Wake za watu wanajiuza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wake za watu wanajiuza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, May 18, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  IMEDAIWA kuwa wanawake wengi wanaofanya biashara ya kuuza miili yao katika maeneo ya Manzese jijini Dar es Salaam ni wake za watu na imegundulika kuwa wanaagizwa na waume zao wakafanye biashara hiyo ili wapate pesa za kujikimu.Hayo yamegundulika katika utafiti wa kina uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Madawa Afrika [AMREF]

  Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Meneja wa Mradi wa Haki za Wananchi wa taasisi hiyo, Michael Kimaryo, wakati wa semina iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa habari za Ukimwi (AJAAT) kwa kushirikiana na taasisi hiyo.

  Kimaryo alisema walibaini hali hiyo wakati walipokuwa wakifanya ufuatiliaji kuhusu mradi huo uliolenga kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya afya ya ukimwi na mambo mengine katika maeneo ya Manzese, Tandale na Kiwalani, Vingunguti na kwingineko

  Alisema wanawake hao wamejiingiza katika biashara hiyo ambayo waume zao majumbani wanatambua hali hiyo na huwaruhusu ili waweze kujipatia kipato cha siku cha kujikimu na familia zao.

  Mradi huo wa AMREF ulianzishwa mwaka 2008 ukiwa na lengo la kuwakomboa wananchi katika nyanja mbalimbali, kuwaelimisha kuhusiana na ugonjwa wa ukimwi na jinsi ya kujikinga na walioathirika kujifunza njia za kuepuka kuwaambukiza wengine.

  Mradi huo ulilenga zaidi maeneo ya Manzese na Tandale.
   
 2. S

  Stapler Member

  #2
  May 18, 2010
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wengi tutakufa!!!!
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ...kwa kutembea na machangudoa wake za watu au kwa kuagiza wake zenu wakajiuze?
   
 4. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,937
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Swali zuri sana hili.
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  Ila kweli miafrika tumechoka kufikiria.
  Unatumwa ukajiuze unakubali, na anayekutuma naye inabidi akajiuze kwa mijibaba myenzie,
  hapo ndio kutakuwa na usawa
   
 6. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  natafakari; inakuwaje? unaanzaje kumwambia wif akajipange barabarani? au wakati mwingine unamlengesha?

  Mungu tuhurumie waja wako na huu mtikisiko!
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hapo unakuta mwanamke asipoenda kujiuza ndio watoto hawali! inasikitisha ...........

  Watu wa chini ndio kila siku anazidi kukubwa na majanga mengine. inatisha
   
 8. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Yeah - Hii ni Biashara Kongwe kuliko zote ambazo zinahusisha CASH!
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo unaiunga mkono?
  Sijaona ukilaani au kupongeza, je unalionaje swala hili la wewe kumtuma mama watoto akatafute riziki kwa njia hii?
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu bado hujakumbwa na ugumu wa maisha, yote haya ni kwa sababu ya ukata, watu wanasaka mishiko
   
 11. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Yet Tanzania has mushrooming Poverty Alleviation programmes!!! which have eroded billions of expenditure through our tax money and the so called busket funding from our famous Development Partners - The GBS Group?

  Hivi MKUKUTA, what has failed? Kwanza wengi wa walengwa hawaifahamu MKUKUTA, yet it is going for the second round?!!!

  Poor mothers, poor kids who in no time will become opharns!!

  Magumu ya maisha yanalazimisha binadamu kujiingiza katika shughuli haramu bila kupenda!!!
   
 12. F

  Froida JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Wanatumwa na waume zao miaka na miaka tafiti zimeonyewsha eneo hilo ndio mtindo wake sio taarifa mpya sana.
  Sasa watafanya nini wakati pato la mkazi halijawahi kukuwa kwa namna ambapo mwananchi ataweza kujikimu hata kupata mlo mmoja kwa siku,inabidi warudi kwnye kazi ya kwanza kabisa hapa duniani,
   
 13. M

  Magezi JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kwa kutembea na wake za watu machangu
   
 14. M

  Magezi JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  binafsi sioni tatizo kwa mdada au mmama akitingwa akitumia mwili wake cha muhimu tu ni kutumia Kinga.
   
