Wake wa King Muswati wachapwa viboko kama wanyama!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wake wa King Muswati wachapwa viboko kama wanyama!!

Discussion in 'International Forum' started by gumzomatata, Sep 26, 2012.

 1. g

  gumzomatata Member

  #1
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 26, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  TANGU Waziri wa Haki wa Swaziland, Ndumiso Mamba, anaswe kitandani anavunja amri ya sita na mke wa Mfalme wa nchi hiyo, Makhosetive Dlamini ‘Mfalme Mswati III', hali ni mbaya kwa wake wa kiongozi huyo.

  Mamba, alinaswa kwenye kitanda cha mke wa 13 wa mfalme huyo, Nothando Dube na tangu wakati huo, walinzi wa Mfalme Mswati, wamepewa madaraka makubwa ikiwemo kuwacharaza bakora hata barabarani na mbele za watu.

  Inaelezwa kwamba wake wa Mfalme Mswati wanafungiwa ndani kama kuku, inapotokea wanakwenda sehemu wanakuwa chini ya ulinzi mkali.

  Ripoti zinasema kuwa endapo barabarani mke wa mfalme atachepuka kwenda hata msalani bila taarifa au atasalimiana na mtu ambaye walinzi wanamjua, hata kama ni ndugu yake, mwanamke husika hucharazwa bakora kama ng'ombe.

  "Ukiwa mke wa Mfalme Mswati ni mateso makubwa. Unavyoishi haina tofauti na ng'ombe anavyochungwa. Ukiwa unatembea barabarani unatakiwa ufuate uelekeo anaotaka bodigadi, ukikosea kidogo unachapwa bakora na vIrungu.

  "Mambo yalikuwa mabaya lakini sasa ni mabaya mno. Kwa sasa nataka kutoka lakini mfalme hataki kuruhusu niondoke. Nipo kama mfungwa, saa 24 nachungwa, sina uhuru hata kidogo," alisema Nothando.

  Mwanaharakati wa demokrasia anayepingana na mtindo wa maisha ya Mfalme Mswati, Lucky Lukhele, aliwahi kuwaambia waandishi wa habari kwamba siyo Nothando tu, wake wake wote wa kiongozi huyo wanaishi katika mazingira magumu afadhali ya wafungwa.

  "Kuna mke mmoja wa mfalme alikutwa getini na walinzi, tena getini kwenyewe kwa ndani halafu geti lilikuwa limefungwa na funguo wanazo walinzi. Ajabu ni kwamba walinzi walipomkuta pale hawakuuliza mara mbili, walimpiga na kumuumiza mno," alisema Lukhele bila kutaja jina la mke huyo wa mfalme.

  Kwa upande mwingine, inaelezwa kuwa mtindo wa maisha ya Mfalme Mswati na wakeze, umesababisha mpaka sasa akimbiwe na wanawake watatu.

  Mke wa sita wa mfalme huyo, Angela "LaGija" Dlamini, ndiye anatajwa kuwa mwanamke wa hivi karibuni zaidi kuondoka katika himaya ya mfalme huyo.

  Mke wa 12 wa mfalme, Inkhosikati LaDube, alitimuliwa Desemba mwaka jana kwa kile kilichobainishwa kwamba aligombana na bodigadi wake.

  Taasisi ya Swaziland Solidarity Network ilieleza kwamba Dlamini, alikimbia makazi ya mfalme baada ya kuwa kwenye mateso kwa miaka kadhaa.

  Dlamini, aliaga anakwenda kuwasalimia wazazi wake kwenye Mji wa Hhohho, lakini aliporuhusiwa alitimka jumla.

  Mfalme Mswati pamoja na tabia ya kupenda kuoa mabikra, vilevile anatuhumiwa kujilimbikizia utajiri wa kutisha, hivi karibuni Jarida la Forbes lilimtaja kwamba anamiliki utajiri wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 200 (shilingi bilioni 300).
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Kwetu tarime tunakata sikio.
   
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wakome¬° tamaa imewaponza
   
 4. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #4
  Sep 26, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Hao hao wanaowachapa viboko ndo walajhivuu wake 30 mzunguko wake ni lini utafikiwa?
  Marehemu Diana wa Prince Charles alifundishwa kumkwea farasi ikabidi huyo Mwl mpanda farasi ampande
  Mswati angefanya km ile ya Dr wa Queen Eliza, Hartings Kamuzu Banda (RIP)
   
 5. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  linaenjoy sana hili jamaa .
   
 6. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Hivi huko hakunaga haki za binadamu?
   
 7. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mfumo dume asilia una raha na karaha zake.
   
 8. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  angelikuwa muisilamu huyo mfalme mswati basi ungesikia wanafiki wa haki za bianadamu ooo anaonea wanawake kwa vile ni kafiri mwenzao wamekaa kimyaaa
   
 9. R

  Rubesha Kipesha Member

  #9
  Sep 26, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mila na desturi zingine hazifai katika dunia ya leo!
  Lol! Unyanyasaji wa hali ya juu, mmh halafu ndie kiongozi
  wa nchi!
   
Loading...