Wakazi wa mbagala kizuiani wasaidiwe na janga la wadudu kunguni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakazi wa mbagala kizuiani wasaidiwe na janga la wadudu kunguni

Discussion in 'JF Doctor' started by kazikubwa, Aug 13, 2012.

 1. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wakazi wa Mbagala Kizuiani wametoa kilio chao kwa viongozi wa Serikali ili waweze kuwasaidia kuwaondolea janga la wadudu waitwao Kunguni. Kilio hicho wamekitoa kupitia Times Radio. Katika mahojiano yao na mwandishi walimueleza janga hilo wanalo kwa takriban mwaka mmoja na zaidi.


  Hapo awali walikuwa wakiona aibu kueleza wazi tatizo hili hadharani. Kwa sasa maji yapo shingoni na wanaiomba Serikali iwasaidie. Kutokana na maelezo yao wananchi hao wanaamini kuwa Kunguni hao huenda wapo hapo kwa njia ya giza (ushirikina) wakitoa sababu mbalimbali:-
  1. Wanadai wadudu hao ukithubutu kuwatia dawa ndio una wa double bora uwaache wakuchakaze wakiwa wachache.
  Hawasikii dawa hata kidogo.
  2. Wanadai wadudu hao ukiwaanika juani au kuwaunguza na maji ya moto hapo ndio unawaongezea ukali mara dufu.

  Wanabchi hao wamedai kuwa kwa sasa wanalala nje ya nyumba zao kuwakwepa kunguni. Wanasema bora kuumwa na mbu lakini siyo kunguni maana washambulia mwanzo mwisho.

  Je, Serikali itakuwa sikivu au itadai kuwa hilo halitekelezeki kama madai ya madaktari na walimu?

  Tunaomba wanchi wenye imani na mapenzi kwa watanzania tuwasaidie wananchi hawa ili nao waishi kwa amani ndani ya jiji la Dar es salaam. Walitoa kilio chao kupitia kipindi cha DIDA wa Mchops na leo wameamua kurudia kupitia redio hiyo hiyo kupitia kipindi cha Bwana Mkisi cha saa 10 jioni hadi saa 1 usiku wakihisi labda redio ya Mbunge wao iliishiwa betri au mgao wa umeme uliiathiri.

  Tuwasaidie watu hawa la sivyo tutapata kazi ya ziada ya kuwaongezea damu.
   
 2. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,571
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Mbagala bila kunguni inawezekana. Serikali ni sikivu kwa ushirikiano wenu na wawakilishi wenu!
   
 3. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 921
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  We! Kunguni ni nouma acha mchezo. Wanashambulia kama siafu,ukiwasha taa tu wanasepa,ukizima wanazingira na kazi inaanza upyaaa. Waliwahi kusumbua lakini tuliwadhibiti kwa kupiga maji ya moto kila wakati na vile vitu vinavyowatunza tulianika juani kila wakati. Unajua tatizo ni kuwa we ni mgonjwa halaf unaona aibu. Fanya hivi kila baada ya siku4 au wikend utawamaliza wala usione aibu kwan ipo siku watakuaibisha mbele ya wageni. Kwani wanatabia kukatiza kwenye pamba mbele za watu. Poleni ndugu zanguni.
   
 4. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wakazi wa mbagala wameiomba Serikali kuwaokoa na tatizo la wadudu aina ya kunguni ambao kwa sasa wanawafanya walale nje ya nyumba zao. Tusisubiri Serikali, shime wananchi tuwasaidie wenzetu mapema kabla ya kuombwa kuwaongezea damu
   
 5. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aiseee baba yangu jei kei si ajarudi?? ngoja nimwambie aonganishe moja kwa moja mpaka kwa obama akaombe msaada wa kinga kama alivyofanya kwa uomba net

  ngoja nipate mbege
   
 6. Dr F. Ndugulile

  Dr F. Ndugulile MP Kigamboni

  #6
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 242
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Nimewasiliana na Bwana Afya wa Manispaa aweze kuwatembelea na kuwapatia ushauri wa kitaalamu.
   
 7. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,377
  Likes Received: 604
  Trophy Points: 280
  Kwani hajui hadi leo? Nadhani ingekuwa bora ukaenda naye mguu na bega.
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 29,259
  Likes Received: 4,244
  Trophy Points: 280
  Khaaaaaa mpaka kuua kunguni wanaisubiri serikali?
   
 9. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,377
  Likes Received: 604
  Trophy Points: 280
  Si ndio inajua waganga.
   
 10. Master jay

  Master jay Senior Member

  #10
  Aug 13, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 189
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  subiri iwekwe kwenye ilani ya uchaguzi ya nyinyiemu
   
 11. SR senior

  SR senior JF-Expert Member

  #11
  Aug 13, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  wachafu wakubwa hao.
   
 12. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,085
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  Hili tatizo alishaambiwa hadi waziri wa afya kwa simu ya mkononi through Wapo Radio. Wakati huo tatizo lilikuwa Mtongani, mashine ya maji na Yombo akaahidi kulifanyia kazi. Sasa sijui bajeti imekuwa finyu tusubiri mwakani?
   
 13. kibonga

  kibonga Senior Member

  #13
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 138
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  poleni sana SIO MBAGALA TU. shule ya GREEN ACRES YA MSINGI ILIOKO SALASALA kunguni ndio waonawamaliza watoto wanao lala mbweni FUATILIENI NAKO HUKO:flypig:
   
 14. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 24,908
  Likes Received: 1,932
  Trophy Points: 280
  Diamond wa mbagala wasaidie watu wako kunguni ni nomaaaaaa!!
   
 15. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #15
  Aug 14, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 19,469
  Likes Received: 294
  Trophy Points: 180
  Nape atasema kunguni hawa wameletwa na chadema na wafadhili wao...poleni waathirika wa kunguni
   
 16. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #16
  Aug 14, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,513
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ...hapo ni mpaka "kwa hisani ya watu wa marekani"
  haka kanchi bana...tunazungumzia kunguni mpaka leo...karne hii!
   
 17. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #17
  Aug 16, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,615
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu wa mbagala fanyeni fumigation bwana bila hivyo hamtawamaliza watawatia aibu tu. Imagine una mgeni unamtandikia shuka safi analala halafu usikua anaamshwa na kunguni, ee bwana asubuhi tu anaaga kuondoka yaani kunguni sio mchezo.
   
 18. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #18
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,680
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Na hao kunguni wameletwa na chadema by nape
   
Loading...