mshikachuma
JF-Expert Member
- Dec 2, 2010
- 2,853
- 626
Sometime huwanawaza kwanini wakazi wa Dar-es-salaam tusiwe chachu ya mabadiliko tunayoyataka? Maana utakuta tunapiga
keleleweeee lakini mwisho wa siku tunaichagua ccm! Hasa wakazi wa ILALA na KINONDONI' kwanini jamani? Tumelogwa? Hakika
haiingii akilini tunazidiwa na hata watu wa mikoani na vijijini?
Tena huko watu ndiyo wamelala na hawana mwamko au mtazamo kama sisi wakazi wa Dar....iweje watu wanaokaa nje kidogo tu ya jiji letu kama Kawe, Ubungo na hata Tabata Segerea hawataki kusikia kitu kinachoitwa CCM, sasa inakuwaje sisi wakazi tunaoishi majimbo ya katikati ya mji (Ilala na Kinondoni) tumeichagua CCM kwenye ucha guzi uliyopita?
Yaani nadiliki kusema hata kesho itokee uchaguzi wa ghafla Kinondoni au Ilala kama ilivyotokea Igunga basi utaona watu wanaichagua
ccm kwa kura za kishindo!. jamani tatizo ni nini? tumelogwa na ccm hii iliyotunyonya kwa miaka 50 na kutulaza na giza kila siku?
Hebu tazama wakazi wa Mwanza,Mbeya,Arusha,Shinyanga mjini,Iringa, Lindi mjini,Moshi mjini na vijijini,Singida vijijini,Mbozi nk huko
kote hawataki tena kusikia kitu kinachoitwa ccm. Sasa iweje sisi tunaojiita wajanja wa mjini (wabongo) kila uchaguzi tunaichagua ccm?
Makao makuu ya Chadema yako jimbo la kinondoni lakini cha ajabu ccm ndiyo inatawala hapo. Makao makuu ya NCCR yapo Ilala lakini
cha ajabu ccm ndiyo inatawala hapo. Makao makuu ya CUF yapo Buguruni lakini cha ajabu ccm ndiyo inatawala hapo. Jamani kulikoni?
Yaani makao makuu ya vyama vyetu yapo milangoni kwetu na tunaona kabisa hawa viongozi wetu wa vyama vya upinzani jinsi wana
vyopambana na kutuelimisha....lakini bado mwisho wa siku tunaichagua ccm. Jamani wabongo tuna nini kwenye vichwa vyetu?
Mageuzi ya kuindoa KANU yalianzia Nairobi, mageuzi ya kumuondoa Keneth Kaunda na sasa Rupia Banda yalianzia Lusaka, mageuzi ya
kumuondoa Ghabo wa Ivory coast yalianzia Abdijani, mageuzi ya kumuondoa rais wa Tunisia yalianzia Tunisia, mageuzi ya kumuondoa
Mubarak wa Egypti yalianzia Cairo na mageuzi ya kumuondoa Gaddafi wa Libya yalianzia Tripoli na baadae Beghazi.
So kuna waliotoka kwa sanduku la kura na kunawaliotoka kwa kufukuzwa na wananchi. So all in all mageuzi yalianzia miji mikuu na kusambaa miji midogo.
Lakini kwa hapa Tanzania mambo ni tofauti kabisa! watu wa mji mkuu wamelala usingizi mfano wa pono....yaani wanatushinda hata wakazi
wa mikoani na vijijini? Hebu angalia kilichotokea Igunga' CCM imetokea kwenye tundu la sindano, chupu chupu ing'oke!
Yaani ilikuwa tia maji tia maji mtu (ccm) isikate roho pale Igunga. Je wakazi wa jiji la Dar ukiondoa Kawe na Ubungo, tuna matatizo gani? tumelogwa na CCM? Au kunatatizo ambalo limejificha mie sijui? Kwa nini tusiwe kioo cha mageuzi kwa faida ya watanzania wote?.
- Nawasilisha