Wakazi wavamia na kukata miti katika hifadhi ya msitu mkoani Tanga

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Serikali mkoani Tanga imeombwa kuingilia kati kabla hali ya machafuko haijajitokeza kufuatia baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kwakombo kilichopo kata ya Kwamsisi wilayani Handeni kuvamia kisha kuvuna zaidi ya hekari tatu kati ya 20 za hifadhi ya msitu wa miti aina ya mikaratusi kwa madai kuwa miti hiyo imepandwa katika eneo lao.

Wakizungumza katika eneo la tukio baada ya zoezi la ukataji wa miti hiyo iliyopandwa miaka saba iliyopita likiendelea,msimamizi wa shamba la msitu wa kwakombo linalosimamiwa na baadhi ya watendaji wa serikali wamesema kitendo cha ukataji wa msitu huo kinakiuka jitihada za serikali za upandaji wa miti ili kujikinga na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kwakombo amesema awali uliibuka mgogoro baina ya wakazi wa kijiji cha Kwakombo na Mratibu wa msitu wa hifadhi ya hatua ambayo ilikwishamaliza na vyombo vya sheria lakini baadae baadhi ya watu wakalazimika kwenda kukata msitu huo hatua ambayo itachelewesha jitihada za serikali za kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

Kufuatia hatua hiyo baadhi ya watu waliohusika na kitendo cha ukataji wa miti hiyo walipotakiwa kuelezea chanzo cha uharibifu huo wamesema shamba hilo wanalimiliki kisheria na hata baadhi ya viongozi wa serikali ya wilaya wanatambua.

Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom