Wakazi wa Dar es Salaam wanatia aibu, je maisha yetu wakazi wa dar ni mazuri kiasi hicho? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakazi wa Dar es Salaam wanatia aibu, je maisha yetu wakazi wa dar ni mazuri kiasi hicho?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kasimba G, Apr 2, 2012.

 1. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,570
  Likes Received: 571
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha mji mkubwa kama Dar es Salaam, ambapo ilitakiwa kuwa kitovu cha mabadiriko ndiko haswa imekuwa ngome ya CCM, hivi ni kweli maisha ya wana Dar haswa eneo la Vijibweni maisha kwenu ni laini, hayawabani kama mbeya, Songea na sehemu nyingine nyingi hapa nchini?

  Kwakweli baada ya kupata matokeo ya udiwani vijibweni nimesikitishwa saana, watu wa mlo mmoja! bado watu wanaowasababishia hivyo mnawaunga mkono! Dar es salaam, kwa kweli inatia aibu, inasikitisha saana, tena saana. Maeneo ya vijibweni mimi nayafahamu vizuri, hivi ni kweli kabisa CCM wameshinda kwa aina ya maisha ambayo mnaishi nyie watu wa vijibweni?

  Yaani CCM is taking a very good care for you? Mnasikitisha!

  Nawasilisha
   
 2. N

  NewOrder JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 489
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Dar es Salaam ingekuwa ndio kitovu cha mabadiliko nchini kama miji mingine maarufu inavokuwa. Hali ya Dar ya huduma za barabara na miundombinu mingine ni sababu moja tosha kutaka mabadiliko. Kama majimbo ya vijinini kama Meatu, Kigoma Vijijini, Kasulu (si katika kudharau majimbo hayo) wanafanya mabadiliko - inakuwaje Dar wasione umuhimu wa hayo kupitia kashfa za UDA, Machinjio na uchafu mwingine mwingi???

  Siku Dar ikibadilika, nchi yetu itakuwa na nafasi kubwa kubadilika pia. Ndio maana ni wazee wa Dar tu ndio wana maana katika uendeshaji wa nchi!!
   
 3. m

  mzee wandimu JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 441
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mkuu! hawa jamaa wmeniudhi sana! yani sisi mikoani tumebadilika walio dar tulitegemea wawe msitari wa mbele kumbe hovyo! sawa sisi tumeamua kuchagua kilichochema! nyie komaeni na MAGAMBA YENU!
   
 4. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  tatizo la watu wa dar wanajiona kama wanaish ulaya kwasbb wanaambiwa ni mji uliojengeka kuliko yote, nawapa miaka 10 km hawajabadilika watajikuta wameachwa mbali sana na miji iliyokubali mabadiliko ya kisiasa.
   
 5. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Achana na hao wapuuzi wa kigamboni wapiga mbizi wakubwa wameongwa biliani waache waendeleze usultani na kucheza bao watakuwa nyuma na wasindikizaji.
   
 6. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,570
  Likes Received: 571
  Trophy Points: 280
  Hivi kwanza wameshinda kwa kura ngapi?
   
 7. O

  Olookule Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM wanashinda huko kwa kina YAKHE NA KILA KITU HEWALA na ndio tatizo kubwa la DAR MISWAHILI MINGI NA WACHEZA BAO PIA NA UNAFIKI MWINGI
   
 8. MwafrikaHalisi

  MwafrikaHalisi JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 1,746
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Vijibweni ni shamba kabisa mkuu usiskie Dar ukajua mjini. By the way, mabadiliko yanakuja taratibu. 2015 hatuwaangushi. Its a promise watu wamechoka sana huku!
   
 9. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,096
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Mkuu miaka kumi ni mingi mno! Kwa hesabu za haraka, tayari washaanza kuachwa!
   
 10. t

  torres0909 Member

  #10
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  Tatizo lililotea Vijibweni mgawanyiko wa kura baina ya CCM, CDM na CUF.

  CCM kama makadirio ya kura 1200
  CDm makadirio ya kura 800 na ushee
  CUF 700 na ushee kwa na pia watu wengi hawakupiga kura.
   
 11. Igabiro

  Igabiro JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Yaani pamoja na kuambiwa wapige mbizi bado vichwa vyao vimejaa upofuuu.....lakini nadhani zile kura za CUF ndio zimeinyima CDM ushindi
   
 12. Loy MX

  Loy MX JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 26, 2012
  Messages: 1,263
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  hapa dar kuna MAKANJANJA pia. Akili wamezikalia badala ya kuzifanyia kazi!!
   
 13. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Suala linaloifanya CCM ishinde si jiographia bali aina ya ubongo na itikadi za wapiga kura wa eneo husika. Huko vijibweni kama lilivyo jina lake ni uswahilini. Binadamu wa huko wanaongozwa na manung'uniko badala ya kuchukua maamuzi. Ni hao hao ambao juzi tu waliambiwa wapige mbizi na wao wakajiapiza na kulia kama wameonewa. Hata maisha yao magumu ni matokeo ya akili zao hizo hizo, kinachokera ni kwamba, maamuzi yao yanatuponza na wengine.

  Au nani anataka kuniambia the so called wazee wa dar es salaam hawajui kuwa kuna wazee wa iliyokuwa EAC wanadai mpunga wao na yule mhutubiaji wa vikao vyao anajua hilo lkn hajachukua hatua yeyote kuona wanalipwa?

  Uswahili ni mzigo mzito kuliko kodi ya kichwa ya mkoloni.
   
 14. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Dar es salaam itakuwa ya mwisho katika kupigania ukombozi wa kweli.
   
 15. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #15
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,727
  Likes Received: 1,634
  Trophy Points: 280
  Dar kweli hamnazo, tatizo uswahili mwingi, angalia sehemu ambazo hakuna uswahili kama kawe, ubungo jinsi watu walivyofanya kweli, kilichobaki ni kuwanunua wazaramo wote popote tuwaonapo
   
 16. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #16
  Apr 2, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Wenyeji wanaponzwa na umasikini wa fikra. Nilikuwa na jirani ccm wa kutupwa, alipewa T-shirt na doti ya kanga 2005 na akajisifia kweli kweli: "uchaguzi wa mwaka huu na mimi nimefaidi". Jioni hiyo hiyo mkewe akaja kwangu kuomba unga!
   
 17. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #17
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Pole pole na Waswahili mkubwa. Usinikumbushe machungu ya mikoa ya Tabora, Tanga na Pwani, ambayo haina mbunge mpinzani hata mmoja
   
 18. M

  Mukalunyoisa Senior Member

  #18
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nililalzimika kuichagua sisiem kwasababu tulitegemea Balozi Ngaiza angegombea bahati mbaya alifariki dunia RIP Balozi Ngaiza
   
 19. next

  next JF-Expert Member

  #19
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 601
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  dar haina historia ya kupinga, hapa kila kitu sawa tu, hata ukicheck historia utaona upinzani kwenye ukoloni ilikuwa mikoani,
  na hata ukisema uhuru ulipatikana dar ni baada ya watu toka upcountry kuja kichaji watu wa darisalama
   
 20. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #20
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,108
  Likes Received: 6,583
  Trophy Points: 280
  Watabadilika mdogo mdogo tu ccm bado kidogo itafutika ktk historia ya tz.
   
Loading...