 15. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #15
  May 19, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  People we should think out of the Box- hii ni dalili mbaya kwa nchi yetu na ni wazi hii ni matokeo ya hali mbaya ya maisha ya watu ambayo yamewekwa mikononi mwa serikali. Ile ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania imeishia wapi watanzania? Kama kweli sababu kubwa ya watu kubehave namna hii ni hali mbaya ya maisha yaani mtu anajitoa mhanga ili apate pesa za kujikimu basi ni wazi kuwa hawana alternative zaidi ya hiyo hawapaswi kulaumiwa hata kidogo bali lawama zitupiwe kwa serikali iliyoshindwa kuleta unafuu kwa maisha ya walio chini huku wachache wakifaidi na kufuja mali.

  Unaielezaje ulimwengu kuwa nchini kwako kuna wanatuma wake zao kujiuza ili wapate unafuu wa maisha na wakati wengine wanatumbua tu mijihela ya EPA, wanaendesha migari ya kifahari wao, watoto zao hadi mashamba boi wao?? wangapi wanakwenda vacasion nchi za nje na kutumbua tu mijihela ya walipa kodi?? Unajiteteaje?

  Bwana Kimaryo tunaomba profiles za hao waliofanyiwa utafiti- their socio-economic profiles tuone ni watu wa aina gani kimaisha.
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  May 19, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  ooh Jeeeeeeeezaz nashindwa kuamini huyo mwanaume sijui atakuwa hampendi mkewe ,,?
  Kweli wanaume mnashindwa kutafuta namna ya kupata mkate wa kila siku mpaka kuwatumia wanawake kujiuza?
  then akishatoka kwenye Biashara hiyo mwanaume unajisikiaje pale unapokuwa faragha na mkeo?
  mungu tuhurumie tumevuka mipaka ooh nawalilia watoto wetu kwani maadali yanazidi kuporomoka siku hadi siku​
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  May 19, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mlitegemea wafanye nini wakati kila nafasi ya kujiajiri au kuajiriwa mnawapa wageni kwa kisingizio cha uwekezaji?
   
 18. K

  KABAZI JF-Expert Member

  #18
  May 19, 2010
  Joined: Apr 19, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Oh Lord have mercy on us!!
   
 19. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #19
  May 19, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  HII NI KAWAIDA KWA WANAUME WANAOENDESHA MAISHA YAO KWA KUTEGEMEA WAKE/MADEMU WAO,
  huwa unakuta demu yuko fresh,maisha yana uhakika wa kupata mlo,mavazi ,pombe na bangi,etc,unamtokea anakubali,and after few days unajua kuwa anawachuna mabuzi,majamaa ila wewe ndo anakupa bure huduma etc,sasa ukishaoa au kuishi naye akikuaga hutashangaa sana kwani alishakuwa akifanya before hamjawa na uhusiano,
  hawa wanaume siyo kuwa walifunga ndoa halafu baada ya ugumu wa maisha ndio wanawatuma wake zao wakajiuze,
  mimi najua cases ambapo unamkuta kijana ana demu and demu wake ana Buzi,limempa gari kumfungulia glosali/bar/pub then jamaa anaendesha gari and sometime anakuwa manager wa pub ambayo anajua fika kuwa kuna MWANAUME mwingine amevilipia, hivyo unakuwa mpole na ukiona pesa za pamba na matumizi zinaisha unamstua wifey aongee na mzee ili kieleweke ,sasa hii haina tofauti na watu wa manzese ,vingunguti ,buguruni etc isipokuwa ni grade tu ya kuuza wake zao,
  Serikali na ustawi wa JAMII inabidi kutoa mafunzo zaidi kwa watu hawa wenye mtazamo wa aina hii.
   
Loading...