Wakenya hawaielewi Katiba yao wenyewe!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
21,593
2,000
Nimesoma kwamba kuna mswada umepelekwa Bungeni kuhusu baadhi ya marekebisho ya jinsi uchaguzi utakavyofanyika, Bunge la Kenya limeridhia na kuupitisha, sasa Vyama vya Upinzani ambavyo vina wawakilishi Bungeni vinataka kuitisha maandamanio nchi nzima ya kupinga na kumshikiza raisi wa nchi hiyo asisaini kuwa Sheria, sasa Bunge lina maana gani, kama kila mtu asipokubaliana na jinsi Bunge lilivyopitisha basi huingia barabarani kufanya uharibifu ili kushinikiza matakwa yake?

Nina uhakika kabisa kwamba Wakenya (baadhi) hawajaielewa Katiba yao, na wala pia hawaelewi maana ya demokrasia, wanafikitri kwamba Demokrasia ina upande mmoja tu, kumbe demokrasia pia maana yake ni Haki, haki ya pande zote mbili kusikilizwa pia na siyo moja tu!
 

mulanKE

JF-Expert Member
Sep 27, 2016
400
500
Nop according to Kenyan constitution Kuna freedom to peaceful protest like wat the opposition did previously..
 

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
21,593
2,000
Mpinzani Mkuu nchini Kenya Bw. Raila Odinga, amesema kwamba Uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika hapo mwakani hatokwenda tena Mahakamani kupinga matokeo kama asiporidhishwa nayo bali atatumia njia mbadala yaani kuingia barabarani!

Ikumbukwe kwamba nchi ya Kenya, imeandika Katiba mpya ambayo imesema kwamba Tume ya uchaguzi ni Huru, kwa maana ya kwamba Uongozi wake hauteuliwi na Raisi wa nchi na vile vile imetoa uwezo wa matokeo ya Uraisi kupingwa Mahakamani, Mahakama ambayo Majaji wake hawateuliwi na Raisi wa Nchi, lkn pamoja na hayo yote bado Upinzani nchini Kenya unasema kwamba hauiamini Tume wala hiyo Mahakama na hawatapeleka malalamiko yao huko!

Hao ndiyo Upinzani, walikuwa wanalilia Katiba mpya na kudanganya watu kwamba ndiyo muarobaini wa matatizo ya Wakenya, sasa wameipata hiyo Katiba mpya na kwa kuwa tu imeshindwa kuwaingiza madarakani sasa hawataki kuitii, najiuliza swali hivi kulikuwa na haja gani kutumia muda na mabilioni ya fedha kuandika Katiba ambayo hamtaki kuitii?
 

Kibstec

JF-Expert Member
May 21, 2016
1,205
2,000
Una jua sisi VIUMBE VYEUSI huwa tuna matatzo sana maana kamwe HATUWEZI RIDHIKA KWA KILE TUNACHOKIITAJI PALE TUNAPOKIPATA.....haya yanayotokea NCHINI KENYA ni mfano tosha kabsa ya HATA SISI HUKU siku tukipata hitaji la kuwa na TUME HURU ya UCHAGUZI still bado kutatokea WAPUUZI kusema TUME HII YA UCHAGUZI SI HURU...KAMA INAVYOTOKEA SASA NCHINI KENYA......watanzania WENZANGU TUTUNZE AMANI YETU hili ni JAMBO MOJA SANA LA muhimu....KINACHOTURUDISHA NYUMA MPAKA SASA NI KUWA NA VIONGOZI WA UPINZANI WAAJABU SANA wanaoangalia KUUDUMIA matumbo yao Badaala ya kutumiza WAJIBU WAO KAMA VIONGOZI....
 

bily

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
8,040
2,000
Huyu ngosha asije kujiroga akamsaidia Raila moja kwa moja kwani matatizo ya nchi ni makubwa kuliko urafiki na maslahi binafsi .
[HASHTAG]#BringbackBenAlive[/HASHTAG]
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom