Wakazi wa DAR, tumelogwa na CCM? Kulikoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakazi wa DAR, tumelogwa na CCM? Kulikoni?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mshikachuma, Oct 6, 2011.

 1. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Sometime huwanawaza kwanini wakazi wa Dar-es-salaam tusiwe chachu ya mabadiliko tunayoyataka? Maana utakuta tunapiga
  keleleweeee lakini mwisho wa siku tunaichagua ccm! Hasa wakazi wa ILALA na KINONDONI' kwanini jamani? Tumelogwa? Hakika
  haiingii akilini tunazidiwa na hata watu wa mikoani na vijijini?

  Tena huko watu ndiyo wamelala na hawana mwamko au mtazamo kama sisi wakazi wa Dar....iweje watu wanaokaa nje kidogo tu ya jiji letu kama Kawe, Ubungo na hata Tabata Segerea hawataki kusikia kitu kinachoitwa CCM, sasa inakuwaje sisi wakazi tunaoishi majimbo ya katikati ya mji (Ilala na Kinondoni) tumeichagua CCM kwenye ucha guzi uliyopita?

  Yaani nadiliki kusema hata kesho itokee uchaguzi wa ghafla Kinondoni au Ilala kama ilivyotokea Igunga basi utaona watu wanaichagua
  ccm kwa kura za kishindo!. jamani tatizo ni nini? tumelogwa na ccm hii iliyotunyonya kwa miaka 50 na kutulaza na giza kila siku?

  Hebu tazama wakazi wa Mwanza,Mbeya,Arusha,Shinyanga mjini,Iringa, Lindi mjini,Moshi mjini na vijijini,Singida vijijini,Mbozi nk huko
  kote hawataki tena kusikia kitu kinachoitwa ccm. Sasa iweje sisi tunaojiita wajanja wa mjini (wabongo) kila uchaguzi tunaichagua ccm?

  Makao makuu ya Chadema yako jimbo la kinondoni lakini cha ajabu ccm ndiyo inatawala hapo. Makao makuu ya NCCR yapo Ilala lakini
  cha ajabu ccm ndiyo inatawala hapo. Makao makuu ya CUF yapo Buguruni lakini cha ajabu ccm ndiyo inatawala hapo. Jamani kulikoni?

  Yaani makao makuu ya vyama vyetu yapo milangoni kwetu na tunaona kabisa hawa viongozi wetu wa vyama vya upinzani jinsi wana
  vyopambana na kutuelimisha....lakini bado mwisho wa siku tunaichagua ccm. Jamani wabongo tuna nini kwenye vichwa vyetu?

  Mageuzi ya kuindoa KANU yalianzia Nairobi, mageuzi ya kumuondoa Keneth Kaunda na sasa Rupia Banda yalianzia Lusaka, mageuzi ya
  kumuondoa Ghabo wa Ivory coast yalianzia Abdijani, mageuzi ya kumuondoa rais wa Tunisia yalianzia Tunisia, mageuzi ya kumuondoa
  Mubarak wa Egypti yalianzia Cairo na mageuzi ya kumuondoa Gaddafi wa Libya yalianzia Tripoli na baadae Beghazi.

  So kuna waliotoka kwa sanduku la kura na kunawaliotoka kwa kufukuzwa na wananchi. So all in all mageuzi yalianzia miji mikuu na kusambaa miji midogo.

  Lakini kwa hapa Tanzania mambo ni tofauti kabisa! watu wa mji mkuu wamelala usingizi mfano wa pono....yaani wanatushinda hata wakazi
  wa mikoani na vijijini? Hebu angalia kilichotokea Igunga' CCM imetokea kwenye tundu la sindano, chupu chupu ing'oke!

  Yaani ilikuwa tia maji tia maji mtu (ccm) isikate roho pale Igunga. Je wakazi wa jiji la Dar ukiondoa Kawe na Ubungo, tuna matatizo gani? tumelogwa na CCM? Au kunatatizo ambalo limejificha mie sijui? Kwa nini tusiwe kioo cha mageuzi kwa faida ya watanzania wote?.

