Wakazi wa Mafia sasa kupata usafiri salama na wa uhakika ( Dar – Mafia), Serikali yaanza mchakato wa ujezi wa Boti jipya.

Cheko Lamhenga

Senior Member
Aug 1, 2018
165
93
Changamoto ya usafiri katika kisiwa cha mafia sasa imefika ukingoni, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza kutatua changamoto ya usafiri toka Dar kwenda kisiwa cha Mafia kwa kuanza ujenzi wa boti la kisasa ambalo ujenzi wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2020.

Ujenzi wa boti hilo utagharimu Tsh Bilioni 7, Katika kipindi cha ujenzi wa boti mpya Serikali imewaandalia wakazi wa Mafia usafiri wa boti la Azam (Sea bus I) ambao unatarajiwa kuanza mapema mwezi octoba 2018. Wajibu wetu kuombea utekelezaji wa ujenzi huo kwa mmanufaa ya usafiri salama na wa uhakika kwa watanzania wenzetu wa Mafia.

Habari zaidi, soma=> Wananchi wa Mafia tunahitaji usafiri wa uhakika na bei nafuu - JamiiForums

Msikilize Mbunge wa Mafia MBARAKA DAU akielezea
 
Kama serikali inavyofanya kwenye kuboresha huduma za mawasiliano nchini kwa kuwapa pesa Tigo, Voda, Halotel, TTCL, Airtel nakadhalika, ili wajenge minara,
Wangeongea tu na Bhakresa wampe pesa kwa mtindo wa hire purchase ili apeleke meli moja ndogo mpya kule
Mfumo wa hire purchase ni mzuri kwa kuwa hulazimiki kulipa pesa zote kwa wakati mmoja na jambo hili huarakisha upatikanaji wa bidhaa/ huduma.
PPP katika maeneo kama haya hasa kwa kuhusisha watu wenye expertise ya muda mrefu ni jambo jema zaidi...
 
Changamoto ya usafiri katika kisiwa cha mafia sasa imefika ukingoni, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza kutatua changamoto ya usafiri toka Dar kwenda kisiwa cha Mafia kwa kuanza ujenzi wa boti la kisasa ambalo ujenzi wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2020. Ujenzi wa boti hilo utagharimu Tsh Bilioni 7, Katika kipindi cha ujenzi wa boti mpya Serikali imewaandalia wakazi wa Mafia usafiri wa boti la Azam (Sea bus I) ambao unatarajiwa kuanza mapema mwezi octoba 2018. Wajibu wetu kuombea utekelezaji wa ujenzi huo kwa mmanufaa ya usafiri salama na wa uhakika kwa watanzania wenzetu wa Mafia.

Msikilize Mbunge wa Mafia MBARAKA DAU akielezea

acha upuuzi
 
Serikali imewaandalia usafiri wa Azam (azam sea bus)? Au amepanga kuanza safari ya Dar-Mafia? Don't fool us men.
 
Serikali inaandaa usafiri wa kampuni binafsi! Je mwenye kampuni akiona kuwa biashara sio nzuri itakuwaje?
Why serikali isiwe na meli yake kwa ajili ya wananchi wa mafia?
 
Serikali inaandaa usafiri wa kampuni binafsi! Je mwenye kampuni akiona kuwa biashara sio nzuri itakuwaje?
Why serikali isiwe na meli yake kwa ajili ya wananchi wa mafia?
Me naona ikiwa na meli ya mtu binafsi itakua bora kuliko wa serakali
 
Me naona ikiwa na meli ya mtu binafsi itakua bora kuliko wa serakali
Napajua mafia nimeshiriki ujenzi wa gati la mafia, umbali wa mafia dar ni karibu mara mbili ya dar na zenji! Hapa naongelea nauli itakuwa bei gani na nani anaweza kuimudu
 
Hawa wananchi wa Mafia wamezoea majahazi na njia wanayoipenda sana Mafia hadi Nyamisati Rufiji.
Mwaka 2013 kuna mzungu aliweka boat ya kisasa kwenye hiyo njia sijui iliishia wapi.
 
Changamoto ya usafiri katika kisiwa cha mafia sasa imefika ukingoni, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza kutatua changamoto ya usafiri toka Dar kwenda kisiwa cha Mafia kwa kuanza ujenzi wa boti la kisasa ambalo ujenzi wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2020.

Ujenzi wa boti hilo utagharimu Tsh Bilioni 7, Katika kipindi cha ujenzi wa boti mpya Serikali imewaandalia wakazi wa Mafia usafiri wa boti la Azam (Sea bus I) ambao unatarajiwa kuanza mapema mwezi octoba 2018. Wajibu wetu kuombea utekelezaji wa ujenzi huo kwa mmanufaa ya usafiri salama na wa uhakika kwa watanzania wenzetu wa Mafia.

Habari zaidi, soma=> Wananchi wa Mafia tunahitaji usafiri wa uhakika na bei nafuu - JamiiForums

Msikilize Mbunge wa Mafia MBARAKA DAU akielezea
Sisi wakaazi wa Nyamisati tumeshazoea kwenda Mafia kwa kutumia hii meli
FB_IMG_1537966598786.jpeg
 
Masaa 2½ - 3 kufika Mafia kutoka Nyamisati ina raha yake na kero zake pia
 
Back
Top Bottom