Wanabodi,
Wakazi wa Ubungo pamoja na wakazi wa Jiji la Dar es Salam wamempongeza Rais Kikwete kwa kitendo chake kujenga barabara za Ubungo kupambana kupunguza foleni.
Serikali imetenga Sh10.5 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo ili kupunguza msongamano wa magari barabara hizo ni pamoja na Mbezi Luis kupitia Goba mpaka Tanki Bovu, Mbezi kwa Yusuph, Msakuzi-Mpiji Magohe, Tegeta Bunju.
Nyingine ni Mbezi Malambamawili-Kinyerezi, Kimara-Mavurunza, Bonyokwa, Ubungo Maziwa-External, Kimara-Kilungule, Makoka, Makaburini, Kimara-Matosa, Mbezi, Ubungo-Msewe, Chuo Kikuu.
Wakazi hao wanasubiri usafari wa treni yenye uwezo wa kubeba abiria walioketi na kusimama wasiopungua 1,000 kila safari, hizo treni zitakuwa na vituo sita Buguruni, Tabata, Matumbi, Mabibo, Ubungo Maziwa.
Usiulize sana mkuu wangu. Hali ya maisha ya wananchi imeboreka. Hivi sasa wananchi wa kawaida wamejitahidi mpaka wameweza kujijengea majumba ya ghorofa. Maisha bora kwa kila Mtanzania. Kwanini wasimpongeze Rais wao?