  - Nawasilisha
   
 2. m

  mwelimishaji Member

  #2
  Oct 6, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unasema kweli lakini ujue wengine wanachagua ccm kwa kununuliwa. Wengine wanakuwa na wasiwasi kuwa baadhi ya vyama vya upinzani hawana upinzani wa kweli bali ni wapiga debe wa ccm kisirisiri.
  Jambo lingine ni la vijana kuupenda upinzani lakini kukosa kujiandikisha kupiga kura.
   
 3. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hatudanganyiki hii thread yakufikiria kwa njia za Masaburi. Dar yetu imetulia na katu chama pinzani hakiwezi igusa dar kwani wanajua ni moto.

  Kama unataka mageuzi hama Dar yetu na nenda uko utakako na watu km ww Dar hii mmehamia tu sio wakazi wa mji huu, ondokeni Dar mrudi makwenu.
   
 4. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mkuu mimi nipo jimbo la kawe...sehemu niliyopo iko pouwa kiaina..maji yanatoka hayakatikikatiki ovyo...miundo mbinu kama barabara zinapanuliwa kwa kasi na mambo mengine.....

  Lakini hata leo hii ukifanyika uchaguzi wa ubunge CCM haiambulii kitu hapa..sanasana kura zake zitapungua zaidi ya uchaguzi uliopita.....! Mimi nadhani sehemu zenye " Uswahili Uswahili mwingi" CCM huwa na mtaji mkubwa sana hata kama hao watu wa maeneo hayo hawapati huduma nzuri za jamii kama maji nk!
   
 5. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu GB mie najua kuwa wewe ni ccm kufa mtu,pia nahisi unacheo fulani ndani ya chama au serikali....so unataka kuniambia ccm itatawala milele?
  Hivi hujui kuwa waweza kuwapumbaza watu kwa mda tu na si siku zote? Je, huu upepo wa mabadiliko unauonaje? Na je mtauzuia mpaka lini?
   
 6. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,397
  Trophy Points: 280
  Tatizo ilala na kinondoni wahindi, waarab na mafisadi papa wanaishi huko,wanaogopa ccm ikitoka madarakani watakimbilia wapi?
   
 7. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu mimi nipo jimbo la Ilala....tena city center kariakoo na kuna miundombinu mibovu usipime! maji yanatoka kwa wiki mara moja tena ni usiku
  lakini watu wanaipenda ccm maeneo haya usipime! hata huwaelimishe vipi hawasikii!
   
 8. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  GreatThinkers,
  Tatizo la Dar ni lile kundi linaloyumbishwa na Si Si Em.
  Hilo kundi halina, lakini pia njaa kwa watu Dar imezidi.

  Watu hawajifikirii unaishi kwa kutafuta nauli na kula tu, ila unangoja dili la wizi ndio ujenge au ufanye kitu xha maendeleo.
  Nimekaa Dar miaka 15 naijua vizuri sana Temeke walianza Temeke miaka ie Mrema akawa Mbunge baada ya hapo ikawa kimya hadi hivi majuzi.

  Mnamkumbuka Kitwana Kondo 'KK' aliwatukana wanakigamboni kuwa niliwapa Pilau langu baada ya hapo Kigamboni ikamchagua Mbunge wa CUF?

  Tatizo la Dar ni njaa na watu kuwa Bize wakizani watapata unafuu wa Maisha, Maisha haya hayawezi kuwa nafuu bila huu mfumo wa kulindana kuuondoa.

  Niwape mfano mdogo: Hapa Mwanza kivuko cha Busisi Mkuu wa wilaya ya Geita ndiye aliyepewa tenda ya kuwa mama Ntilie ndani zile Feri mbili za Serikali?, Je, Mnafahamu nani kawakusanyia ushuru hapo Dar akiwa na Kampuni Tanzania Parking Solutions "TPS" ahaa Kinguge, na Je- wajua kwanini UDA imepigwa mnada, Je unadhani kuna nini wanataka kule kurasini? Yard Ya Makontena ili kina Masaburi wale Mihela!

  Siwalaumu, ila ngoja tutwasaidia kuwaondoa hawa wezi. Vijana tuliosoma baadhi tumerudi Kanda ya ziwa tuna mkakati wa kutosha kuiondoa Si Si Em na itaondoka 2015.

