Wakazi wa Kipawa kulipwa fidia kwa sheria ya zamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakazi wa Kipawa kulipwa fidia kwa sheria ya zamani

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Invisible, Sep 14, 2009.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Sep 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Na Geofrey Nyang'oro

  HATIMAYE kitendawili cha sheria gani itatumika katika kuwalipa fidia wakazi wa Kipawa, jijini Dar es Salaam, kimeteguliwa baada ya serikali kuelezea msimamo wake kuwa itatumia sheria ya ardhi ya mwaka 1967.

  Msimamo huo wa serikali, ulitolewa juzi na Afisa Ardhi Mkuu Mwandamizi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Edgar Japhet, alipokuwa akizungumza na wawakilishi wa wananchi hao, kuhusu sheria itakayotumika katika kuwalipa fidia.

  Japhet alisema malipo hayo yanazingatia sheria iliyotumika wakati wa uthamani.

  "Serikali ilifanya tathimini mbili moja ikitumia sheria ya zamani na nyingine ikitumia sheria mpya lakini ikamua kutumia sheria ya zamani katika kuwalipa fidia wananchi wa Kipawa," alisema.

  Hata hivyo wananchi hao wamekuwa wakiilalamikia sheria hiyo kwa madai kuwa inalenga katika kuwadhulumu.

  Katika kikao hicho, wananchi wa Kipawa walimlalamikia Japhet kuwa ndiye chanzo cha kutaka kudhulumiwa.

  Hata hivyo Afisa huyo alisistiza kuwa huo ndio msimamo wa serikali na kwamba unatokana na sheria iliyotumika katika tathimini ya eneo hilo.

  "Siyo mimi niliyeamua ninyi kulipwa kwa sheria hiyo, maamuzi yaliyotolewa yanawataka mlipwe kwa sheri ya mwaka 1967 sheria iliyokuwa ikitumika wakati wa uthamani"alisema Japhet.

  Alisema uamuzi huo, umezingatia ushauri kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

  Alisema kutokana na msimamo huo, tayari serikali imetenga Sh 30 bilioni kwa ajili ya malipo ya fidia kwa wananchi wa eneo hilo.

  Kwa mujibu wa afisa huyo, fedha hizo ziko tayari wakati wowote wananchi hao wataanza kulipwa haki zao.

  Japhet alisema fedha hizo zitatumika kuwalipa fidia wananchi wa maeneo ya Kipawa, Kigilagila na Kipunguni.

  Kwa mujibu wa Afisa huyo, watu wa Kipawa, wametengewa Sh18 bilioni katika fedha hizo, taarifa ambazo zilionekana kuwachanganya watu.

  Mwenyekiti wa wakazi hao Magnusi Mulisa,alisema kimsingi wananchi wa eneo hilo hawakubaliani na uamuzi huo wa serikali.

  "Sisi tupo hapa kuwawasilisha wenzetu hata hivyo hatukubaliani na majibu haya tutakwenda kuonana na wenzetu ili kujua la kufanya,"alisema.


  Chanzo: Gazeti la Mwanchi la Sept 13, 2009
   
 2. W

  Wasegesege Senior Member

  #2
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 22, 2009
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tafadhali jamani msichanganye MADAWA au TIBA ya Mtu wa Kichwa kupasuliwa Mguu na Mtu wa Mguu kupasuliwa Kichwa.

  Taratibu za Kisheria zinasema, Mtu yeyote anapata stahili yake ya Kisheria kwa kutumia Sheria mpya iliyopitishwa iwapo tu Sheria hiyo wakati inapitishwa na Mtu huyo alifanya au alifanyiwa jambo kwa Sheria ya zamani basi sheria hiyo Mpya itamke kwamba, wale wote waliofanyiwa jambo kwa kuzingatia au wakati wa Sheria inayofutwa ilikuwa inatumika basi watashughulikiwa jambo lao kwa mujibu wa Sheria Mpya. Lakini kama Sheria Mpya haitamki hivyo, Mtu au watu hao wataendelea kulipwa stahili zao kwa kuzingatia Sheria ya zamani ambayo ndiyo waliyoshughulikiwa nayo.

  Nitatoa Mfano. Hadi tarehe 30.06.2002 Sheria ya Makosa ya Kubaka ilikuwa inasema mbakaji atahukumiwa kulipa faini ya Tshs.... au atafungwa Miaka mitano au vyote viliwili. Lakini ilipofika tarehe 01.07.2002 Sheria Mpya ya Makosa ya Ubakaji ikasema watu wote watakaokamatwa kwa kosa hili watahukumiwa kifungo cha Miaka 30 au zaidi. Sasa Mr. X alibaka tarehe 21.06.2002 wakati wa Sheria iliyofutwa lakini hukumu yake imetolewa mwezi 12, 2008. Mr. X huyu hata hukumiwa kwa mujibu wa Sheria iliyopitishwa mwaka 2002 mwezi Julai kwa sababu kosa lake alilifanya wakati kabla Sheria hiyo haijaanza kutumika eti.

  Lakini katika suala la Madai ukitazama Sheria ya Fidia ya malipo inasema mtu akitakiwa kuhama eneo lake anapaswa kulipwa na kama hakulipwa kwa muda wa miaka kadhaa kuna fidia inayotakiwa alipwe pamoja na gharama za awali. Na hilo ndilo linalofanyika.

  Unajua hivi sasa kuna Watu wanaishi kwa kutumia mbinu mbalix2 na hasa za kujifanya wanasheria UCHWALA.
   
 3. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,356
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  Hapo nakubaliana na wewe! Nshaona kitu kama hiki!
   
 4. F

  Franki Member

  #4
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmemsikia Captain John Chiligati? Amewaonya wakazi wa Kipawa kwamba, wasitumie fedha zao kufungulia kesi, bali waende wakajenge. Amewaeleza pia kwamba, watapoteza pesa kuwachangishia mawakili feki...wengine ndo kula yao hapa mjini.
   
 5. W

  Wasegesege Senior Member

  #5
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 22, 2009
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fank

  Mhe. Chiligati yupo sahihi kabisa kuwaonya hao watu wa Kipawa kwani hakuna watakachoambulia soma uchambuzi hapo juu. Ni vema wakazingatia ushairi huo kwani ama sivyo "VIJISENTI" walivyopewa vitaishia kwa MAWAKIRI wetu wa siku hizi kwanza hawana ushauri kwa Mteja hata kama wanaona kesi hashindi wao ni "AFTER MONEY". Nami nawashauri Baba zangu na Mama zangu, Shangazi na Wajomba zangu wa Kipawa waachane na madai eti ya kulipwa kwa kutumia Sheria ya mwaka 2005. wao wadai malipo yao yawe halali na yaendane na fidia ya kukaa muda mrefu bila kulipwa na ilihali walizuwiliwa kuendeleza maeneo yao. Ni kweli kuna WANASHERIA FEKI wengi ambao kula yao wanasubili umegombana na Mkeo au Mumeo wanakushauri mwende Mahakamani watakutetea lakini uwape nauli na hela ya kununua karatasi. Ukiwapa ndiyo wanavyoishi Mjini hao ni wa KUWAOGOPA kama UKOMA.
   
Loading...