Wakazi wa Mishamo waomba serikali iingilie kati migogoro ya kila wakati kati wakulima na wafugaji

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,257
Wananchi wa kata ya bulamata, pamoja na kata za jirani zilizopo Mishamo mkoani Katavi kutoka wilaya ya Tanganyika wameomba serikali kuingilia kati migogoro iliyopo kati ya wakulima na jamii ya wafugaji.k

Wananchi wa vijiji hivyo wamesema kuwa jamii ya wafugaji wamekuwa na idadi kubwa ya Mifugo inayopelekea uharibifu mkubwa wa mazingira ikiwa ni pamoja na vyanzo vya maji,na hivyo kuelekea Kukosekana kwa maji.

Pia Mifugo hiyo imekuwa ikichafua maji ya mito ambayo wakazi hao hutumia kwa matumizi ya kunywa na kupikia.

Baadhi ya viongozi wa vijiji hivyo wamedai ya kuwa wafugaji hao hawana sehemu maalumu ya kufuga mifugo yao bali wamekuwa ni watu wa kuhama hama leo hapa kesho pale na hivyo kufanya uharibufu mkubwa wa mazao pamoja na mazingira.

Kumekuwa na migogoro ya Kila mara hali ambayo inahatarisha usalama kati ya wafugaji hao na wakulima siku za usoni serikali isipoingilia kati.
 
Hivi kuna upungufu wa ardhi Mishamo pamoja na mapori yalivyo mengi kiasi kile!?
 
Back
Top Bottom