  2015 Wataiba kura lakini hazitatosha.
  Wilaya karibu zote za Shinyanga Si SI Em haina chake ispokuwa kuna sehemu moja inatatizo, nalo tumeshaliona Dawa yake inaandaliwa ili tuanze na uchaguzi wa mitaa kwanza.

  Tumewasukuma vya kutosha na sasa tumefika Igunga, huo ni koa wa Tabora ambao haujawahi kuwa na Mbunge wa Upinzani, Hivi majuzi it was neck to neck, Si Si Em mbinu yao tushaipata.
   
 9. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapa DAR waoga kweli wakiona tu gari la polisi mbio utadhani wako marathoni, sasa usiombe likapita gari lenye maji ya kuwasha watu hukimbia hadi soksi huvuka kiatu kinabaki. Mimi huwa nawashangaa sana utadhani huwa hawaogi.
   
 10. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  CCM wezi wa kura.
   
 11. Naibili

  Naibili JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,681
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  tatizo la dsm ni watu wengi ni washabiki tuu, nakumbuka wakati wa uchaguzi mkuu tulikuwa pale kariakoo, kuna mzee mmoja ni mwosha magari na mwingine ni mshona viatu ndo waliokuwa wakishabikia sisiem bila hata hoja ya msingi!
   
 12. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ona ulivyo potea kwenye ushabiki! Ubungo na kawe vipo wapi?!
   
 13. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Siku zote huwa nasema Dar ni tatizo kubwa, uelewa wa watu wengi wa dar upo chini sana, nakuhakikishia 60% ya wakazi wa dar ni mbumbu, hawajui chochote yeye ili mradi kala kalala basi kwisha kazi.
   
 14. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Usiwe na shaka, ni swala la wakati tu. Mimi nawaomba CDM waitishe maandamo hapa Dar kama walivyofanya Mwanza, hapo ndipo utakapoweza kusema kama Dar wanaipenda CCM ama vipi. Mimi nionavyo ni wizi wa kura tu ndio unafanya tufikiri kuwa ccm inapendwa dar.

  Makamanda leteni maandamano hapa dar, kama JK alilia ya Mwanza sasa ya Dar ataanguka kama Jangwani.
   
 15. d

  dotto JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tujiulize katika maeneo ambayo yana wabunge wa upinzani na yale ambayo yana wabunge wa ccm, uelewa wao ukoje? Na maanisha elimu dunia kwa ujumla ikoje?. Katika hili pia tuangalie jimbo la Segerea na Wizi wa mchana kweupe wa Kura.
   
 16. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vijana Dar wakijiandikisha kupiga kura CCM kwisha kazi na hilo limeonekana ongea na vijana mtaani wanajuta kutojindikisha mwaka jana wanaona ilikuwa inawezekana kabisa kuiondoa ccm kama wangepiga kura, na indicator ya igunga ni nzuri mno kwani wapiga kura walikuwa ni walewale wa zamani daftari halikuboreshwa,vijana wengi wana hasira ya kutojiandikisha 2015,no way CCM!
  Jimbo kama la Temeke ni aibu, mbunge wake ndo anayeongoza kwa masaburi. kawe na Ubungo wameonyesha njia naamini kabisa 2015 labda wapitishe sheria vijana hakuna kuandikishwa ndipo CCM itashinda bila hivyo,kwa heli magamba
   
 17. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Umesema kweli, muwe mnalinda kura zenu!
  Mbona Mwanza imewezekana?

  Your vote is your future, Linda kura yako.
   
 18. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Shauri yenu na Dar yenu kwa ambao hamtaki mabadiliko
   
 19. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Maeneo ambayo yamechukuliwa na CCM ni Ilala ambayo asilimia kubwa ya wakazi ni wahindi na waarabu na wasomali,pia Temeke kwa sehemu kubwa na Kinondoni.
   
 20. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2011
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  Tatizo la watu wengi wa mitaa hiyo na subutu kusema ni sawa na (vifuu Dume ) wanaeleweka ni watu wa starehe mmno na ndio maana utagunduwa wanadangayika kwa hara sana unapowatangulizia starehe kama vile nyama choma, pombe na hanasa za hapa na pale ijapokuwa maisha yao ni duni lakini wao hufurahia sana zile starehe wazionazo katika miji ya dar na kuambiwa Dar ndio Newyork ya Africa
   
Loading...