Wakazi wa Kigamboni wakataa mchakato wa mradi wa mjimpya na kuomba imma kuufuta au kuanza upya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakazi wa Kigamboni wakataa mchakato wa mradi wa mjimpya na kuomba imma kuufuta au kuanza upya

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by mkomatembo, Dec 19, 2011.

 1. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2011
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Ndugu wana jamvi,

  Juzi nilikuwa naangalia star Tv majira ya saa tatu usiku, nikakuta wakuu wa tatu wanaowakilisha wananchi wa Kigamboni wakiongelea kuhusu mradi wa kigamboni na jinsi sheria ZILIVOPINDISHWA!

  walieleza jinsi gani kabla ya mradi wananchi wanavotakiwa washirikishwe lakini cha kushangaza, mheshimiwa chiligti wakati ule akiwa waziri aliwaita watu wachache tena wa kuchaguliwa wakawaita pale CHADIBWA NA KUWAPA POSHO ZA 50,000 na vinywaji na kupiga picha na baadae kwenda kupeleka wizarani kuoensha kuwa wamezungumza na wananchi wa Kigamboni, wakaitisha mkutano mwengine MGULANI, na mkutano mwengine KARIMJEE wakati wana kigamboni wana viwanja vingi vya hadhara ambavyo mikutano aina hiyo ingefanyika.

  Aidha mkuu yule aliendelea kusema kuwa, mradi wa Kigamboni ni sawa sawa NA RADAR, NDEGE YA RAIS NA EPA, kwa kuwa inaoneshwa jinsi gani wakazi walivo hawashirikishwi katika mradi huo, na kwamba wamekuwa kama mifugo ndani ya zizi ambao wanasubiri kuchinjwa, kuuzwa au kugawiwa kwa mtu ambae wao "wanyama" hawamfahamu na kwamba siku yeyote watauzwa, kugawiwa au kuchinjwa pasi na ridhaa yao!

  Kuthibitisha hili, juzi juzi tuliona wakazi wa Gezaulole walivofanyiwa baada ya serikali kuwalipa wakati wale fedha kiduuuchu na baadae kuuza kila "square meter moja" kwa tsh 6,000 halafu kuwauzia tena wakazi wale ardhi hiyo hiyo yao kwa bei ya juu! huu ni uonevu wa hali ya juu!


  Kinachisikitisha ni kwamba, tokea Oct 2007. wakazi wamesimamishwa wasiendelee na maendeleo ya maeneno yao! na mpaka sasa serikali haijatoa muongozo wowote zaidi ya maneno "MUWE NA SUBIRA"

  Kinachosikika kutoka kwa wakazi wa kigamboni, wanasema kuwa "DAMU ITAMWAGIKA" hasa kama watadhulumiwa haki yao! kwa sababu hakuna ambae yupo tayari kuona akidhulumiwa ukizingatia mtu ameshakaa pale miaka lukuki halafu umhamishe kwenda kukaa kwenye hizo ghorofa zao wanazotaka kujenga ili wahamishie watu huko! hili HALITAWEZEKANA ! kumtoa mtu kwenye nyumba yake ya vyumba sita au 12 , ana wapangaji ambao wanamlipa kwa mwenzi halafu umchukuwe kumuweka katika nyumba ya vyumba vtatu tena vya kujibana.

  Fikiri mtu ananyumba yake amejenga kubwa na ana uwanja wa kutosha wa kucheza watoto umtoe aende akakae kwenye nyumba ambayo hakuna hata sehemu ya kutolea pumzi!

  Nadhani serikali iliangalie upya suala hili imma kwa kulianzisha upya na kuwashirikisha wana Kigamboni kwa UWAZI na wawe na ufahamu wa hatua kwa hatua! au wafutilie mbali kwani tunaamini KUNW AMAENEO MAKUBWA SANA hapa nchini ambayo ni mapori ambayo serikali wanaweza kuyatwaa na kuanzisha miji.. NA WASIKAE NA KUSUBIRI WATU WAMESHAENDELEZA NA WAO WAJE KUPORA MALI KWA ULAINI...


  fikra zangu... Kuna mtu mmoja ambe inaonekana halali usiku au hana kazi na badala yake amekaa usiku kucha au asubihi na mchana wake akiwaza JINSI GANI ATAPATA PESA KWA URAHISI kwa "DHULMA" pesa bila kutoka jasho ! mtu huyu aliwaza jambo hili yeye mwenyewe! na kisha kulieleza kwa wenzake ili wafanye utekelezaji w\a kupata 10% KWA NZA UA KUCHORA RAMANI YA MJI WA KIGAMBONI ! alichora amepata fedha nyingi na walompa tenda bila shaka wamekula 10%, na vingine vafutata..

  je Great Thinkers mnafikiria nini kuhusu jambo hili???

  Kwa Uchungu sana , Nawakilisha
   
 2. c

  conman Member

  #2
  Dec 19, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Ya gezaulole, wananchi walilipwa sh. 700/- kwa square metre. Wao serikali wakauza kuanzia sh. 6000/- kwa square metre. Hesabu hizi sizielewi !!!
   
 3. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ukiona hivyo ccm washajiwekea zao maslahi mbele kwakuwakandamiza waliowaweka madarakani
   
Loading...