiyo chetu chao.
ndio jamaa wa Kenya wanatuambia tuamke!

Si tulisema suala la ardhi halimo kwenye mambo ya EAC? Hawa Wakenya sijajua kwa nini hawatupendi, ni kama Waarabu wasivyowapenda Waisraeli bila sababu yoyote!
 
wao wakijenga ni sawa, haina athari yoyote kwenye mazingira na utalii, lakini sisi kuweka lami serengeti ni mbaya, kwani tutawamalizia watalii... our road will be a huge attraction to many who dont like the current road situation

lakini kama kawa sie ni kulalama tu.... waache wajenge uwanja, sie tuna viwanja viwili na tuna barabara hadi geti la ngorongoro, foo of kilimanjaro na tutaweka serengeti pia

then we will see who is at advantage

mkuu thanks!serengeti highway inapingwa na rivals wetu kiuchumi.hakuna kulalamika wala kuogopa!
 
Hivi kwanini Ule uwanja unaotaka jengwa Bagamoyo pesa zake zisitumike kukarabati Kia na Arusha airport? Maana at this time terminal 3 inajengwa pale kipawa!why kuna na big airport sehemu zilizo karibu dar na Bagamoyo?
 
sioni tatizo kama wanajenga ndani ya eneo la nchi yao, si nchi huru jamani. ngoja wajenge labda na hawa wetu watona sasa thamani ya KIA
 
Tatizo la Tanzania ni kumuendekeza rais Mwizi. Akiondoka Jambazi mkuu mtaona mambo yanavyokwenda. Huwezi kuwachekea Wezi na Mafisadi!
 
Back
Top Bottom