Wakazi wa mabondeni wagoma kuondoka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakazi wa mabondeni wagoma kuondoka

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Nov 21, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  WAKAZI waishio mabondeni wamepuuza agizo la Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Evance Balama la kuwataka wakazi hao waondeke maeneo hayo kwa kuwaepusha na madhara ya mvua zinazotarajiwa kuanza kote nchini zilizotabiriwa kuwa na maafa makubwa Wananchi hao wanaendelea kukaidi maagizo ya viongozi hao na kuendelea kuwepo katika maeneo hayo hatarishi.
  Maeneo ambayo wananchi wametakiwa kuhama kabla ya mvua kunyesha ni yale yalioko katika bonde la Kigogo, Jangwani na maeneo mengine yote ambako ni hatarishi kwa mvua hizo..


  Baadhi ya wakazi hao wamesema hawahami katika maeneo hayo hadi pale serikali itakapowaandalia maeneo husika na kusema serikali inataka wahame bila ya kujiandaa .


  Katika hali ya kushangaza wakazi hao wanaonekana kudharau na kutojua madhara ya mvua tarajio


  “Hatuhami hapa kwani tukiondoka hapa tutaelekea wapi? Isitoshe sisi tumeishi maeneo haya kwa muda mrefu sana mbona madhara hayo hatujayaona? Tuaenda wapi na nani anaweza kupokea mtu mwenye familia ya zaidi watu watano hadi kumi Dar es Salaam hii maisha magumu kama haya?”

  "Hao wanaotaka tuhama watutafutie mahali pa kwenda kuishi"

  Agizo la mkuu limekuja baada ya Mamalaka ya hali ya hewa kutangaza kuwa mvua zinazotarajiwa kunyesha kote nchini zitakuwa kubwa na wananxchid kupewa tahadhari na mvua hizo.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3579334&&Cat=1
   
Loading...