Wakazi wa Ilala kota watimuliwa kama mbwa; damu yaweza kumwagika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakazi wa Ilala kota watimuliwa kama mbwa; damu yaweza kumwagika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by domokaya, Oct 27, 2011.

 1. domokaya

  domokaya JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2011
  Joined: Apr 22, 2010
  Messages: 3,129
  Likes Received: 1,252
  Trophy Points: 280
  Wakazi wa Ilaka Kota katika nyumba za NHC wamefukuzwa kama mbwa na kupewa fidia ya shilingi laki tatu baada ya kuwa wapangaji katika nyumba hizo kwa zaidi ya miaka arobaini.

  Nyumba hizo ambazo zilijengwa kwa ajili ya watu wa kipato cha chini sasa zimeamriwa zivunjwe kupisha maendeleo ya watu wastaarabu na kuwaacha masikini hao raia wa Tanzania wasijue la kufanya.

  Wanajamii, wanaharakati na taasisi za kushughulikia haki za binadamu angalieni suala hili kuona kama haki inakiukwa basi ipatikane kwa hawa wananchi masikini ambao walipewa fulana na t-shirt lakini sasa wananyanganywa moja ya hitaji kuu la banadamu ambalo ni malazi.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Viongozi wao wa kisiasa wanatoka chama gani katika eneo hilo?
   
 3. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  yaani ni wale Green and Yelo
   
 4. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,464
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Inaonekana wana taarifa ya kutakiwa kuondoka zaidi ya miezi nane sasa
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Waambieni waandamane hadi Ikulu kwa JK, muungwana atasikia kilio chao...
   
 6. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160

  Wakoje hao??????????????????
   
 7. KANUTI SILAYO

  KANUTI SILAYO Member

  #7
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  wana magari na kila mtu atakaa kwny geti lake,hawaombani chumvi wala kiberiti,upo
   
 8. domokaya

  domokaya JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2011
  Joined: Apr 22, 2010
  Messages: 3,129
  Likes Received: 1,252
  Trophy Points: 280
  Wakazi wa Ilala kota amboa ni wapangaji katika nyumba za Ilala experimental nao wanatarjiwa kufanyiwa kama walivyofanyiwa wenzao wa Dodoma kwa baadhi yao kuonyesha adhma ya kutotaka kuondoka baada ya kuwa wapangaji kwa zaidi ya miaka 41.

  Wakazi hao ambao wanaamini sheria za kiupangaji zinawapa haki ya kuwa wamiliki wa nyumba hizo wanatakiwa kuondoka baada ya kulipwa "huruma" ya shilingi laki tatu kwani NHC wanadai hawatakiwi kuwalipa wakazi hao chochote.

  Wakazi hao ambao waliomba kuuziwa nyumba hizo mwaka 2002 wameamriwa kuondoka kwa notisi ya siku 30 ambapo notisi hiyo iliandamana na barua ya kujibiwa kuwa ombi lao la kuuziwa nyumba limekataliwa na barua hiyo kurishwa tarehe nyuma na kuonekana iliandikwa mwaka 2003.

  Wanasheria haki, wapenda amani, wanaharakati na taasisi za haki za binadamu nawasihi chondechonde tujutokeze kuona haki ikitendeka kwa jamii hii masikini ya watanzania
   
 9. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Dah!Wacha tusubiri wanaoifahamu hiyo ishu kwa undani watufahamishe kama taratibu zilifuatwa ama kulikuwa na ukiukwaji!
   
 10. Somji Juma

  Somji Juma Verified User

  #10
  Oct 27, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,502
  Likes Received: 2,043
  Trophy Points: 280
  WAna taarifa miezi mi3 kabla.
   
 11. J

  J.K.Rayhope JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi juzi kulikuwa na zoezi kama hilo Mwanza,Arusha nako likawepo,Dodoma nako na sasa Mchikichini Dsm.Kote huko jeshi na serikali ya magamba wanatumia nguvu.Naamini kwamba licha jeshi na vyanzo vingine vya kulinda amani watumie mbinu nyingine za juu zaidi ya kutumia nguvu.Unakwenda kufukuza watu uko full guns,full bombs,full magari,full polisi wakati unaweza kupita nyumba hadi nyumba na utoe notice ya 24hrs,kweli baada ya muda nenda full greda,magamba sintokulaumu.Lakini wakati mwingine full magamba & full masaburi
   
 12. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,156
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Hii hali inabidi iendelee ili ifikie hatua watu wanyoke kwenye mstari wa kujitambua kifikira, hii itasaidia tumwagane vinyesi ili tujenge heshima iliyopotea
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  Wapangaji ni wapangaji tuu, mwenye haki ni mwenye nyumba. Sheria yetu ya upangaji ndio sheria bora kuliko zote duniani. Mwenyenyumba akiitaka nyumba yake, kwanza anakupa notice ya miezi mitatu ukae bure, ikipita, anatakiwa akutafutie nyumba ya kodi kama unayolipa mpangaji na yenye hadhi sawa, ndipo akuhamishe. Akikuta nyumba yenye hadhi sawa lakini kodi iko juu, basi mwenyenyumba huyo lazima aitop up hiyo kodi kwa miezi mitatu!.

