Wakazi wa Magamba Songwe wachoma mazao yao ya ufuta mashambani mwao kupinga agizo la Mkuu wa Wilaya ya kutaka wauze kwa mfumo wa stakabadhi ghalani

Hao wakazi ni wapumbavu sana,mfumo huo ndio wenye faida kwao kwani hakuna mtu wa kati,wanauza kwa bei ya soko moja kwa moja na pesa zao hulipwa ndani ya masaa 48 tokea kufanyika kwa mnada,narudia tena ni wapumbavu sana wataendelea kulanguliwa hadi mwisho wa dunia kmmzao
Unaweza kukuta wewe ndiye mpumbavu wa kutupwa, yaani wakulima wilaya yoooteee wasione hiyo faida ya huo mfumo? Acha upimbi jombaa..
 
Nafikiri hujui uliongealo,udalali unafanywa na wanaoupinga ili waendelee kudalalia jasho la mkulima,mfumo huu unasimamiwa na wakala wa Serikali aliye chini ya Wizara ya Fedha anayeitwa TMX,sasa Serikali itaundaje chombo cha kumlalia mkulima?
Tatizo hawalipi on time, sasa kwa nini unikope mazao yangu??
 
Inawezekana hakukuwa na utashi wa serikali ila kuna mtu mmoja aliyeharibu taswira kwa maamuzi yake mabaya,ila dhamira ya mfumo ni njema mno
Kama dhamira ni nzuri leteni pembejeo muwape wakulima halafu wakiuza ndiyo muwakate, siyo mnasubiri mtu anateseka halafu mnakuja mbio ili mpate kodi.
 
Hili swala la stakabadhi ghalani nlishawahi kulifikisha hadi kwa Mh Bashe Naibu waziri wa kilimo
Tatizo la serikali yetu WANAINGIZA SIASA KATIKA BIASHARA YA MAZAO..
 
Hamjajifunza kutokana na zao la korosho nyinyi CCM ni kizazi cha nyoka.
Muhimu ni elimu ya kutosha tu
Warehouse receipts ndio njia Bora kuliko zote inayomuhakikishia mkulima kuwa na fedha mpaka off season
Tatizo ni madalali na wafanya biashara wanawaharibu akili wakulima kwa kuwaletea pesa kiduchu mazao yakiwa bado hata kupevuka
 
Mimi Wilayani kwangu nautumia huo mfumo hasa kuuza ufuta,hakuna malalamiko kutoka kwa wakulima,sana sana wamefurahi kwa kupata bei nzuri ambayo hawajawahi kuipata,nikufumbue kitu kuwa wafanyabiashara walanguzi ndio wanaoupinga huu mfumo ili waendelee kumpiga mkulima,tena wanasaidiana na viongozi wakubwa serikalini kuuponga mfumo huu kwa wao pia ni wafaidika juu ya unyonyaji kwa wakulima
Bei nzuri ni bei gani huo ufuta mnauza!
 
Bora wote mkose kuliko kutapeliwa na serikali🤓 wanajua kilichowakuta kusini zama za korosho
Ni ukosefu tu wa elimu stahiki
Huyo Dc nae badala ya kutoa elimu kwanza,anatoa amri.Nahisi amechanganyikiwa na mkwara wa mama
 
Ww acha kudanganya watu ,wakulima wamejaa maumivu ya kahawa mwaka jana kule Songwe wameteseka mpaka kahawa wakalipwa bei ndogo na kuchelewa juu.Hujui tu unaongea shida wanazo pata ww huzijui.
Anajiropokea tu huyo ama labda yeye ni miongoni mwa wastaafu wa CCM. Serikali inajali ingekuwa inalipa wakulima cash yao wanapopeleka mzigo ili wao wakiuza wanajilipa juu kwa juu!

Ila biashara ya kupeana stakabadhi halafu hela kulipwa inaambatana na blaah blaah nyingi hio inaifanya serikali na wakala wake kuonekana madalali tu! Saa zingine hata msilipwe kabisa ni story tu! Hao wananchi wamefanya jambo zuri tu kwa kuponya nafsi zao na machungu ya dhuluma. Inaonesha walishaiamini serikali na huo mfumo huko nyuma ila iliishia kuwaangusha vibaya mno.

“You can fool some people sometimes, but you can never fool all the people all the times”~ Bob Marley
 
Back
Top Bottom