Ulongupanjala
JF-Expert Member
- Apr 9, 2013
- 7,659
- 12,283
Heshima kwenu viongozi wa wizara ya ardhi.
Sisi wakazi wa wilaya ya Muheza Tanga kata ya Ngomeni tunapata changamoto kubwa na hii kampuni ya MAKAZI SOLUTIONS LTD inayopima maeneo yetu ili kurasimisha.
Wamekuja na kanuni yao ya kuchukua asilimia 60 kutoka kila shamba eneo na mwenye shamba kuachiwa asilimia 40.
Endapo mwenye shamba/eneo akitaka hizo asilimia 60 wanazochukua wao inabidi alipie pesa nyingi sana.
Na akishindwa kulipia hizo asilimia 60 wao hutafuta wateja na kuuza eneo la shamba.
Hivi huu ndio utaratibu waliopewa na wizara ya ardhi au ni uhuni wao wakishirikiana na baadhi ya watendaji?
Haingii akilini mtu atunze shamba lake zaidi ya miaka 30 halafu anakuja mtu na kuchukua asilimia 60 ya eneo lote la shamba.
Naomba waziri husika na naibu waziri wako mje kuona wananchi tunadhulumiwa mashamba yetu.
Asante.