Wakazi wa Madale wapatwa na taharuki baada ya kuvamiwa na Nyati wa Porini

Savimbi Jr

JF-Expert Member
Sep 23, 2011
6,819
9,171
Wakazi wa Madale wa jijini Dar-es-salaam wakumbwa na taharuki na wngine kukimbia makazi yao baada ya kuvamiwa na nyati ambaye hajulikani alipotoka.

Nyati huyo amejeruhi watu na baadhi ya mifugo...Kikosi kazi cha Ant-robbery cha mabwepande wamefika haraka na kumuua nyati huyo.

Kiongozi wa kikosi amesema nyati huyo ni jike hivyo kuna uwezekano wa kuwa na nyati dume maeneo hayo ya madale.

NYATI.jpg
 
Da! Bado kuna wanyama pori DSM? Au ndio ndagu za uchaguzi
Inatisha inawezekana mambo ya numba na ngaye za uchaguzi,huyo nyati sijui ametoka pori gani la akiba bila kuonekana,pori la karibu ni saadani ,sasa kutoka saadani hadi madale ina maana hapa kati kati hakuna aliyemuona? Na mara nyingi nyati hutembea kwa makundi possible bado kuna nyati wengine ukanda wa Madale.
 
Miaka ya themanini nyuma ya kiwanda cha saruji Wazo hill kulipokuwa na basketball uwanja wa mpira kulikuwa na pori kubwa hadi kwa Mzee kiwiya. Tulikuwa wadogo Nakumbuka tukiona paa sungura ngedere. Nilisikia kulikuwa na Chui pia. Ila binadamu waaribifu wamefyeka mapori yoyote.
 
Duuuuh miaka ya 80 si hadi simba walikuwepo hapo? Maana mpaka sasa bado hapajachangamka.
 
Wakazi wa mtaa wa Madale jijini Dar es salaam wakumbwa na taharuki na wengine kukimbia makazi yao baada ya kuvamiwa na nyati ambaye hakujulikana alipotoka na kujeruhi watu na baadhi ya mifugo kabla ya kikosi cha polisi Ant-Robbery cha Mabwepande kufika na kumdhibiti kwa risasi.

Nyati huyo inadaiwa katoea mto Nyakasangwe na kuingia mitaa Madale majira ya asubuhi ambapo Kiongozi wa kikosi cha Ant-robbery kilichotoka Mabwepande Constebo Sixberto Salakana amesema wamekabiliana na nyati huyo bila kusababisha madhara yoyote kwa wakazi na kufanikiwa kumlenga risasi ya kichwa mnyama huyo.
 
Wanakimbia kitoweo!!!!
 
Inakuwaje Anti- robbery unit itumike? Mali asili walikuwa wapi? Huyo mnyama si jambazi na hakupaswa kupigwa risasi. Ni utaalamu wa Mali asili ungetumika na kumrudisha anakostahili. Hili ni doa jingine kubwa. Tunasomesha wataalamu wasiotumika wanapohitajika.
 
Back
Top Bottom