  Wakazi hao wa Ilala ni wapangaji, nyumba sio zao, wamepewa notice ya miaka 8 wakikaa bure!. Wamepewa kodi ya pango ya nyumba za hadhi hiyo kwa miezi mitatu. Wamesaini mkataba wa hiyari wa kuhama, kwa ahadi kuwa wao ndio watapewa preference ya kwanza kuhamia kwenye nyumba mpya zitakazo jengwa hapo.

  Kusema ukweli, msiwasikitikie kufukuzwa kama mbwa, kwa sababu mpaka kodi za makazi mapya wamelipiwa!. Kitu cha kuwasikitikia na kuwahurumia ni changa la macho walilosainishwa eti wao ndio watakuwa wapangaji wa mwanzo wa hizo nyumba mpya!. Kama wamekaa bure miaka 8 bila kulipa kodi, hiyo kodi ya pango jipya kila mtu kalipwa kodi ya laki kwa mwezi, hayo majengo mapya, kodi yake itakuwa ni milioni kwa mwezi, hata wakipewa wao hiyo preference, wataweza kulipa?.

  Hilo ndilo changa lenyewe la macho, wamesainishwa kama wapangaji na wataendelea kuwa wapangaji only if kama wataweza kulipa. The good deal, walitakiwa wawe wabia katika mradi huo kwa mkataba wa kupatiwa nyumba moja moja kwenye hayo maghorofa mapya, jambo ambalo halikufanyika!.
   
 14. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #14
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Wakati mwingine ni vizuri kutumia nguvu kuweka heshima. Kama wanakaa hovyo au hawalipi kodi basi wacha watolewe. Maisha lazima ugharamie hata kwa wenzetu wameendelea kwa sababu wanalipia gharama za maisha
   
 15. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2011
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Lengo la kujengwa hizo nyumba pamoja na zile za magomeni ni ili kuwasaidia watu wa hali ya chini- na tuko wengi wa aina hiyo, sasa nyie miaka yote arobaini mmeng'ang'ania ndani ya hizo nyumba hamtupishi wengine kwa nini? Baadhi mmejenga majumba yenu maeneo mengine na mnapangisha watu kwa bei mbaya lakini hizi mziachii, wacha wabomoe zijengwe zingine za kisasa zitakazobeba watu wengi zaida!!!
   
 16. R

  Reasoning Member

  #16
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hivi ni wao tu ndiyo watanzania maskini wanaostahili kukaa kwenye nyumba za shirika la UMMA kwa zaidi ya miaka 40? Hivi maskini wengine tukifukuzwa kwenye nyumba baada ya kupewa notes tunapewa pia pesa za kupanga nyumba miezi mitatu? Hivi hizo pesa walizopewa wao ni mali ya nani na ni kwa nini ni wao tu wapewe na siyo sisi pia tulio watanzania wenye haki sawa na wao?
   
 17. B

  Bob G JF Bronze Member

  #17
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Inaelekea Watanzania wanaipenda hali ya kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao, Ilikua Dodoma hata wiki haijaisha haya yana mwisho haya....!
   
 18. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #18
  Oct 28, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  kuna watu wanafanya mambo ya kijinga kwa sababu wanajua tuna serikali dhaifu, hivi siku hayo magorofa/nyumba zilizochakaa zikiwashukia watasema hayo wanayosema?
  na kama hizo nyumba zingekuwa za tajiri mmoja hapa nchi wangelipwa fidia kuhama
  tu hache siasa makazi bora ni lazima yajengwe sasa kwa ghalama yoyote
   
 19. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #19
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu angalizo kwanza, zile nyumba si za NHC ni za halmashauri ya jiji. Nakumbuka kabla ya mradi huo kuanza wakazi wale walihakikishiwa kupewa priority katika upangaji wa mijengo hiyo mipya (something unrealistic) lakini kulikuwa na modality ya ni namna gani wakazi wale wangekuwa accomodated. Sasa inashangaza kusikia kwamba wamefukuzwa. Lakini hii haiwezi kutokea bila baraka za wakuu wa jiji. Zungu inabidi akomae nao hao lakini pia wananchi wakomae na huyu Masaburi. Nadhani ameamua kufanya safisha safisha, UDA sasa Ilala kota.
   
 20. A

  August JF-Expert Member

  #20
  Oct 28, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  nafikiri kuna mchangiaji moja kaeleza hapo mtu akikaa kupita miaka kadha basi sheria ina mpa haki ya kwanza kununua nyumba hiyo ikiwa nyumba hiyo ina uzwa, pili uingereza wana sheria ambayo inawapa haki squaters kuingia na kuishi kwenye nyumba ambayo mwenyewe hayupo au ana nyumba nyingi na hiyo alio kupangisha ni ya ziada au za ziada, na pia ukiwa mpangaji wa muda mrefu, halafu ukawa una shindwa kulipa mahakama itaangalia haki zako , na pia ujerumani kuna mthungu moja ana nyumba kadhaa ambazo hapati kodi kwani squaters wamw vamia nyumba zake na kuwatoa ni issue, na ndio maana nhc kwa kuwatia ujinga wamejaribu kuwapa hiyo tshs laki tatu kupoza mambo, lakini ikiwa nhc wanataka kufanya haki, kwenye hizo nyumba mipya si watatoa nyingi, yaani maflat, ya chumba kimoja, viwili, vitatu nk nk hivyo kwa hesabu rahsi kwenye nyumba 100 watatoa 300 kwanini hizo 100 wasiwape wapangaji wa zamani na hizo mpya 200 wapangaji wapya?
   
Loading...