Wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro wanashika nafasi ya kwanza kwa kupima virusi vya ukimwi kwa hiari.

Mtoto wa Mkulima

JF-Expert Member
Apr 12, 2007
683
124
Kilimanjaro Yaongoza Kwa VVU.
Wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro wanashika nafasi ya kwanza, kwa kupima virusi vya ukimwi kwa hiari.

Rais Kikwete alizindua kampeni ya kitaifa ya kupima virusi vya Ukimwi kwa hiari Julai 14, mwaka huu katika viwanja vya mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Ripoti ya utekelezaji wa kampeni hiyo, inaonyesha kuwa Mkoa wa Kilimanjaro unashika nafasi ya kwanza, kwa kuwa na watu wengi waliojitokeza na kupima afya zao.

Ripoti hiyo yenye takwimu zinazoanzia Julai 14 hadi Oktoba 16 mwaka huu, inaonyesha jumla ya watu 118,656 katika mkoa wa Kilimanjaro wamejitokeza na kupima afya zao, ambapo wanaume ni 53,536 na wanawake 65,120 ambayo ni sawa na asilimia 73.

http://www.darhotwire.com/home/news/2007/10/25/kilimanjaro_yaongoza_kwa_vvu.html
 
Katika pitapita yangu nikakutana na hii habari. Nadhani kichwa cha habari kinawalakini wangeandika Kilimanjaro ya ongoza kwa kupima ukimwi badala ya waliyoandika.
 
Mkuu watake radhi hicho kichwa cha habari sio, hii ilipaswa kuwa pongezi na ya kuigwa mfano!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom