Wakazi wa Kipawa:Serikali kutumia Sheria ya Ardhi 1967 na siyo ya 1999 ina nia gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakazi wa Kipawa:Serikali kutumia Sheria ya Ardhi 1967 na siyo ya 1999 ina nia gani?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Magobe T, Nov 1, 2009.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Ndugu wadau, nilikuwa nafuatilia 'issue' ya wakazi wa Kipawa kwenye luninga wiki iliyopita nikasikia kuwa Serikali inatumia Sheria ya Ardhi ya mwaka 1967 na siyo ya 1999. Kwanza, msemaji mmoja wa Wizara ya Ardhi alisema, "Wananchi wakilipwa kwa sheria ya 1967 watanufaika zaidi kuliko ya 1999."

  Niliona kama kunufaika kwa wananchi ndiko kulikoifanya Serikali itumie sheria ambayo haitumiki tena, basi Serikali yetu inawajali sana watu wake. Lakini kadiri nilivyoendelea kusikiliza niligundua kuwa siyo kweli. In fact, kwa kutumia Sheria ya Ardhi ya 1999, wakazi hao wangenufaika zaidi na hivyo msemaji huyo wa Ardhi alikuwa anasema uongo.

  Hoja yangu hapa ni kwamba kama hii itakuwa 'trend' ya kuchagua ni sheria gani itumike (kama hata hizo ambazo hazitumiki zinatumika tena), je kutakuwa na sababu gani ya kuendelea kutunga sheria mpya kama za zamani zinaweza kutumika tena?
   
 2. W

  Wasegesege Senior Member

  #2
  Nov 1, 2009
  Joined: Oct 22, 2009
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hoja yangu hapa ni kwamba kama hii itakuwa 'trend' ya kuchagua ni sheria gani itumike (kama hata hizo ambazo hazitumiki zinatumika tena), je kutakuwa na sababu gani ya kuendelea kutunga sheria mpya kama za zamani zinaweza kutumika tena?

  Katika majadala kama huu niliwahi kutoa somo kwamba, Wananchi wa Kipawa hawawezi kulipwa na Sheria ya Ardhi ya Mwaka 1999, kwa sababu wakati wanafanyiwa uthamini ilitumika sheria ya mwaka 1967.

  Kwa mujibu wa Sheria Mtu au watu hawawezi kuathirika na Sheria Mpya iwapo walifanya tendo hilo wakati Sheria hiyo haijapitishwa au kuanza kutumika isipokuwa mpaka pale Sheria hiyo mpya itamke kwamba, wale wote waliotenda kosa au waliokuwa na kitu fulani ambacho kilikuwa kwa kujibu wa Sheria inayofutwa sasa wanashughulikiwa na Sheria mpya. Kama Sheria Mpya haina kifungu kama hicho, mtaendelea kutumikwa na Sheria ya zamani kwa kuwa ndipo mlipoanzia.

  Ngoja nikupe mfano upate kuelewa.

  Mwaka 2002 Serikali ilitunga Sheria mpya ya Ubakaji na Sheria hiyo ilianza kutumika tarehe 01.07.2002 kwamba anayepatikana na hatia ya kosa la kubaka ni jela miaka 30 au zaidi au faini Tshs. 10,000,000/ au vyote kwa pamoja.

  Angalia Mr. P. alibaka tarehe 22.06.2002 na akapelekwa Mahakamani tarehe 23.06.2002 akafunguliwa kesi ya Ubakaji kwa mujibu wa Sheria iliyokuwa inatumika wa wakati huo kwa sababu hii Sheria Mpya ilianza kutumika 01.07.2002. Hukumu ya Huyu Mr. P ikisoma leo tarehe 01.11.2009 atahukumiwa kwa Sheria ya zamani kabla ya mabadiliko yaliyoanza kutumika 01.07.2002 ama Sheria hiyo mpya itamke hivyo.

  Kumuhukumu kwa Sheria mpya itakuwa siyo kumtendea haki kama Sheria hiyo haijatamka kuhamishia makosa kwenye Sheria mpya. Vivyo hivyo kwa Wakazi wa Kipawa, Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 haikutamka kwamba, wale wote waliofanyiwa tathmini kwa mujibu wa Sheria ya mwaka 1967 basi watalipwa kwa mujibu wa Sheria ya mwaka 1999. Hivyo kuwalipa kwa mujibu wa Sheria ya mwaka 1999 ambayo haikutamka kuhamishia masuala ya ardhi yaliyoamuliwa kwa mujibu wa Sheria ya mwaka 1967 ni kutokuwatendea Haki wananchi wa kipawa.
   
 3. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #3
  Nov 1, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Hapa nimeelewa. Lakini kama Serikali yenyewe ilichelewesha malipo na ni wazi kwamba gharama zimeongezeka toka wafanyiwe hiyo tathmini na kukaa bila kulipwa kwa takriban miaka 10. Kwa nini Serikali, isifanye tathmini mpya ili kuendana na sheria ya sasa na hivyo pia kuendana na gharama ambazo zimeongezeka. Pili, nisheria gani imetumika kuwafanya hao wananchi wahame ndani ya siku 48 baada ya kulipwa na wakati hata eneo wanakopaswa kwenda halijalipwa?

  Kwa maoni yangu, is it still worthwhile to hang on such a law, which is detrimental to evictees?
   
 4. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2009
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,424
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Magobe, ni bahati mbaya matamshi ya ofisa moja serikalini kuchukuliwa ni serikali imetamka! Nakumbuka mara baada ya kusikia kauli za wananchi kulipwa kwa sheria ya 47 ya 1967 eti badala ya 4 ya 1999, nilishtuka na nilipiga simu kwa watu wa Ardhi kuuliza kulikoni.

  Ni muhimu kujua sheria ya 47 ya 1967 ni hai kabisa na inatumika katika kutwaa ardhi ya mwananchi kwa makusudio mbalimbali. Upungufu katika sheria ya 1967 ni kifungu kimoja ambacho kilinyima mwananchi haki ya kufidiwa ardhi tupu. Hii iliwanyima haki sana watu wa mijini ambao wangeweza kuwa na eneo ambalo ni tupu wakisubiri wapate uwezo wajenge. Mashambani ikiridhika hakuna shughuli yeyote iliyofanyika kwa zaidi ya kipindi cha miezi 12 basi Serikali ingeweza kutwaa ardhi bila fidia. Kifungu hiki kimerekebishwa na msisimko mkubwa wa sheria ya 4 ya 1999 ni kuwa Ardhi TUpu ina thamani.

  Kule Kipawa, wakati wa zoezi la uthamini 1997, ardhi tupu haikuthaminiwa. Lakini fidia zilicheleweshwa mno, na zimefanywa miaka 10 na zaidi baadae. Yanayojiri akilini mwangu kwa matamshi ya serikali ni kuwa ardhi tupu haitafidiwa. Hiyo kamwe isingekubalika na wananchi wana kila sababu ya kupambana mahakamani. Ila katika dodosi zangu na watu wa Ardhi, kilichokusudiwa ni kuwa misingi ya kuttotoa fidia ingekuwa taarifa (field surveys za zamani). Na kweli Ofisi ya Mthamini Mkuu wa serkali walipitia mahesabu yale ya zamani na kuya-index pamoja na kuruhusu 'penalties' za 6% kwa ajili ya ucheleweshaji. Sasa katika maelezo wanasema hii ni nzuri zaidi, kwani 6% imetajwa katika sheria ya 1967 na sio katika ya 1999.

  Sheria ya 1999 inafafanua jinsi ya kutotoa fidia ikiwa ni pamoja na malipo ya ziada kwa kuchelewesha. Chini ya Kifungu 179 katika kanuni, walitengeneza Kanuni zilizoanza kutumika Mei 2001 ambazo zinaelezea haya. Ucheleweshaji na usumbufu unakadiriwa kama asilimia ya fidia iliyokadiriwa na kiwango ni riba ya fixed deposits kwa wakati husika. Sasa kuanzia 2001, imekuwa kama desturi kutumia kiwango cha 4% kwa yote haya,(yaani mwambie mtu wa serikali kiwango wakati huu ni hiki, atakingangania hadi mwisho wa dunia, hawabadiliki!). Hivyo kwa kudhani bado riba iko kwenye wastani wa 4 waliona kwa kutumia maelezo na kiwango cha 6% walikuwa wanafanya vyema. Ukweli ni kuwa viwango vya riba sasa hivi viko juu ya 6%.

  Watendaji wa serikali walijikanyaga katika maelezo. Isingekuwa busara kutuma watu upya wakapime zile nyuma maana nyingi zingeonekana kuwa zee zaidi, na pengine hazikuwepo tena(zimevunjika). Uwezekano wa kukuta nyumba nzuri zaidi zilizojengwa na wale ambao hawakutii amri ya kusitisha ujenzi ulikuwepo pia, hawa wangelipwa kwa kukaidi na wale watiifu wangepunjwa kwa kutii. Nionavyo kwa kutumia records za zamani serikali walifanya vyema lakini hawakutolea maelezo ya kufaa.
   
 5. W

  Wasegesege Senior Member

  #5
  Nov 1, 2009
  Joined: Oct 22, 2009
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli ukisoma Sheria ya Ardhi ya mwaka 1967 sehemu ya fidia ya nyumba, mali zisizohamishika na ardhi inasema iwapo mtu atafanyiwa tathmini na akazuwiliwa kuendeleza eneo lake lakini wakati wa mchakato wa malipo ikachukua zaidi ya miaka mitatu basi mtu huyo atalipwa fidia kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa mwaka ule pamoja na nyongeza ya asilimia 20 ya fidia (fidia ikiwa ni Tshs. 100 + 20% ya Tshs 100) ndiyo yanakuwa malipo yako. Na ndicho kinachofanyika.

  Kula Kigoma Wakazi wa Tarafa ya Mwandiga walifanyiwa tathmini mwaka 1998 na hata mwaka jana walikuwa hawajalipwa na walizuwiliwa kuendeleza maeneo yao ili kupisha ujenzi wa barabara ya Kigoma - Mwandiga - Kidahwe hadi Manjovu. Lakini mwaka huu wamelipwa fedha zilipopatikana jumla ya fidia ya malipo yao kama ilivyokuwa kwenye tathmini ya mwaka 1998 jumlisha na 20% ya kucheleweshwa kulipwa.

  Ninachowahurumia wakazi wenzangu wa Kipawa unajua siku hizi kuna Wanasheria feki ambao maisha yao ya Mjini wanategemea kujifanya kama wanasadia watu. Nataka nikuambie ukiwauliza wakazi wa Kipawa utasikia kuna kijana mmoja amejitolea kutusaidia. Lakini wanachangishwa fedha kwa ajili ya nauli na kununulia makaratasi na kufungulia kesi zote wanamkabidhi huyo Mwanasheria Mganga Njaa. Watu tuwe makini.sana
   
 6. W

  Wasegesege Senior Member

  #6
  Nov 1, 2009
  Joined: Oct 22, 2009
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni muhimu kujua sheria ya 47 ya 1967 ni hai kabisa na inatumika katika kutwaa ardhi ya mwananchi kwa makusudio mbalimbali. Upungufu katika sheria ya 1967 ni kifungu kimoja ambacho kilinyima mwananchi haki ya kufidiwa ardhi tupu

  Sasa Magobe watu wa Kipawa hawaambiwa kusoma maelezo kama hayo niyonukuu kutoka kwa Njirembela- Wanasheria wao BUTU na WAGANGA NJAA wanawakamua hata kile kidogo wanachookota kwa kuchoma maandazi na Vitumbua.

  Huu ni WIZI MKUBWA kuna umuhimu wa JFM kuona namna ya kuweka jukwaa la wazi kwa wananchi ambao hawapati nafasi ya kuingia kwenye Mtandao. Ukawepo mjadala kwenye Viwanja vya K/Chekundu DSM, Pasua Moshi, Kilimbero Arusha, Nyerere Sqr - Dodoma, K/Ndege S/Msingi Morogoro, Urusi - Kigoma, Majix2 Songea, Songwe Mbeya, Samora Iringa, Nyamagana Mwanza, n.k ili wananchi waelimishwe haki zao
   
Loading...